ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Ndugu wana JF, kwa muda mrefu Kumekuwa na utaratibu wa idara forodha -customs dept. kuongeza thamani ya bidhaa bila vigezo vyovyote(arbitrary uplifting of value of goods). Hata kama mwenye bidhaa akiwapa ankara(invoice) halisi hawaiamini. Utaratibu huu husababisha bei ya juu kwa mlaji wa mwisho bila sababu. Kwa nini tra wasiwe na idara ya research itakayo kuwa na database ya bei za viwandani za bidhaa zote zinazoingizwa nchini ili kuwa na uhalali wa kufanya uplifting? Hao wasomi waliojaa huko kwa nini wasitumie utaalamu wao kikamilifu. ANGALIZO: Nyaraka nyingi zinazokuja na bidhaa zimeghushiwa kwa hiyo data Base za bei halisi za viwandani ndiyo suluhisho la kero hii.