Traffic barabarani wanatatua matatizo au wanayazidisha?

Guantanamoh

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
1,983
4,170
Habari ya Jumatatu mwananchi. Leo naomba tudiscuss kitu kimoja ambacho kimekua kinanisumbua sana kichwa. Hivi kiuhalisia, Askari Barabarani wapo kutatua changamoto au kuongeza. Nna incidents chache nnazoweza kuzitolea mfano.

Unakuta mtu amepata matatizo barabarani ghafla tu, gari yake imeanza kumharibikia akiwa barabarani anatanua apaki pembeni ili ajue tatizo traffic anakuja anamuandikia fine.

Incident nyingine, dereva wa gari la mbele anachezea simu huku anaendesha hivyo anayumba then wewe wa nyuma yake unampigia honi za kutosha ili akae sawa hasikii unahofia asije akakuletea matatizo unaamua umkwepe(overtake) traffic anakuandikia fine na anamwacha yule aliekusababishia kufanya hivyo. Sawa sheria zipo ila traffic wanajua kwamba kuna muda unaweza ukateleza kinyume na sheria ndogo ili kuepuka maafa makubwa.

Traffic wapo kutukomoa na sio kusaidia. Na unaweza kuta traffic anajificha kwenye nyasi ili akudake unajiuliza huyu ni afisa wa sheria au muwindaji?

MNAACHA KUTOA ELIMU MBADALA MNASHINDA KUSUBIRI WATU WAFANYE MAKOSA MWISHO WA SIKU HAMSOLVE TATIZO.

Na balaa lingine ambalo traffic mnalo nyie ndo sababu ya foleni maeneo mengi sana hapa DAR ES ALAAM. Siku unapita hukuti traffic gari zinaenda vizuri siku ukipita na traffic yupo anavuta eneo ambalo hata halina msongamano na kwenye watu wengi kuna baki na foleni kubwa. Ni kero kubwa sana hii. Traffic sio lazima wote mjae barabarani, angalieni sehemu zenye uhitaji wenu na ambapo hamhitajiki achieni Taa zifanye kazi yake.

Kuna maeneo unakuta traffic kasimama anasubiri watu wafanye makosa ila ukiangalia barabara ya eneo hilo ni kichefuchefu mfano barabara ya kitunda kwenda machimbo kuna siku nilipita nikishangaa kumuona traffic anapata nguvu za kuadhibu madereva nikasema huko wanakotumwa kufata sheria wanawapa na mirejesho kuwa huko kuna hali mbaya ya barabara?

Na lingine unakuta gari imesimama kwenye zebra ila apishe watu wavuke ile anataka kuondoa gari anatokea mvukaji mwengine anasimama, anataka tena kuondoa gari anatokea mwengine , au taa za kijani zimewaka na wavukaji nao wanataka kuvuka na traffic anaweza kukukamia kwamba ulitaka kumgonga raia.

Rai: TRAFFIC WEKENI KIPAUMBELE KWENYE UELIMISHA MADEREVA na HATA WAENDA KWA MIGUU

Na kwa kuongezea hapo, nimechunguza sana chanzo kingine cha foleni ni vituo vya daladala, kipindi hiki barabara zinatengenezwa naona ingekua vyema kama wangeangalia namna ya kuhakikisha vituo vinasogea metre chache ndani ili kuepusha madereva wa daladala kupakia abiria barabara kuu na kusababisha msongamano. Kama sehemu ina open space, pale kwenye kituo watanue kuelekea ndani( pembeni) ya barabara ili nafasi inayobaki huku isizue watu kuendelea na safari maana ukichunguza sababu za foleni kiuhalisia hazina msingi.

Wahusika fikirieni hilo swala
 
Fine za barabarani ni chanzo cha mapato cha serikali katili ya CCM.

kwa maana hiyo ni jukumu la traffic kuzidisha matatizo ili serikali ya CCM izidi kukusanya mapato umiza kwa wananchi wake wenye akili za makondoo.
 
Mara nyingi hawasaidii, wanaongeza foleni, maana huwa wanasimamisha sehemu zingine hazina parking or service road. Inakuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara.

Traffic huwa hawana muda kuelimisha. Wanapambana na makusanyo tu
 
Mara nyingi hawasaidii,wanaongeza foleni,maana huwa wanasimamisha sehemu zingine hazina parking or service road.....inakuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara...
Kuna siku kama miaka 5 hivi nyuma, nilishuhudia pale kisutu karibu na Mahakama, traffic alimsimamisha mtu ghafla wakati taa zimeruhusu yule mtu kusimama kumbe wenzake nyuma tayari walikua kwenye motion ya kuondoka kwasababu taa zimewaka, aisee ile kufunga brake mwenzie wa nyuma akamvaa, na wa nyuma akamgonga wa pili ikawa hivyo kwa gari nne!! Sijui nini kilifuata hapo ila sikupata majibu ya nlichokua nakiwaza akilini🙌🏽
 
Kuna siku utaelewa ni kwa nini mtu mweusi huwa hasogei hapo alipo,yaani tokea enzi za zama za mawe yeye yupo palepale!
 
Kuna siku kama miaka 5 hivi nyuma, nilishuhudia pale kisutu karibu na Mahakama, traffic alimsimamisha mtu ghafla wakati taa zimeruhusu yule mtu kusimama kumbe wenzake nyuma tayari walikua kwenye motion ya kuondoka kwasababu taa zimewaka, aisee ile kufunga brake mwenzie wa nyuma akamvaa, na wa nyuma akamgonga wa pili ikawa hivyo kwa gari nne!! Sijui nini kilifuata hapo ila sikupata majibu ya nlichokua nakiwaza akilini
Damn
 
Back
Top Bottom