TRA watendee haki wafanyabiashara wa Kariakoo makadilio yenu

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,764
895
Wana JF.

Serikali kupitia TRA pitieni upya makadilio yenu mliyopanga kariakoo ya milioni tatu (3) kwa mwaka haya ndiyo makadilio ya chini kwa wafanyabiashara.

Serikali hizo pesa ni mzigo mkubwa kwa wafanyabiasha bado hawajalipa kodi ya maduka, bado hawajalipa leseni, bado hawajalipa ushuru wa takataka, bado hawajalipa fire, bado hawajalipa ulinzi wa maduka.

Serikali hawa Watanzania wanaofanyabiasha zao Kariakoo mnadhani wanapata faida kiasi gani mpaka mnawakamua kiasi hicho hizo kodi wanazolipa kuingiza mizigo yao zinawasaidia nini.

Makadilio ya chini kutoka laki nane mpaka milioni tatu hii ni hatari.
 
Tra wanategeneza mgogoro mkubwa na wafanyabiashara kwani hakuna atayeweza kulipa hyo kodi..
 
Wana JF.

Serikali kupitia TRA pitieni upya makadilio yenu mliyopanga kariakoo ya milioni tatu (3) kwa mwaka haya ndiyo makadilio ya chini kwa wafanyabiashara.

Serikali hizo pesa ni mzigo mkubwa kwa wafanyabiasha bado hawajalipa kodi ya maduka, bado hawajalipa leseni, bado hawajalipa ushuru wa takataka, bado hawajalipa fire, bado hawajalipa ulinzi wa maduka.

Serikali hawa Watanzania wanaofanyabiasha zao Kariakoo mnadhani wanapata faida kiasi gani mpaka mnawakamua kiasi hicho hizo kodi wanazolipa kuingiza mizigo yao zinawasaidia nini.

Makadilio ya chini kutoka laki nane mpaka milioni tatu hii ni hatari.
Ni kweli mdau lakini hapa shida ni pale tunapoingiza siasa kwenye mambo ya msingi niliwahi kuleta uzi hapa wao wanataka wadouble makusanyo ya kodi kwa kuongeza kodi na sio kuongeza vyanzo vya mapato .....ni wavivu wa kufikiri kama wafanyabiashara mngeweza kujustify kua wapo wrong huenda wangewasikiliza !! Lakini sasa kinachotokea ni kutafuta mianya ya kuiba na kukwepa kodi zaidi wakisaidiana na hao hao watumishi wa TRA kwa sababu baba zao ndugu zao mama zao wajomba zao ndio hao wafanyabiashara wa kariakoo
 
Wafanyabiashara waliitwa ngo'mbe wa maziwa .lakini kwa sasa wako katika stagevya kutoavdamu badala ya maziwa .natabiri anguko kubwa la wafanyabiashara wa kati na wadogo muda si mrefu

Wanalipishwa kodi utadhani walipwa kodi waliwekeza kwenye mitaji yao

Tatizo kubwa katika nchi yetu linaanzia wakati wa kampeni .wagombea wetu wanakuwa na uwoga wa kukosa kura .kwa hiyo wanatoa ahadi nyingi nzito kwa lengo la kupata kura

Lakini kimbilio lao ni kwa wafanya biashara bila kujali wafanyabiashara wako kwenye hali gani?

Nadhani huko mbele mamlaka za kikatiba ziweke kiwango maalumu cha ahadi za wagombea vyenginevo wafanya biashara wataendelea kuwa ndio wabebaji wa ahadi za wanasiasa
 
Asilimia 90% ya uchumi wa Tanzania wanamiki wagen hawa ni pamoja na hao wanaomiliki maduka uko kariakoo serikali ya awam ya 5 imewweka mikakat yakuhakikisha watanzania tunamilik uchum wet wenyew .miongon mwa njia za kutimiza azma hiyo ya serikal ni kuhakikisha kila mmoja analipa kod ya serikal hususan wafanyabiashara wakubwa.
 
Kama ni kariakoo wageni itakuwa ni wachina tu hakuna wengine .ambao nao pia ni tatizo kwa upande wa pili .
Maana wanafanya biashara kama wanazofanya wazawa
 
Kwani wamelazimishwa kufanya biashara?ukiona kodi kubwa, badili biashara na fanya shughuli unayodhani utalipa kodi kidogo...tuache kulalamika ovyo..Kodi lazima ikusanywe hamna namna..
 
