TRA yavunja rekodi ya makusanyo ya mwezi Desemba 2020

Darasa nilijenga mwaka 2014 kabla ya wapenda sifa kuingia madarakani, na darasa halikuvuka 6m, nililipa vijana wakachoma matofali, pickup yangu ikabeba hayo matofali. Mbao za kupaua zilikuwa za mnazi bei karibu na bure. Water tank la lita 5,000 nilinunua kwa 720,000, kusafirisha pamoja na guter, gharama nzima mpaka kulifunga haikuzidi 800,000. Na sasa nawasaidia wanafunzi 10, 7 wakike na watatu wavulana uniforms na madaftari, maana elimu ni bure. gharama zote hizo hazifiki 1m. Inaonekana hujui bei za vitu boss. milioni 40 ni nyumba self contained yenye room 3 za kulala na garden ya kuweka mbogamboga. water tank la shilingi 2m ni la lita 10,000.
Nashukuru mkuu kwa kuwa umetambua umuhimu wa Sera za CCM kwa watoto maskini kwenye bold kwa Elimu kugharimiwa na Serikali ya Awamu ya Tano!
 
Unaamanisha mboe ameanza tena kuuza?

Ila ajue laana ya kuharibu vijana wa watu itamwandama

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
Kuna ule unga alikamata makonda akampa Le mutuz kubwa jinga akauze China ndiyo wameuzungusha hapo Nchini, ebu anza kuwakemea maofisa wa TRA vinara wa Rushwa ambao ni mabingwa wa kufunga biashara, Account na kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kwa njia haramu za kishetani kwanza,
 
Takukuru anzeni kuwachunguza maofisa wa TRA ambao ni vinara wa kufunga biashara, Account kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kwa njia haramu za kishetani kutengeneza mazingira ya Rushwa, Serikali inakosa mapato biashara zinayumba kisa wafanyabiashara kufungiwa Account zao na baadhi ya maofisa wa TRA ambao siyo waaminifu wenye roho mbaya
 
Watumishi wanatunyonya Sana, yaani karibia nusu ya pato kwa mwezi wanachukua wao, na bado wanadai nyongeza,

Sioni kama Taifa namna tunaweza fanya maendeleo kama kipato almost chote tunalipana mishahara tu.
Lengo la kazi yoyote ile ni kukusanya makusanyo ili uyatumie katika shughuli zako kwa 10% na shughuli za kimaendeleo kwa 90% sasa hapa tunakusanya halafu tunalipana kwanza 40% ELEECTRONIC DEVICES NDIO SULUHISHO SUALA HILI HATA ULAYA LILIWAHI KUWAPA TABU SANA
 
Ni kweli mkuu,

Uchumi wetu bado tunategemea movement ya pesa physically, ni ngumu kukusanya mapato stahiki.

Kama tukianza kuwa na electronic devices itakuwa rahisi Sana kukusanya mapato.

Tatizo jingine nalo bado kuna watu hata akaunti tu hawana.
 
bil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
Wabunge pekee kwa salary ya 12,000,000 per month wanatumia karibia 10 bilioni... Hawa ingetakiwa salary yao basic iwe only 2 million.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ipo haja ya serikali ama kupunguza mishahara ama kupunguza wafanyakazi pesa zinazotumika kulipia mishahara tu ni nyingi Sana.
Mkuu 600 bilioni ni pesa ndogo sana, hiyo ni pesa ya dream liner moja tuu. Tatizo kubwa ni ukusanyaji mdogo wa mapato, imagine kwa jinsi tulivyo na rasilimali za kufa mtu kuanzia ardhi nzuri na kubwa ya kilimo, mito na maziwa, bahari, misitu na mbuga za wanyama, madini etc halafu tunakusanya only 2 Trilioni? Sisi ilitakiwa kwa mwezi tukusanye zaidi ya 5 Trilioni...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwenye takwimu pekee ndio uchumi unapopanda
Halafu wanasema wamevuka lengo wakati walipoliweka hilo lengo hawakuja publically kutuambia kwamba lengo la Disemba ni X, lengo la January ni Y etc.... Mfano lengo la makusanyo ya January to March (robo ya kwanza) hawajatuambia kabisa ili kuweke hiyo record...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Takukuru anzeni kuwachunguza maofisa wa TRA ambao ni vinara wa kufunga biashara, Account kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara kwa njia haramu za kishetani kutengeneza mazingira ya Rushwa, Serikali inakosa mapato biashara zinayumba kisa wafanyabiashara kufungiwa Account zao na baadhi ya maofisa wa TRA ambao siyo waaminifu wenye roho mbaya
Acha ufala kijana.. hakuna mtu amefungiwa account bila kufuata sheria. Ukiona account zako zinafungwa ujue umeshindwa kulipa kodi kama mlivyokubaliana. Ujue TRA wanaweka mpaka mikataba ya namna gani mtu atalipa kodi yake aliyolimbikiza ikiwa kila mwezi apeleke kiasi fulani so ukiona akaunti inazuiliwa na kwamba umekiuka mkataba ule. Hali hiyo ipo hata benk ukichukua mkopo wanauza vitu vyako hivyo kwa TRA wao wanazuia akaunti zako zote na wanakomba pesa zao wanazodai kisha mnajengewa flyover mnapita na maguta yetu. Jinga kabisa ww
 
NAONA hujui kuanaluse trend ya mapato ya kodi..Jua kuwa miezi ya march..june..sepr na dec mapato ya kodi huwa juu kwani wafanyabiashara wanalipa zaidi kuliko miezi ya kawaida.Kwa maana hiyo usichukue maoato ya Dec kama average ya mapato kwa miezi ijayo..JITAHIDI KUSOMA ILI USITOE MICHANGO KAMA KILAZA

Leo 01/01/2021 mamlaka ya mapato Tanzania kupitia kwa waandishi wa habari, imetangaza makusanyo ya mwezi Disemba 2020 kuwa ni takribani trilioni 2, hii ni rekodi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hii mwaka 1996

Hi ni hatua ya kupongezwa sana kwa watanzania wote walipa kodi na mamlaka ya mapato nchini, kukusanya trilioni 2 kwa mwezi( Disemba) ni jambo lenye kutia moyo sana kwa sisi wananchi

Nilikuwa napitia mapitio ya uchumi ya kila mwezi( Monday Economic Review) kutoka benki kuu yetu( BOT) kwa mwezi Disemba 2020

Ripoti hiyo ya Disemba, inaonyesha kwa mwezi October pekee, 2020, serikali ilikusanya takribani trilioni 1.682, hii ni jumla ya makusanyo yote ya kikodi( Tax Revenue) na yasio ya kikodi ( Non Tax Revenue)

Ambapo kwa mwezi huo wa October 2020, makusanyo ya kikodi( Tax Revenue) pekee yalikuwa ni trilioni 1.295 , na makusanyo yasio ya kikodi( non tax revenue) yalikuwa ni bilioni 282.2 na makusanyo kutoka local government ( own source ) yalikuwa ni bilioni 51.2

Lakini tukienda kwenye matumizi ( Government Expenditure) kwa mwezi October 2020, ripoti hiyo( Monthly Economic Review) inaonyesha kuwa serikali ilitumia takribani trilioni 1.854

Ambapo matumizi hayo yalikuwa ni kama ifuatavyo, kwenye matumizi ya kawaida ( Recurrent Expenditure) ilikuwa ni trilioni 1.282 na matumizi kwenye miradi ya maendeleo ( Development Expenditure) ilikuwa ni bilioni 571

Ambapo matumizi makubwa zaidi kwenye serikali yanakwenda kwenye mishahara( wages bills) za watumishi wa umma, kwa mwezi October serikali ilitumia takribani bilioni 601.7 kulipa mishahara kwa mwezi mmoja tu

Na pesa nyingine inatumika ku service madeni yetu( Debt expenses), ambapo kwa mwezi October pekee, serikali ilitumia takribani bilioni 192.4 kulipia interest ya madeni yetu ya nyuma na sasa

Kwa maana hiyo kwa mwezi October 2020, serikali ilitumua fedha nyingi zaidi( trilioni 1.854) kuliko pesa tulizoingiza(trilioni 1.628) kwa mwezi( budget deficit)

Kwa hatua ya leo ya mamlaka ya mapato kukusanya trilioni 2, kama itaendelea hivi hivi kila mwezi, maana yake ni kwamba serikali tunakwenda kuwa tunaingiza/ kukusanya fedha nyingi zaidi kuliko matumizi yetu kwa mwezi

Hii itasaidia sana kwa nchi yetu kupunguza mzigo wa kuendelea kukopa mikopo ya bei nafuu( concession loan) kutoka kwenye multilateral lending institutions au mikopo ya kibiashara( non concession loan) kutoka kwenye mabenki ya kibiashara duniani

Kongole kubwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania 👏👏👏

Ngamanya Kitangalala Mwaswala kngamanya@yahoo.com
0756 669494
bil 600 ni pesa nyingi mno katika kulipa mishahara hapa ni lazima ubuniwe utaratibu wa namna wa kulipunguza hili wataalamu wabobezi wakisaidiwa na wa nje wakae chini waone ni jinsi gani tutatumia ELECTRONIC DIVICES kukusanya zaidi na kupunguza watumishi ambao shughuli zao zinaweza kufanywa na vifaa vya kikompyuta automatically
MKUU UNASEMA SERIKALI IPUNGUZE WAFANYAKAZI WAKATI WATU WANASUBIRI SERIKALI IWAAJILI WALIOKO MTAANI
 
