TRA yawaomba viongozi wa dini kuhamasisha ulipaji kodi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,803
4,467
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi (TRA), Richard Kayombo amewaomba viongozi wa Dini kuhamasisha ulipaji wa kodi nchini huku akidai asiyetoa risiti ana nia ya kijidhulumu yeye na Serikali yake na wananchi wenzake na atawachelewesha kwenye masuala ya upatikanaji wa huduma za kijamii.

Kayombo ametoa kauli hiyo jana jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye mkutano wa Amani wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania wenye lengo la kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuongeza kasi ukusanyaji mapato.

Kayombo amesema asiyetoa risiti ana nia ya kijidhulumu yeye na serikali yake na wananchi wenzake na atawachelewesha kwenye masuala ya upatikanaji wa dawa, barabara za lami, maji, umeme.

Mkurugenzi huyo amesema serikali imeleta jambo zuri la wananchi kudai risiti kila wanapofanya manunuzi lakini kuna changamoto ya wengi kutodai.

Aidha, amewaomba viongozi hao kupaza sauti zao kwa upole, kuhamasisha watanzania watekeleze wajibu wao wa kulipa kodi wakati wa mahubiri kwenye nyumba za ibada.

“Nichukue fursa hii kuwaomba viongozi wangu wa dini mliopo hapa na mahali popote nchini usitoke bila kudai risiti, zungumzeni na waumini kupitia mahubiri kuhusu umuhimu wake ili kuwepo ukadiriaji kwa haki,”amesema Kayombo.

Pia, alieleza kuwa nchini kuna ukanda mrefu wa bahari, maziwa na kumepakana na nchi nane, hivyo kuna vichochoro vingi vya magendo ambavyo vinanufaisha baadhi ya watu na kusababisha ukusanyaji mapato kutoongezeka wakati lengo la kufikia zaidi ya Sh trilioni 3 lipo.

Kayombo alifafanua kuwa suala hilo likiendelea kuna athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo bidhaa zinazoingia kupita sehemu isiyo sahihi kwa kutofanyiwa ukaguzi na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) zinazoweza kuathiri afya za watanzania.

“Lakini kuna hatari nyingi kama silaha haramu, madawa ya kulevya ndio maana sisi kama TRA kazi yetu si kukusanya tuu bali kudhibiti bidhaa haramu zinazoweza kuingia nchini na kuvuruga amani,” amesema.

Naye,Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutumia viongozi wa dini kuelimisha waumini na watanzania kuhusu umuhimu wa kupa kodi.

Chanzo: Mtanzania
 
Viongozi wa dini wanakusanya ya Mungu, japo haifiki alikokusudia. TRA wakusanye ya Kaisari.
Wote wanamtegemea mtu mmoja atoe. Akitoa nyngi kwa Kaisari anapunguza ya kutoa kwa Mungu!
 
Back
Top Bottom