TRA yashinda kesi ya Tshs bil 38 dhidi ya VIP ya Rugemalila

Utatu

JF-Expert Member
Dec 31, 2008
436
183
TRAB wameitupilia mbali rufaa ya VIP kupinga malipo ya kodi ya ongezeko la thamani kwenye dili lao la kifisadi na PAP. Hili dili ndio bado linawanyonya watanzania vibaya sana hadi leo hii.

Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited ilikata rufaa kwenye bodi ya rufaa ya mapato(TRAB) dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuzidishiwa kodi ya dola za kimarekani 23,629,434.75, baada ya kuuza hisa zake kwa IPTL.

Katika rufaa iliyokuwa imewasilishwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kampuni ya VIP iliitaka bodi hiyo kuifuta hiyo kodi na kuiamrisha mamlaka TRA kurudisha dola za kimarekani 17,980,934.75.

MY TAKE: Je kesi yake ya kufisadi viongozi waandamizi wa serikali ya CCM na jamii, ni vipi mzee Mlowola wa Takukuru hapo umekaa mkao wa kula nao sahani moja?
 
Yaani mtz mmoja anadaiwa pesa hiyo yote? Sasa watanzania hawako sawa, hiyo kodi tu, kabakiwa na ngapi?
 
Safi sana...huu ni ujumbe tosha kuwa judiciary system imezaliwa upya na imejipanga kutetea "wengi"
  1. JPM anawatisha, akimaliza kutumbua, awafunge tu hakuna jinsi.
  2. Wakati majizi yakiwa ndani arekebishe taasisi zetu.
  3. Halafu atuletee katiba ya wananchi.
  4. Halafu aende zake, akachukue Tuzo ya Mo Ibrahim.
 
Hiyo kesi naamini itafika mpaka mahakama ya rufaa, Mzee Ruge ni mbishi kama roho ya paka!
 
Hongera Magufuli...!! Judges wametoa hukumu halali, ingekuwa enzi za mzee wa Msoga, hii kesi Ruge angeshinda kwa kucheka tu..!!
 
Back
Top Bottom