TRA wameniomba rushwa lakini sitoi rushwa kwenye maisha yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA wameniomba rushwa lakini sitoi rushwa kwenye maisha yangu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kamundu, Oct 3, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nimebahatika kufanikiwa kupeleka vitu vya kufungua Hospitali Tanzania ambavyo nimevipata hapa USA kwa miaka miwili na nusu. Vitu vyote ni vya Hospitali na sijachanganya Container langu na kitu chochote ambacho sio cha hospitali. Nina List niliyopewa na barua zakuonyesha kuwa vitu ni vya misaada kwa Hospitali mpya ninayotaka kufungua. Sasa bandarini Tanzania watu wa TRA wanasema eti sio vitu vyote vina msamaha wa kodi na kusema vitu kama vitanda havina msamaha. Vitanda ambavyo ni vichache ninavyo ni vya Hospitali na ni vifaa vya kihospitali sio vitanda vya vyumbani, Dialysis Chair sio kitu cha nyumbani bali ni kiti cha kutumia wakati wa kufanya Dialysis. Sasa sisi tunahangaika huku kujaribu kusaidia kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kufungua Clinics ambazo ukiangalia vizuri hatupati kitu lakini vikwazo visivyo vya msingi vimewekwa na TRA ili kupata sababu ya kuomba rushwa. Sasa huyo jamaa wa TRA anaomba rushwa kama nataka vitu hivyo vitoke vyote na mimi sitatoa rushwa kwa mtu yeyote. Vitu vyangu vikipigwa Mnada mimi na Tanzania basi! nilikuwa nataka kuleta CT Scan ambazo ni hadimu Tanzania lakini nikiendelea kusumbuliwa bila sababu ya msingi sitafanya hivyo tena na watakao umia ni Watanzania masikini. Raisi yuko New York anaomba misaada lakini sisi Watanzania wenzake tunaofanya jitihada za kusadia nchi na uchumi tumekuwa watu wa kunyanyaswa bila sababu za msingi. Kama Watanzania wanaofanya kwenye hizi sehemu hawana uzalendo je mnategemea vipi nchi yetu kuendelea. Je kama Tanzania itatukosa sisi ambao tumetumia pesa zetu, muda wetu kuleta vitu kama vya hospitali na kusumbuliwa je tutategemea wazungu watusaidie mpaka lini badala ya kujisaidia wenyewe. Kama nivyosema siku za nyuma kama hutuwezi kubadilika tusilalamike kwa umasikini.
   
 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Wauzie dili takukuru
   
 3. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kamundu pole sana kwa usumbufu anaokupa huyo jamaa wa TRA. Komaa hivyo hivyo usimpe rushwa, kwani rushwa ni adui wa haki. Hivyo vifaa vikiruhusiwa kutoka pale bandarini na kwenda kufanya kazi iliyokusudiwa,itakuwa ni faraja kwa watanzania wengi wenye kuhitaji huduma bora na wenda itakayokuwa nafuu toka katika Clinic utayoifungua.

  Lakini sijafurahishwa na kukata kwako tamaa ghafla eti kwa sababu ya kuombwa rushwa na kuonyesha ni jinsi gani uzalendo wako kwa nchi yako na watu wake ni mdogo! Kwa nini useme kama havitasamehewa kodi, basi watakaoumia ni wananchi? Kama kweli upo serious na kufungu Clinic ili utoe huduma kwa wananchi, ambayo infact haitakuwa bure kazana kufuatilia hatua zinazofaa.

  Toa taarifa kwa vyombo vinavyohusika kuhusu huyo mtu wa TRA anayetaka rushwa. Nina imani atashughulikiwa mara moja. Nchi hii itajengwa na wenye nchi kama wewe. Keep it up!
   
 4. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Haswaa na ahakikishe umepitia taratibu zote za misamaha ya kodi.

   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa hujui kuwa hii ni Tanzania Revenue Abracadabra? Hawa ni wezi sawa na TAKUKURU yaani Tume ya Kuendeleza na Kupamba Rushwa. Kwa ufupi ni kwamba nchi yetu inatawaliwa kipanya panya ambapo kila mwenye nafasi yake ni toboa toboa anayefikiri kwa tumbo badala ya kichwa. Ni bahati mbaya kuwa ugonjwa huu unaanzia ikulu hadi mtaani kwa mama ntilie.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sijawahi kuona nchi ya kipumbavu kama nchi yetu. Watanzania wanawaogopa wageni kuliko wenyewe nchi. Mzawa utanyanyaswa na kusumbuliwa kupata huduma za jamii au katika wizara lakini wageni hawasumbuliwi. Ni rahisi mgeni kupata ajira kuliko mzawa. Hii ni nchi ya ajabu kuliko nchi zote duniani, inayothamini wageni na kudharau wananchi wake.

  Mkuu wakikusumbua kafungue Hospital Malawi au Rwanda achana na akina Vasco dhaifu
   
 7. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  TRA ni Genge la Majambazi au ni kitengo cha kukwapulia kodi za walalahoi kwa manufaa ya Mafisadi waliopo Magogoni na Dodoma.
   
 8. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Uko mbali lakini last two weeks Naibu waziri wa ardhi akiwa songea kama sikosei aliwaambia maofisa ardhi wasikubali kupokea rushwa, pia akawaambia yeye mwenyewe alikataa RUSHWA YA DOLA LAKI NANE ili atoe favour ya ardhi. Nikajiuliza kweli kiongozi wa serikali anaenda kulalamika kama sio kujitamba kwenye press eti alikataa hongo wakati alitakiwa kuripoti takukuru ili liwe fundisho? Jipime nawewe mkuu, si mda wa kulalamika, just take action,huna sababu hiyo, hapa ungetuletea ripoti tu jinsi ulivyomkomesha huyo jamaa wa tra. CHANGE BEGINS WITH YOU.
   
 9. N

  Nyakwec's Bro JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Pole sana mkuu,nchi yetu inahali mbaya lkn komalia haki yako mwisho wa siku utaipata na kutuhudumia wa tz wenzako ambazo hzo huduma za afya tunasikia tu zipo india hapa bongo ni zakubahatisha km unabahati utapona vinginevyo ni balaa!..
   
 10. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  kumbuka tanzania yenyewe ni majaabu saba ya dunia.
   
 11. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  ukienda tra kukadiwa kodi ya biashara lazma utoa rushwa kwanza ndio ukadirwe sasa hapa kuna nchi
  ushauri wangu nenda kwa kamishina wa kodi ukiwa na docment japo kuna kafoleni kumwona ila namiini ukimwelezea utapata haki yako kaka
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Takukuru yenyewe rushwa tupu
   
 13. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Pole saana ndugu yangu kwa ushauri nenda wizarani ukaonane na katibu mkuu wizara ya fedha anaweza kukuelewa, hawa jamaa wa TRA kazi yao kukwamisha maendeleo ya watu, hasa Watanzania!!!!

   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sasa hili nalo tutamlaumu Mr Prezident?

  Huyo mdai rushwa unakuta nae ndio wa kwanza kulalamika maisha magumu!

  Wasiliana na TAKUKURU bro mkamkamate huyu jamaa ajute kukufahamu.
   
 15. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tutapiga mayowe hadi tuzimie. Tanzania inahitaji kitu kimoja tu cha muhimu nacho ni kubadilisha ufumo wote wa utawala uliooza hadi unanuka kuliko maiti iliyofukuliwa baada ya kuzikwa siku 20. Tuna viongozi ambao aibu zao walishazivua na wanajitembeza dunia nzima wakiwa uchi wa mmnyama ilimradi tu kodi yote imeishia tumboni mwao. Ni mjamzito anafia kwenye daladala haiwahusu. Ni mzee anajikongoja kwa maumivu hawajui. Ni mtoto anapoteza maisha kwa kukosa oxyjen wala hawajali. Ni shule za kata zinazolea wavuta bangi na wazinzi hiyo haiwahusu. Jamani tunaenda wapi na hizi CCM RUSHWA?
  Vilio vya wanyonge vinazidi kuwapumbaza viongozi wa Tanzania. Hawaoni hawasikii wala hawaelewi. Ni wakati umefika tutawatosa baharini tu hakuna njia.
   
 16. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Sasa ndugu zangu hili litanibadilisha mimi kwani ni wakati wa kuwa mbinafsi!! Hivi familia yako na watu waliokusaidia utawaambia nini kama vitu vimekwama bandarini. Na kitu cha kuhuzunisha anayefaidika yote haya siyo Tanzania, Mimi au hata TRA bali ni kampuni ya Meli ya France ambayo vilevile ina Storage pale Dar $50 a day!! wakati sisi Watanzania tunabishana kitu gani cha kodi kitu gani si cha kodi!!. Vilevile ni lazima tuelewe mtu yeyote Tanzania kwasasa ukipata Stroke kubwa una masaa matano tu kufanyiwa operation na kupona sasa hata kama una pesa huwezi kwenda India bali utakufa. Lakini mimi leo nikileta X-Ray, Mzalendo mwingine anaweza kuleta CT, mwingine MRI n.k baada ya muda kutakuwa na hudumu na vifaa vya kotosha Tanzania na si lazima viwe vya Makanisa au Agha Khan pekee!
  Siwafichi kama nikichukuliwa vifaa vyangu nitawatafutia wazazi wangu viza za kudumu ili waweze kuja kufanya check-up USA kila mwaka na mimi nitaendelea na shughuli zangu za binafsi na kuwa mbinafsi kama Watu wengine. Naona upole na upendo kwasasa hautoshi kusaidia Tanzania
   
 17. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  wote tuwe waumini wa kanuni namba 5 ya Tanu"Rushwa ni adui wa haki,sitatoa wala sitapokea rushwa"
   
 18. K

  Kaleja Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba TRA iko pale kukadiria na kukusanya mapato ya serikali kwa mujibu wa sheria na kwa haki bila kumwonea mtu yeyote na pia vitendo vyovyote vya rushwa havikubaliki na hatua kali huchukuliwa kwa mfanyakazi yeyote wa TRA anayebainika kujihusisha na rushwa. Hivyo ndugu mtoa mada toa taarifa kwa namba ifuatayo - Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi simu namba 0784411991 e-mail akiula@tra.go.tz au fika ofisini TRA Makao Makuu onana na Meneja wa kitengo cha Maadili (Internal Affairs Unit). Tuna hakika hatua stahili zitachukuliwa
   
 19. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Katika ufisadi unaofanywa nchini hapa TRA wanaongoza. Hawasemwi kutokana na makusanyo wanayofanya lakini ndani ya TRA kuna ufisadi wa ki-mafia na jamaa ambao wako kwenye mtandao huu ni untoucheable. Wizi wa bandarini wamo, ufisadi katika ucheleweshaji wa mizigo kwa visingizio mbalimbali[ukweli wanataka rushwa] mimi nimesusa kwa hasara yangu kwani nimelipa ushuru wa gari used lakini hadi leo hakieleweki ila bahati niliyonayo garil lenyewe lipo mahala ambapo halinigharimi na lipo salama. Kama kuna chombo kinachostahili kumulikwa na wachunguzi basi TRA ni namba moja.
  Ushauri wangu ni kuwa wakuonyeshe documentary evidence kuhusu hilo dai lao
   
 20. next

  next JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 601
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  na sku iz wanamsemo wao huo "serikali sikivu"
  sikivu my foot.
   
Loading...