TRA waingia mitini kwenye mdahalo wa marekebisho mbalimbali ya kodi

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
276
Jana kwenye kipindi cha KIPIMA JOTO kulikuwa na majadiliano makali kuhusu marekebisho mbalimbali ya kodi na tozo katika bajeti ya 2016l17. Swali kubwa lilikuwa NINI TAFSIRI YAKE KISHERIA?

Katika mada hii wahusika wakuu walitakiwa wawe TRA ili waje wauelezee umma juu ya marekebisho hayo na faida na hasara kwa wananchi. Kinyume chake wakaingia mitini.Kama masuala yote yanatakiwa yafafanuliwe na TRA sisi kama wananchi tuwaelewe vipi?. Je hawajui maana ya marekebisho haya?.

Ninawashukuru sana wale wenzetu walioalikwa kwenye mdahalo ule hasa yule mtalaam wa kodi na Ndugu Ngatunga kwa maelezo yao juu ya mada hiyo ya jana walivyotupa uelewa juu ya marekebisho haya.

Mwisho,ni AIBU KUBWA kwa TRA kuingia mitini.
 
Back
Top Bottom