TradeMark East Afrika, Yazindua Mpango Kamambe wa Women and Trade Drive Kuwasaidia Wafanyabiashara Wanawake wa EAC

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000


Nairobi, December 04th, 2017, By Pascal Mayalla Trademark East Africa launches women and trade drive.

Taasisi ya TradeMark, East Afrika, imezindua mpango kamambe uitwao Women and Trade Drive wenye lengo la kuwasaidia wafanyabiashara wanawake wa nchi 6 za Afrika ya Mashariki, ikiwemo Tanzania, kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa kwa kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, bara la Afrika hadi nje ya Afrika.

Mkakati huo, umezinduliwa na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa TradeMark East Africa,
Frank Matsaert, jijini Nairobi mwishoni mwa wiki ambao utahusisha kuwasaidia wafanyabiashara wanawake wa nchi 6 za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani ya Kusini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TradeMark East Africa Tawi la Tanzania, John Ulanga amesema, TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade” uliolenga kuwajengea uwezo wa wafanyabiashara wanawake kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa kwa kuanzia na wafanyabiashara wanawake wanaovuka mipaka ya nchi xa Afrika Mashariki

Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12.

TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kwa kuongeza fursa za upatikanaji wa masoko, kuboresha mazingira ya biashara, biashara ya ushindani na kuongeza mchango wa biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini kwa kuleta maendeleo na ustawi wa jamii.
interview  trademark, 1.JPG


TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com
Paskali
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Haya ni miongoni mwa mafanikio ya awamu ya tano kutokana na mazingira mazuri na wezeshi ya biashara yaliyokuwa set na serikali ya awamu ya tano chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo tarehe 28 October, do the right thing, mambo mazuri zaidi ya haya, yaje.
P
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom