TRA yafanikiwa kukusanya Tsh. Trilioni 5.151 ktk robo ya kwanza ya mwaka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeripoti kufanikiwa 94.3% katika malengo ya kukusanya Tsh. Trilioni 5.462 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2021/22

Taarifa imesema hiyo ni sawa na ukuaji wa 17.4% ambao umechangiwa na ukuaji wa ulipaji kodi kwa hiari hasa kwa wachimba madini na mawasiliano na uchukuzi

Pia kuimarika kwa biashara ya kimataifa baada ya kuchukua hatua ya kudhibiti janga la #COVID19
1633248604100.png
 
KWA MAKUSANYO HAYA MAANA YAKE WAKATI TUNAFUNGA ROBO YA MWISHO WA MWAKA HATUTAHITAJI TENA PESA ZA WAHISANI KWA AJILI YA BAJETI YA MWAKA UJAO

NI MAKUBWA SANA KAMA SIO TAKWIMU ZA KUPIKWA
 
Hongera sana. Ina maana zitapatikana kama tr 22 kwa mwaka! Bado sana kufikia bajeti yetu.
 
MAFAO ya wastaafu hawalipi. Wanatudanganya wanakopa mikopo IMF midogo inafanana na kukaribia makusanyo wanayotudanganya kwa mwezi.
 
Duuuh! Miradi inasimama, pesa zilizotoza na kusambazwa hazionekani zikifanya kazi, ukusanywaji wa kodi kuongezeka, kuna vyanzo vipya au ndo mnahesabu na tozo mlizoweka kwenye mitandao na mafuta?

Hakuna kutoa wala kudai risiti tena, ulafi umeanza kuanzia level ya chini kabisa, rushwa kama tai, serikali imeamua kukaba wa chini ili kunufaisha wajuu, sasa ukisema wakubwa wanalipa kodi kwa hiari, nitashindwa kuzikubali hizo data.

Kimsingi tumerudi kwenye matamko na mipango isiyotekelezeka.
 
Back
Top Bottom