Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,441
- 113,450
Wanabodi,
Kwanza angalia, kisha ndio tuzungumze
Hii taasisi ya TradeMark East Africa, (TMEA), ambayo siku zote imekuwa ikifanya mambo makubwa kimya kimya, imeendelea kufanya makubwa nchini kwetu Tanzania. Safari hii kupitia Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, wamewachukua wanawake wafanya biashara zaidi ya 200, wakawapiga semina elekezi ya jinsi ya kufanya biashara, wakawapaisha mpaka nchini China, kwenda kuwaonyesha wanawake wenzao wa Kichina wanafanya nini, kisha wakawarudisha nchini, wakawapa mafunzo ya kutengeneza bidhaa bora, wakawapatia nembo za ubora za TBS na Barcode, na kuwapa mitaji ya kuanzisha biashara, kisha wakati wa maonyesho ya Saba Saba, wakawadhamini kuonyesha bidhaa zao, ambazo sasa zina ubora wa kimataifa, na hawakuishia hapo, sasa wanawasaidia kuzitangaza bidhaa hizo, na kuzitafutia masoko ya kitaifa na kimataifa. Watanzania sijui tupewe nini?.
Soma na kushuhudia mambo ya TIMEA kupitia TWCC
Mungu Awabariki Sana Hawa Jamaa