TRA .wanazuia watu wasifanye biashara makisudi.

stemcell

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
677
1,000
Mimi naagiza magari kwa wateja wangu mara kwa mara,ila tumefika sasa hali ni mbaya kifedha na tra wanatukwamisha makusudi,kuna mteja anataka gari thamani hadi da dola 12000 lakini TRA wanasema ni 24000,nikaenda ofisini kwao nikawaambia hii gari mteja wangu anataka lakini thamani yake 12000 website beforward akahakikisha na bado akaniambia nitalipia thamani ya 24000,sasa nauliza kama rais wa jamhuri ya muungano anasema tujifundishe kulipa kodi na huku TRA wanataka kodi isiyo ya halili jee tutafika?sasa mimi ninakosa hela Tra wanakosa hela nchi itafika vipi? Ushahidi huu hapa.
SmartSelectImage_2016-12-18-09-12-50.png
SmartSelectImage_2016-12-18-09-15-01.png
 

Attachments

kasamba12

JF-Expert Member
Aug 18, 2016
341
250
Hiii nchi ngumu sana yaani hawa tra wanafanya isiwe pahali salama kwa kuishi aisee yaan huwa hawaelew kabisa, kingine nahisi hapo kunamtu anataka kitengeneza mazingira ya rushwa
 

Alpha M

Senior Member
Nov 8, 2016
165
250
Pole mkuu kwa upande wangu naamini sera za kuagiza "luxury goods" kutoka nje zinakua na gharama hiyo ili kupunguza uwiano wa biashara (balance of trade- import vs import)

Mathali kwa uzoefu wangu, Benz ukilinganisha name magari mengine ya ujerumani yana gharama kubwa sana ya ushuru. Kalinganishe na BMW au Audi zilizo tengenezwa 2009 kama 5 series au Audi A5 zitakua chini sana.
 

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Unawalaumu TRA bure haya ni maelekezo kutoka juu wafikie lengo kila mwezi kwa namna yeyote ile
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
10,599
2,000
--hopeless / ili mradi kukomoana tu../
GARI SIO ANASA / NI USAFIRI,ILA KWA AFRICA NI ANASA.../
#LINI_TUTASTAARABIKA?
 

Lumwagoz

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
978
1,000
Mimi sijui tra lengo lao nn...kama ni kukusanya tu kodi bila kuja huyo unayemkusanya kodi hali yake vp kibiashara basi ipo siku watakusanya mawe badala ya pesa. nimeamua kufunga maduka yangu mawili nimeamua hela yote kununua ngombe karibia 88 hivi nikatupia shambani lkn yote hiyo nimeamua kufanya sababu ya makodi ya tra. Kulipa kodi ni jambo jema sana lkn wekeni uwiano mzuri kati ya biashara ya na anachostahili kulipa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom