TRA wamekuja ofisini kwetu wakitaka kukagua hesabu za 2012 Hadi 2017

Umeandika ukitetemeka?

TRA wana haki ya kukagua na kujiridhisha document muhimu kwa mwaka wowote ingawa muda wa ukaguzi hufanyika walau ndani ya miaka mitano ingawa siyo kigezo cha kuwazuia kukukagua.

Toa document na onyesha ushirikiano
Shida serikali inaendesha mambo kisiasa sana,Mwaka juzi Magufuli alimwagiza waziri wa fedha wakae na TRA kuwasaidia wafanyabiashara kwa kufumbia mahesabu ya nyuma ili ukurasa mpya ufunguliwe na waanze upya-Na magufuli kwenye ile Bussiness Council alisema hana tatizo kabisa,Leo awamu ya sita inawarudisha wafanyabiashara tena kule kule magufuli alipowatoa,very sad
 
Kama mahesabu yako yalikaguliwa na hiyo miaka na ukapata Tax clearance certificate basi waonyeshe lakini kama hukukaguliwa kaka unalo hilo kaa nao mezani huna namna.
kupewa tax clearence sio kigezo cha mwisho ndugu yangu.
 
Umeandika ukitetemeka?

TRA wana haki ya kukagua na kujiridhisha document muhimu kwa mwaka wowote ingawa muda wa ukaguzi hufanyika walau ndani ya miaka mitano ingawa siyo kigezo cha kuwazuia kukukagua.

Toa document na onyesha ushirikiano
May be, ila nadhani motive halisi hapo ni kutaka kupewa rushwa
 
Utakuwa tax evader wa mitandaoni! Natania
Pole mkuu, yaani hii nchi ni ngumu balaah!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
TRA ina aina tatu tofauti za ukaguzi wa kodi.. kuna examination, audit na investigation. mtu unaweza kufanyiwa examination na bado ukafanyiwa tena audit na baadae muda umepita unashangaa unafanyiwa investigation kwa kesi ileile
Ikitokea hivyo kuna tatizo kubwa. Jinai. Audit yenyewe haifanyiki kwa kila mtu....
 
kushindana na TRA si jambo dogo, cha msingi wakae meza moja wayaone mapungufu yatakayojitokeza kwenye hiyo miaka kisha wayamalize yanajadilika hayo. Kwanza wawape info zote wanazohitaji hao mabwana then mapungufu yatakayojitokeza wakae mezani - yanajadilika tu.

Kutunishiana misuli na TRA ni shughuli si ya kitoto.
Si kushindana. Ni kutoa majibu sahihi. Wahasibu wengi ni weupe, badala ya kumtumia wataalam wakati assessment zimetoka ni bora mapema.
 
Watanzania huwa hatupendi kutumia wataalamu. Kuna watu wako tayari kujenga nyumba ya 300mil lakini hawapo tayari kumlipa injinia 5mil ili asimamie kazi yake.

Siku ufa ukitokea ndio anatafuta mtaalamu.
Kabisa, hilo ni tatizo kubwa. Hapo atakaa atakomaa siku assessment imetoka ndo anaanza tafuta mbobezi na mtaaalam.
 
Kampuni nyingi ndogo hazina chochote na zina sales karibia 1b per year

hawana chochote

computer zenyewe zina crash kila siku,excel sheet records kila siku zinaanza upya,etc

records zipo,ila sio straight kiivyo

serikali yenyewe karibu 60% ya records zake za matumizi na manunuzi always go missing..ndio private little companies?

Viofisi vya fremu hizi?Hapana

Na wanaponunua hizo bidhaa awapewi risiti?

Business accounts inatumika vipi

Mambo ni mengi nikisema nioredheshe utaratibu wa huku kijijini kwetu.

Tax ni sheria na kila nchi ina zake naona tume chukua mambo kadhaa ya kidunia Ila ata applications zake kwetu lege lege.

Lakini uhalisia ukisema records keeping ni story ndefu, TRA awajafikia huko.

Niamini watanzania wakiambiwa utaratibu wa record keeping ya nchi za wenzetu kama Magufuli walimuona shetani mama watamuona mchawi.

Basically ukwepi kodi; hizi nchi za wenzetu unaweza punguza profit TAX na ata ukawadai serikali; lakini VAT ni mziki mwingine hiyo hela wanaitaka.

Sasa nikianza kuweka ivyo vielelezo vyao hapa atumalizi leo; ni vingi basically kukwepa VAT tax ni ugomvi mkubwa na hizi serikali za wenzetu.
 
kupewa tax clearence sio kigezo cha mwisho ndugu yangu.
Nini maana ya tax clearence? Ilipaswa ukipewa hiyo unaanzia hapo kwenda mbele unless kuna sababu ya msingi sana. Kuna uzembe sana kwenye taasisi ya kodi. Ndo maana nasema wataalam watumike.
 
Nini maana ya tax clearence? Ilipaswa ukipewa hiyo unaanzia hapo kwenda mbele unless kuna sababu ya msingi sana. Kuna uzembe sana kwenye taasisi ya kodi. Ndo maana nasema wataalam watumike.
Hapo ndio ujue TRA inaendeshwa kimazoea na si kitaalamu au la watumishi wake wengi ni Vilaza.
 
Tax clearance inaonesha umelipa kodi a,b,c haina maana kuwa kodi uliolipa ni kiwango stahidi.
Ndo maana nasema wataalam watumike. Embu chukua tax certificate uisome halafu pitia sheria ya kodi inasemaje kuhusu haki ya kupewa tax clearence certificate. Ile document haitakiwi kutolewa endapo kuna utata wa kodi.
 
Ndo maana nasema wataalam watumike. Embu chukua tax certificate uisome halafu pitia sheria ya kodi inasemaje kuhusu haki ya kupewa tax clearence certificate. Ile document haitakiwi kutolewa endapo kuna utata wa kodi.
Mambo mengine sio utata, ni mahesabu tu yametofautiana. Ukiomba tax clearance unawasilisha tu risiti ulizolipia hata kama hujafanyiwa ukaguzi. Haizuii wao kuja kudai kodi nyingine watakazona wanadai.

Disclaimer: This tax clearance certificate shall not preclude the commissioner general from demanding and recovering taxes established after issuance of this crtificate.
 
Mambo mengine sio utata, ni mahesabu tu yametofautiana. Ukiomba tax clearance unawasilisha tu risiti ulizolipia hata kama hujafanyiwa ukaguzi. Haizuii wao kuja kudai kodi nyingine watakazona wanadai.

Disclaimer: This tax clearance certificate shall not precludethe commissioner general from demand and recovering taxes established after issuance of this crtificate.
Hiyo disclaimer ni Sawa, mfano umekadiriwa kodi milioni, ukalipa laki 5... ukaomba clearence utapewa, hapo haimaanishi kuwa laki tano iliyobaki hutalipa na hutadaiwa.

Ila kama mwakani kama sitalipa hiyo laki tano, nikiomba certificate siruhusiwi kupewa. Sasa unanipa tax clearance ya 2021 wakati 2020 una matatizo na mm ya kodi? Tutumie wataalam tutaumizwa sana na kodi kwa kutokujua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom