TRA yaikadiria ACACIA deni la Tsh. Trilioni 425.4 kama Malimbikizo ya Kodi

1. kama haipo kwenye sera ya CCM inakuwaje, ESCROW,KAGODA, MEREMETA,RADA, NETPROOF,MIKATABA MIBOVU, nk inakuwaje vilitokea na wahusika wapo na wanajulikana na wengine ni wafadhiri wa chama, wengine wabunge kupitia chama husika lakini hakuna hatua walizochukuliwa??..
2.IKULU,TRA,TISS.TANROAD, TCRA,TAA,POLISI,TPA,TMAA nk hazina miongozo yakuhakikisha wizi unatokea kifupi kazi yao ni kutenda majukumu yao kulinda maslahi ya taifa na wizi usitokee, - walishindwaje kulinda maslahi ya Taifa na wizi ukatokea? kifupi walishindwa kutekeleza majukumu tuliowapa hivyo wanastahili adhabu.
3. Kwanini waliweza kutudanganya na hapa ni kwetu, madini ni yetu na serikali ni yetu?.. Kama waliweza kutudanganya na tukaingia mkenge na wakatutia hasara kubwa - kuna haja gani ya Taifa hili kuwa na Serikali sasa kama mtu anaingia kienyeji na kufanya atakalo?..
4. Uzalendo hauhisiwi, Uzalendo ni vitendo pale muhusika anapokuwa sehemu husika, ni wapi tuliwaamini tukawapa nchi wapinzani wakashindwa kuonyesha uzalendo wao?, Wazee wetu waliamua kumuamini Nyerere na kumpa nchi wakiwa hawajui kama ni mzalendo au sio, kwa bahati hakuna kipimo cha uzalendo duniani kwa mtu ambaye hujampa nafasi ya kuonyesha uzalendo wake, kiuhalisia walioshirikiana na ACACIA kwa 90% wako CCM maana ndio waliokuwa na mamlaka na mamlaka ya kusaini mikataba ya hovyo ambayo leo tunaipigia kelele na kujiita wazalendo tunapoipigia kelele..Kati ya hao na Chama kilichopo madarakani ni nani anakusanya hela nyingi??? na je ameweza kutatua matatizo muhimu toka 1961???
Uzalendo sio chama ni hullka binafsi ya mtu. Ufisadi pia sio chama ni tabia na tamaa za watu wachache walopewa madaraka. Na watu hao wako kila chama, kila dini, kila kabila. Ndio maana wale wajiitao wana demokrasia (isiyokuwepo hata chembe), walifuta agenda ya ufisadi baada ya kuwa mwambata na fisadi papa.
 
Nimeishia kucheka tu

Kampuni haijasajiliwa ila inapokea assessment ya kodi. Kampuni hewa ila TRA wana data zao.


Acacia Mining pays 120 billion/- in corporate tax 2016- Acacia Mining pays 120 billion/- in corporate tax


Kinachoniuma hapa ni kuwa watz tunapumbazwa na propaganda za makinikia wakati kitu pure kinapaa na ndege. Kama kuibiwa ni kweli tumeibiwa na tunaendelea kuibiwa kwa hisani ya usanii wa CCM.

$190billion ni kama 420trilion Tsh. Hii ni budget ya TZ miaka 13. Kama walikuwa wanalipa kodi isiyozidi 10% inamaana hawa jamaa walikuwa wametengeneza zaidi ya $900 billion from Tanzania ndani ya miaka 17. Na hapa acacia ni branch tu ya Barrick. Hii pesa tungekuwa tunalipwa, hivyo basi kodi ya Acacia ingetosheleza kufinance budget yetu ya miaka 13 iliyopita. Yani Watanzania tungekuwa hatulipi kodi wala kuomba mkopo. Yan ni kupokea kodi tu toka acacia na sisi tungekula tu bata. Pia usisahau kuna Migodi mingine mikubwa kama ishirini.
8db4829c43c06d8b06ad4fe19c6f3bf2.jpg


Kumbuka pia acacia ni moja tu ya Gold mine company in Tanzania. Kuna mgodi mikubwa unaomilikiwa na AngloGold& Ashant kama bonge la openi pit lile la "Geita Gold Mine(GGM)' lililoanza operation toka mwaka 2000. Kwa pesa tunayowadai acacia, kama Geita Gold mine nao wangekuwa wanalipa kodi iyo, bac Tanzania ingekuwa na uwezo wa kupokea zaidi ya $15billion kutoka katika iyo migodi miwili tu. Hata budget yetu tungekuwa tunaongelea zaidi ya Trillion 50 kwa mwaka.

Ki uhalisia, GGM kodi yao haifiki $300m kwa mwaka. Mwaka 2013 GGM walipokea award kutoka TRA kwa kuwa the best tax compliance company in tanzania. Ambapo mwaka 2013 walilipa cooperate tax ya $213.8m 123Tanzania Quiz.
Nakumbuka mwaka 2015 GGM walivyopandishiwa kodi kufikia 4% kwa mraba kulikuwa na utata kidogo maana ilikuwa walipe karibu $200m kwa mwamka ila acacia ndyo waliokuwa wakwanza kukubali kulipa ndipo GGM na wengine wakafyata mkia.

Sasa kama GGM kodi yao haifiki $300m, inakuaje Acacia ndyo wanatakiwa kulipa mara 20 yake kwa mwaka? Yani zaidi ya $4b kwa mwaka na hapo bado penalty!!!!!!!!!!

Labda ACACIA uzalishaji wao ni mkubwa kuzidi GGM, Ila probable gold reserves and other resources katika migodi mitatu ya acacia(north Mara, buzwagi na bulyanhulu) haizidi 22m oz. Na average production per year haizidi 700,000 oz per year kutoka kwenye migodi mitatu. Geita gold mine mwaka 2015 iliweza vunja record na kuzalisha 527,000 oz of gold. Ambapo kodi ilikuwa around $200m.

Ikiwa kweli acacia wanatuibia na iyo ndyo pesa wanayopaswa kutulipa, basi hata na GGM wanatuibia sana sambamba na migodi mingine.

466349f6eb07d7cc7646bff5abb4c811.jpg


Tanzania ni nchi ya 4 duniani kwa kuzalisha Gold. Tanzania imekuwa ikizalisha Gold yenye value isiyozidi $1.5billion kwa mwaka. Ila kwa kodi tu tunayoidai acacia ni kuwa mgodi mmoja uliweza kutoa gold yenye thamani zaidi ya 10b.

Hapa ndipo napozidi kucheka kabisa maana kodi tunayowadai acacia($190b), ingekuwa ndyo sisi tunajichimbia, iyo pesa ingepatikana ndani ya zaidi ya miaka hata 200 baada ya kutoa operation costs.

South Africa ni nchi inayoongoza katika uzalishaji wa Gold. Lakini haijawai zalisha gold yenye value inayofikia $4billion kwa mwaka. Kwa maana hiyo, kwa data wanazotumia TRA, Tanzania inabidi ndyo iwe nchi inayoongoza uzalishaji wa gold na ipewe Guiness Award kwa kuvunja record ya kuzalisha Gold nyingi kiasi kuwa hata dunia nzima haikuwai zalisha.

Mimi elimu yangu ni kadegree kamoja tu. Ila naimani kule TRA kuna mpaka maprofessors. Inamaana hata simple analysis kama hiyo hawawezi fanya?

GOD BRING MY TANZANIA BACK.

Inabidi ifikie atua watu wazima waache kufanya maigizo ya kitoto aseeee. Watanzania sio wajinga to that extent. Huwezi badili million kuwa billion kirahisi hivyo.
Siku chache zijazo tutaanza kuchekwa na kukejeliwa na mataifa mengine kwa upuuzi kma huu unaofanywa na watu wachache na wanaojiita wasomi.


Siku acacia wakilipa hata 10% ya ilo deni, mimi nitatembea uchi toka kibiti hadi kariakoo. I swear.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lllllllllllal0
duh!.very saad
 
TRA wametumia reference za Hotuba na Report za Ile Mi Prof ya Kijamaa kina Prof Mruma kupeleka Tax assessment kwa Acacia!

Kama Acacia tuliambiwa haijasajiliwa inakuaje tunapeleka kadirio kwa Kampuni inayofanya kazi kwa Njia haramu?
TRA wamepeleka hayo Makadirio kujikosha mbele ya Rais wasitumbuliwe lakin hata wao ndani ya nafasi zao au wakiwa kwny Mazungumzo wao kwa wao staff wanajua kabisa hiyo Kodi ni ya kufikirika na Acacia hawana uwezo wa kuilipa hata 25% ya Hilo kadirio!

TRA wajiandae kwenda kwny Tribunal kutetea Mzaha huo wa kikodi
That's true..
 
Jamani kwa hiki kiasi cha hela wanachodaiwa TRA mnatudhalilisha .Inabidi Tanzania.iwekwe kwa kitabu cha kuvunja record duniani.kwa uzalishaji wa madini amabacho hakijawahi kutokea kuanzia dunia.kuumbwa.Sipendi.wazungu.wanavyotunyonya ila hii kali?Wekeni report zotewazi.tusome na tujue maabara mliotumia vinginevyo hii.ni siasa tu
 
Walifata nini ikulu na kutoa ahadi ya kulipa kama tuhuma hizo ni kweli? Anyway wamepewa assessment notice ambayo ni sawa na mashtaka kikodi ....waende kupangua hoja ....sheria za kodi si ziko wazi? Tatizo ACACIA wanapiga siasa na kuwachota watu kama nyie. Wale wamekamatwa pabaya ....na hii ikikubalika ni kweli itakuwa mtikisiko dunia nzima na mfumo wa biashara ya madini ....hushangai kwanini wanashindwa kuchukua hatua haraka na kuona kila wito wa serikali ni mtego kwao? Hawachomoki labda JPM awe compromised kitu ambacho si rahisi kihivyo ....

