TRA: Watumiaji kilevi kutambua kama kinywaji anachokunywa kimelipiwa kodi kwa kutumia simu ya mkononi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,479
141,189
Kamishna mkuu wa TRA ndugu Kicheere amesema mamlaka yake iko mbioni kuanzisha mfumo ambao wanywaji watatambua kama pombe wanayokunywa imelipiwa kodi.

Mlevi atapaswa kutumia simu ya mkononi kuhakiki kinywaji chake kama ni halali na kimelipiwa kodi.

Kicheere amesema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza mjini Babati.

Mlale unono
Maendeleo hayana vyama!
 
Huyo kamishna hana adabu kabisa, walevi ndio kina nani? msomi mzima ameshindwa kuwasilisha vizuri agizo lake? siamini kabisa
 
Basi hakiki kinywaji chako kabla hujalewa!
Yaani badala ya kuwabana barrick watoe hela , wanabanwa walevi walipe kodi.
Khaaa.
Huyu mtu miaka 5 yake ikiisha aondolewe ameshindwa kazi,
Hili libarrick lililoletwa na majizi ya ccm, majizi ya sisim bado hawaliwezi.
 
Walevi ndio wanaendesha uchumi wa Nchi yenye watu wasio na akili za kubuni vyanzo vya mapato, wameshikilia tu kubandisha kodi za sigara, bia na mishahara ya wafanyakazi
 
Kamishna mkuu wa TRA ndugu Kicheere amesema mamlaka yake iko mbioni kuanzisha mfumo ambao wanywaji watatambua kama pombe wanayokunywa imelipiwa kodi.

Mlevi atapaswa kutumia simu ya mkononi kuhakiki kinywaji chake kama ni halali na kimelipiwa kodi.

Kicheere amesema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza mjini Babati.

Mlale unono
Maendeleo hayana vyama!
This time tutaona mengi. Mimi mnywaji co kazi yangu kuangalia kinywaji imelipiwa kodi inamaana kila nikienda kunywa niwe na cmu nakuanza kuangalia au kuscan bia. Kama wameshindwa kz wajiuzulu kuliko propaganda ambao hazina mbele wala nyuma
 
Back
Top Bottom