Yah, lkn kwny kukokotoa bei ya bidhaa uwa wanakadiria kodi ni shs ngapi then wanaongezea kwny cost ndio wajue bei ya kuuzia
ww Mmasai kwanini usifungue na wewe Duka hapo Kariakoo
mtu maisha yako yote na kabila lenu mnalala nje
hujui Kodi ya Chumba cha biashara ni ngapi?
hujui Kodi ya kulala familia ni ngapi?
hujui usafiri wa familia ni ngapi?
hujui ada za watoto wa shule, mavazi yao wala kula yao
UNACHOJUA NI KUKOKOTOA bei km TRA wanavyoelekeza wakati hawajui mali zinapatikanaje?
TRA wanaweka visasi baada ya wafanyabiashara kukataa mashine za FDA
hao TRA wakistaafu wanaona doubeldouble hata umpe nyanya auze hawezi
 
kariakoo tukifunga maduka , hakuna hata panadol itapatikana nchi hii , sisi ndio tunaifanya bandari ifanye kazi , busara kubwa sana inatakiwa kwenye hili .
 
Wana JF.

Serikali kupitia TRA pitieni upya makadilio yenu mliyopanga kariakoo ya milioni tatu (3) kwa mwaka haya ndiyo makadilio ya chini kwa wafanyabiashara.

Serikali hizo pesa ni mzigo mkubwa kwa wafanyabiasha bado hawajalipa kodi ya maduka, bado hawajalipa leseni, bado hawajalipa ushuru wa takataka, bado hawajalipa fire, bado hawajalipa ulinzi wa maduka.

Serikali hawa Watanzania wanaofanyabiasha zao Kariakoo mnadhani wanapata faida kiasi gani mpaka mnawakamua kiasi hicho hizo kodi wanazolipa kuingiza mizigo yao zinawasaidia nini.

Makadilio ya chini kutoka laki nane mpaka milioni tatu hii ni hatari.
Zaidi ya asilimia tisini nyie ni wezi
Unalalimika kadirio la milioni tatu kwa mwaka? Pango ni milioni mbili mpaka nne kwa mwezi mnalipa miezi sita mpaka mwaka hamlalamiki.
Acheni kulia lia lipeni kodi
 
Mkuu hawa TRA hata kuwezesha TIN kupatikana wilayani bado shida,unalazimika kusafiri kwenda hadi mkoani.
 
Hawa wafanyabiashara wamedekezwa sana, mtu analipa pango kwa mwezi zaidi ya 1m halafu analalamikia kodi ya 3m kwa mwaka, mfanyakazi mwenye mshahara zaidi wa kama 2m kwa mwezi anakatwa PAYE zaidi 450k kwa mwezi ambayo ni zaidi ya 5m kwa mwaka, sasa hawa wafanyabiashara inamaanisha wanatengeneza chini ya 1.5m kwa mwezi hadi walielie?
 
KADIRIO LA 3MIL, IS QUET FAIR BINAFSI NAFURAHIA NIPO KARIAKOO NA NINALIPA KWA AWAMU 4.
THANKS.
WE ENJOY.
 
Wangeweka viwango tofauti kariakoo wapo wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili wasikwepe kodi kuliko kutaja kodi ya kuwakomoa wengi watakwepa kodi na wachache watalipa kodi..ndio maana naona watanzania wengi wanafanya biashara nje ya Tanzania wanafanikiwa kwa kuwa huko kodi wanalipa na si za kukomoana..wageni wanafanikiwa kufanya biashara kwa kigezo cha wawekezaji lakini mitaji ndio iyo iyo walionayo Wazawa..
 
Hawa wafanyabiashara wamedekezwa sana, mtu analipa pango kwa mwezi zaidi ya 1m halafu analalamikia kodi ya 3m kwa mwaka, mfanyakazi mwenye mshahara zaidi wa kama 2m kwa mwezi anakatwa PAYE zaidi 450k kwa mwezi ambayo ni zaidi ya 5m kwa mwaka, sasa hawa wafanyabiashara inamaanisha wanatengeneza chini ya 1.5m kwa mwezi hadi walielie?

Well said. Kodi za pango kariakoo ni kubwa sana ila wanalipa six months wengine hadi mwaka. Iweje walalamike 3M? Ina maana hapo 250K kwa mwezi sawa na PAYE ya mfanyakazi wa kawaida kabisa serikalini!
 
Back
Top Bottom