Mkuu wangu mimi nakujua ni mtu muungwana, mstaarabu na mwelewa sana.

Basi ndugu yangu, samahani ikiwa nitakukera ila ni kwamba hakuna hesabu inayoweza kukubali katika uchimbaji wa dhahabu. Kwa kifupi ile kodi ya dola bilioni 40 inamanisha uwe umechimba ounce za dhahabu kama milioni 200 (200,000,000 gold ounces)

Sasa mkuu nakuomba sana kwa kuongeza tu maarifa yako uende pale wizara ya madini uombe rekodi za kiasi cha dhahabu kilichopo katika ardhi ya Tanzania kutokana na tafit i zilizofanyika tangu na baada ya uhuru.

Jitahidi ufanye hivyo mkuu, wewe ni mtu makini mno!!!
 
Waje waje tukae walipe wanachoona wao basi maana tumejionyesha ujinga wetu mchana kweupeeee!!!! Waje waseme wao wana ngapi!!!! Yaishe maana ujinga ni wetuu
 
2 Timotheo, Sura ya 3, Mstari wa 1 - 6:
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi; wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli. ................. ........... 9. Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri. "MAMBO YOTE YATAPITA LAKINI NENO LITASIMAMA".
 
If you have ever invested on anything, you know that now is the time to buy Acacia shares when share prices are declining and because Acacia is likely to successfully show that most of the government accusations are false.

Acacia lost another 6.6% (about 30 m GBP) share value today.

You don't seem to understand attitude, mentality and psychology of investors. Investors normally don't like uncertainty. If they are not sure they sell their stocks they don't buy share in any company which is in limbo.

Therefore Acacia share will continue to slide until

1.) They reach agreement with Tanzania government. It means negotiate with Tanzania Government to be allowed to keep their Tanzanian assets and pay some fine much lower than 190bn usd. They can only afford to pay around 1bn usd. Even that they will need to find a loan from parent company, issue new shares or taken over by another bigger company.

2.) Write off their Tanzania assets which are most profitable to them and comprises about 50% of their assets. This will automatically devalue their share price.

3.) Take Tanzania government to court, Now incourt they might win or lose. Even if they win Tanzania government might appeal or to higher court. The whole process will takes years, by time the case finish the company will be out of stock markets.

4.) Tanzania government and Acacia might try to find a neutral investigator to investigate the 277 containers in now in Dar Harbour to find out who is telling the truth. If they find out Tanzania government is right, that Acacia were under declaring the amount of gold and other precious metals they ship to Europe, they will have to pay fine and compensation which will cripple the company. If they find they Acacia were right then they will receive their 277 containers and compensation which will boost price of their shares.

Personally i doubt very much if they search those 277 containers they will found Acacia were right. I accept that Tanzania government have over exaggerate the amount. But may be they want to send a signal to all companies which operate in Tanzania. That you have to do things rights way and stop messing about.

By the way i don't support any party. This is just neutral observation.
 
Jamani kwa hiki kiasi cha hela wanachodaiwa TRA mnatudhalilisha .Inabidi Tanzania.iwekwe kwa kitabu cha kuvunja record duniani.kwa uzalishaji wa madini amabacho hakijawahi kutokea kuanzia dunia.kuumbwa.Sipendi.wazungu.wanavyotunyonya ila hii kali?Wekeni report zotewazi.tusome na tujue maabara mliotumia vinginevyo hii.ni siasa tu

Kabisa, wote inabidi watuonyeshe vipi walifika kwenye hayo makadirio yao, Pia Acacia waonyeshe all documents watu waliosaini hayo mambo kuanzia mwaka 2000. Pia watu wa Serikali waonyeshe documents zote. Kama Serikali ilikubali kusaini ujinga inabidi waitwe wajieleze au wapelekwe mahakamani.

Pia wanaweza kupima live hayo makontena yote bandarini. Wenyewe wanasema 0.3% ni gold serikali inasema ni mara kumi. Kwa nini sasa wasikubariane na kupima mbele ya watu wa serikali, TV cameras, waandishi habari na watu wa Acacia na Watanzania wote waone live.

Hiyo ndiyo inaweza kumaliza hili tatizo na kujua ukweli.
 
Back
Top Bottom