TRA yakusanya Trilioni 7.27 kwa kipindi cha miezi 6

sechex

Member
Aug 24, 2016
84
39
TRA imetangaza makusanyo yake kwa kipindi cha miezi 6 ni trilioni 7.27 kwa 2016/2017 ukilinganisha na trilioni 6.44 ya mwaka 2015/2016.

Kwa mwezi Disemba 2016 TRA ilikusanya trilioni 1.41.

=======

MAKUSANYO YA KODI KIPINDI CHA NUSU MWAKA WA FEDHA 2016/17


Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.

Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.

Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
Screenshot from 2017-01-17 15-42-21.png

Jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.

TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.

Pamoja na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.

TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.

Kwa wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.

Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .

Pamoja Tunajenga Taifa Letu’

17/01/2017

Richard M. Kayombo

MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
 

Attachments

  • PRESS+RELEASE+-Makusanyo+Desemba+2016.doc
    198 KB · Views: 88
Trilioni 7.27 kwa miezi 6.Makusanyo kwa mwaka tunakadiria 14.54.
Bajeti iliyopitishwa 2016/2017 ni 29.5. Deficit 29.5-14.54 baki 14.9 trilioni. Naona tuko katika hali ngumu kiasi sasa tunahitaji 'usalama wa raia' washiriki kuwakamua wenye magari na madereva. Mwisho wa siku tunagawana faida na serikali.(Hasa gari za biashara roli,daladala,basi,bajaji nk)
 
Trilioni 7.27 kwa miezi 6.Makusanyo kwa mwaka tunakadiria 14.54.
Bajeti iliyopitishwa 2016/2017 ni 29.5. Deficit 29.5-14.54 baki 14.9 trilioni. Naona tuko katika hali ngumu kiasi sasa tunahitaji 'usalama wa raia' washiriki kuwakamua wenye magari na madereva. Mwisho wa siku tunagawana faida na serikali.(Hasa gari za biashara roli,daladala,basi,bajaji nk)
Mkuu hayo ni makusanyo ya TRA tu, serikali ina vyanzo vingi vya mapato tofauti na kodi.
 
Hivi na za trafiki zimejumlishwa hapo!? Maana wengine wanaziitaga forced labour nasi twaiita forced taxes.
 
Back
Top Bottom