Acha ufala kijana.. hakuna mtu amefungiwa account bila kufuata sheria. Ukiona account zako zinafungwa ujue umeshindwa kulipa kodi kama mlivyokubaliana. Ujue TRA wanaweka mpaka mikataba ya namna gani mtu atalipa kodi yake aliyolimbikiza ikiwa kila mwezi apeleke kiasi fulani so ukiona akaunti inazuiliwa na kwamba umekiuka mkataba ule. Hali hiyo ipo hata benk ukichukua mkopo wanauza vitu vyako hivyo kwa TRA wao wanazuia akaunti zako zote na wanakomba pesa zao wanazodai kisha mnajengewa flyover mnapita na maguta yetu. Jinga kabisa ww
Wewe mbweha ndiyo uache ufala tena wewe inaelekea ni mbumbumbu juha zuzu mnufaika wa udhalimu uonevu unyanyasaji wa TRA kwa wafanyabiashara, kwa taarifa yako TRA hawafuati Sheria wanafunga Account kienyeji tu kuwakomoa watu na wengi waliofungiwa Account wana Tax Clearence safi kabsa, lakini kwa ufala wako mnaamua kuwakomoa wafanyabiashara matokeo yake mnadhiathiri benk kwa kukosa kuaminika na kuonekana si sehemu salama ya kutunza pesa za wafanyabiashara, wewe utakuwa ni mnufaika wa huo usumbufu kwa wafanyabiashara ndiyo maana unatetea upumbavu wa kufunga Account za watu kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetani
 
Flyover siyo Hisani za CCM ni pesa inatakiwa ipatikane kwa uhalali siyo kuwabambikia kodi kufunga biashara Account za watu kienyeji kwa njia haramu za kishetani kutengeneza mazingira ya Rushwa
 
Wanufaika wa Rushwa na uonevu unyanyasaji wa TRA kwa wafanyabiashara sasa naona wameamka kuja kutetea upumbavu wao wakiamini watanzania wamelala watakubali ujinga wao
 
Wewe mbweha ndiyo uache ufala tena wewe inaelekea ni mbumbumbu juha zuzu mnufaika wa udhalimu uonevu unyanyasaji wa TRA kwa wafanyabiashara, kwa taarifa yako TRA hawafuati Sheria wanafunga Account kienyeji tu kuwakomoa watu na wengi waliofungiwa Account wana Tax Clearence safi kabsa, lakini kwa ufala wako mnaamua kuwakomoa wafanyabiashara matokeo yake mnadhiathiri benk kwa kukosa kuaminika na kuonekana si sehemu salama ya kutunza pesa za wafanyabiashara, wewe utakuwa ni mnufaika wa huo usumbufu kwa wafanyabiashara ndiyo maana unatetea upumbavu wa kufunga Account za watu kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetani
We ni mpumbavu hakuna mfanyabiashara amefungiwa account bila taarifa. We hujui lolote ni mpiga kelele kama mafala wengine. Watu wanahangaika kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana au umesikia akaunti zikifungwa hizo pesa zinaenda mifukoni mwa maofisa wa TRA? Ficha upumbavu wako mara moja. Kama unadhani TRA wanakula RUSHWA kawakamate sio unaingiza wivu wa kike mbweha wewe. Yani watumishi wa TRA wasiwe na maisha mazuri basi rushwa acheni uboya. Mishahara yao mizuri mazingira ya kazi sehemu nyingi mazuri kwann wasiwe na maisha mazuri? Acha wivu wa kike UT@0MBWA. Kila siku kusema vibaya TRA wakati mnalalamika hudumu za jamii mbovu. Hao takukuru hutegemea hizo kodi walipwe vimishahara vyao mbuzi. Huwa nikiona mtu anawakatisha tamaa TRA namuona boya kweli. Kila siku watumishi wasiowaamifu mara hivi. Wakitoa tangazo la kazi nenda kaombe na ww uwe mtumishi wa TRA.
 
Wafanyabiashara wengi hawataki kuweka pesa bank kwa hofu ya pesa zao kunyemelewa na TRA kuwabambikia kodi kubwa kisha kufunga Account zao kienyeji, tunapokwenda mbele mabenk yatafirisika kwa kukosa wateja baada ya wafanyabiashara wengi kuhamishia pesa zao kwenye mabenk ya nje na Nchi Jirani kukwepa kuporwa kienyeji na TRA
 
Back
Top Bottom