TradeMark East Africa Yatenga Bilioni 12 Kusaidia Wafanyabiashara Wanawake wa Tanzania

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548

Tanzania, itafaidika na msaada wa Dola za Marekani Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania, zitakazotolewa na Taasisi ya TradeMark, East Afrika, kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata nje ya Afrika na kwa kuanzia, TradeMark, itaanzisha madawati ya jinsia kwenye mipaka mitatu ya Holili, Kabanga na Mutukula.

Ahadi ya fedha hizo, imetolewa na Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania, TWCC, kujadili vikwazo kwa wafanyabiashara wanawake mipakani, uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Ulanga amesema fedha hizo zitatolewa na TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade” uliolenga kuwajengea uwezo kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa.

Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12, kati ya hizo, Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, TWCC, kitapatiwa shilingi milioni 500.

Akishukuru kwa msaada huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Bibi Jaquiline Mneney Maleko, ameishukuru TradeMark kwa msaada huo, na kuahidi utatumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.

TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani.
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.

TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com

Paskali
TMEA PHOTO 1.jpg
John Ulanga 2.jpg
JOHN ULANGA 3.jpg
PICHA ZA PAMOJA.jpg
Washiriki 1.jpg
DSC_1514.jpg
DSC_1519.jpg
DSC_1526.jpg
DSC_1529.jpg
DSC_1533.jpg
DSC_1558.jpg
DSC_1556.jpg
DSC_1547.jpg
DSC_1539.jpg
DSC_1542.jpg
 
Sijui kama fedha hizo zitawafikia walengwa....maana serikali ya Huyu jamaa sina Ima.ni nayo....cc:KAGERA

Ovat
 
Pesa zote hizo kazi yake kubwa ni KUWAJENGEA UWEZO, miradi kama hii ni ndoto kafanikiwa, ni vyema pesa hizi kiwango kikubwa wapewe wajasiriamali direct kuboresha bidhaa zao etc.. Lakini utakuta pesa zote zinaishi kwenye consultant, warsha, makongamano. Wajasiriamali hawataki hayo wameshaattend Sana mengi tu. Wapewe fedha for packages etc
 
Back
Top Bottom