Traffic / fire: Sticker za fire za station wagon kuuzwa 20,000, na saloon 5,000 why? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Traffic / fire: Sticker za fire za station wagon kuuzwa 20,000, na saloon 5,000 why?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elly-The Tishbite, Oct 29, 2012.

 1. E

  Elly-The Tishbite New Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni baada ya kupata usumbufu wa traffic polisi kudai sticker za fire pamoja na kuonyesha mtungi wa fire extinguisher niliamua kwenda kupeleka mtungi ule kukaguliwa ili nipate sticker. Afisa mkaguzi akaniambia nitoe 20,000 nikakumbuka mara ya mwisho nilikata kwa 5000. Nilipouliza kulikonimajibu ni kuwa magari ya station wagon ndio 20000 na saloon 5,000. Ukichunguza unakuta mitungi inayotumika ni size moja, uzito wa injini ni cc sawa, idadi ya passangers ni moja. Hoja hapa ni mamlaka ipi imepanga bei hizo za stika? na jukumu la serikali ni kufanya biashara au kutoa huduma? kuna act yoyote iliyoipa idhini Idara ya Zimamoto kufanya biashara hivyo? Mbona ukaguzi wa traffic polisi unaotoa sticker za Road Worthness ni tsh 3000/ ambazo kimsingi ni kama gharama za printing? Naomba ushauri kwa sababu nataka kuipeleka mbele zaidi-bungeni au mahakamani
   
 2. N

  Njaare JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Ninavyojua kwa sasa ukienda kurenew road licence unalipia na stika za fire. Kwa magari yasiyozidi CC 2000 unalipa 30,000/= na unapewa risiti na TRA. Ukitoka na risiti yako TRA unaenda nayo fire ukiwa na mtungi wa wako wa gas wanaukagua na kama wakiuona u mzima wanakupa stika bila malipo. Kama una matatizo wanautengeneza ila sijajua ni kwa gharama za nani.

  Sina uhakika kama huu utaratibu umebadilika tena ila najua umeanza kutumika toka julai mwaka huu.
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sticker haiuzwi ukienda lipa road license unalipia na mambo ya fire wenyewe watakagua extinguisher yako na watakupa sticker angalia usitapeliwe ndugu yangu .........................!:bowl::nimekataa
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Serikali ya CCM inatumia mbinu nyingi kuwakamua wananchi. Na hii ndiyo sababu umasikini hautaisha. Kodi hii ya mitungi na hata motor vehicle licence ni kero na ni namana nyingine serikali hii dhalimu inavyowakomoa raia wake maskini.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ndo sera ilivyo kwasasa lakini mkuu nikwambie kuwa hili halitekelezwi kwa mujibu wa utaratibu, nilikwenda kukata Road Licence, na baada ya hapo nikapeleka mtungi na hao jamaa wa TRA walinambia "kwasasa hatuna sticker njoo baadaye. Nimekwenda baadaye hola, nimekaa mwezi mzima na niliporudi hakuna. Juzi nimempeleka ndugu yangu naye akakate road licence na nkaulizia sticker za fire HOLA. Tangu 28 June 2012 hadi leo sijapata kabisa hiyo sticker. Mbaya zaidi polisi katika wilaya moja hapa nchini walikuwa wanakagua vyombo vya usafiri katika wiki ya nenda kwa usalama lakini hawakuwa na zile stickers za nenda kwa usalama. wizi mtupu na hii ninaisema kutokana na uzoefu wangu mimi mwenyewe!!!!
   
Loading...