TRA waangalie pia kanisa Katoliki na mengine ambayo ni tajiri sana baada ya Kakobe

Tukitaka kusimama imara tuachane na masuala ya dini, Kanisa ndilo lenye wapiga kura wengi tuachane nao wakimlilia Mungu kwa mateso yanayosababishwa na wanadamu watokanao na Mungu hatutabaki salama.
Ni wachache wanyajua hayo.
 
Mkuu, simfahamu.
Jaribu kuwatembelea kina Kakobe kesho kisha uje utupashe ya huko kama una nafasi. maana sijui wako sehemu gani. Maana tayari wamempa MIDEA promotion ya bure bila malipo.
Baada ya kuujua ukweli sasa unamkataa!!......ungeendelea kubaki uzidi kunyonyolewa!
 
Mtoa mada naona kama umetoka nje ya mstari kidogo kwa kulilinganisha Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume na Vikundi vya harakati za kidini.
Kanisa Katoliki ni TAASISI yenye nguvu hapa Tanzania na Duniani kote.
Ni taasisi yenye Muunganiko wa kidunia, pia ni taasisi yenye kuendesha mambo yake kwa utaratibu maalumu.
Huwezi kulinganisha na Vikanisa vinavyoanzishwa na mtu mmoja, akijipa uchungaji yeye nwenyewe na hatimaye anajipa Uaskofu yeye nwenyewe.
Mtu huyo anakuwa yeye au mke wake au ndugu yake wa karibu ndiyo anakuwa MHASIBU wa kanisa.
Kwa hiyo usilinganishe Kanisa Katoliki(ROMAN EMPIRE) na Vikanisa vya watu binafsi(SACCOS).
 
Hilo kanisa lake na huyo Kakobe afadhali alilinganishe na saccos ya Chadema!
 
Mtoa mada naona kama umetoka nje ya mstari kidogo kwa kulilinganisha Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume na Vikundi vya harakati za kidini.
Kanisa Katoliki ni TAASISI yenye nguvu hapa Tanzania na Duniani kote.
Ni taasisi yenye Muunganiko wa kidunia, pia ni taasisi yenye kuendesha mambo yake kwa utaratibu maalumu.
Huwezi kulinganisha na Vikanisa vinavyoanzishwa na mtu mmoja, akijipa uchungaji yeye nwenyewe na hatimaye anajipa Uaskofu yeye nwenyewe.
Mtu huyo anakuwa yeye au mke wake au ndugu yake wa karibu ndiyo anakuwa MHASIBU wa kanisa.
Kwa hiyo usilinganishe Kanisa Katoliki(ROMAN EMPIRE) na Vikanisa vya watu binafsi(SACCOS).
Hebu nipe utaratibu kufikia kuwa MTUMISHI wa Mungu.
Je ni Kwenda kusoma Seminary?
Je ni kuwa na PhD in Theology?
Je nikuchaguliwa na watu na kufuata TARATIBU na desturi?
Ama ni WITO ambao Mungu huwaita watumishi?
Kumbuka Yesu Kristu alisema Math 9:37 "MAVUNO ni mengi LAKINI watendakazi HAWAKO.
basi MWOMBENI baba Mungu ili APELEKE WATENDAKAZI shambani mwake". Math
 
Kuna mtu mmoja hapa anauliza utaratibu wa kuwa mtumishi wa Mungu.
Naomba niseme kuwa, mtumishi wa Mungu kwanza anaitwa na Mungu. Kisha anawekwa WAKFU na Mungu kupitia mikono ya watu wengine.
Hata kama wewe ni Daktari bingwa namna gani lakini ukiugua ni lazima akutibu Daktari mwingine. Hivyo utaona kuwa hata Yesu ingawa ni Mungu lakini HAKUJIBATIZA mwenyewe bali alibatizwa na Yohana.
Kwa hiyo kama kweli Kanisa lako ni taasisi huwezi kujipa Uchungaji na Uaskofu wewe mwenyewe.
Kufanya hivyo ni sawa na kujitungia mtihani wewe mwenyewe, kujisajihishia wewe mwenyewe na kujitangazia matokeo ya mtihani huo wewe mwenyewe.
Ndivyo yanavyofanya makanisa ya watu binafsi na ndiyo maana tunayaita SACCOS.
Lakini pia suala la Elimu kwa kiongozi wa Kanisa ni muhimu sana. Katika Dunia ya leo huwezi kuwa kiongozi wa Dini bila kuwa na Elimu angalau kwa kiwango fulani.
Mchungaji kutokuwa na Elimu angalau kwa kiwango fulani hustahili kuitwa MCHUNGAJI bali ni MCHUNGWAJI.
Kwa kawaida huwezi kuchunga kondoo waliokuzidi sana maarifa.
Mchungaji ni lazima awe na maarifa ya kuelimisha watu mambo ya KIROHO na KIMWILI.
Mambo ya KIROHO unaweza kusema umefunuliwa je, mambo ya kuelimisha KIMWILI?
Ili kuwa na Maarifa ya Mambo ya KIMWILI ni lazima uende shule.
Waamini wako wanaweza kuugua kipindupindu kisha wewe mchungaji kwa kukosa maarifa ya KIMWILI ukaanza kuwaaminisha kuwa wana mapepo badala ya kuwapeleka Hospitalini.
Makanisa ya watu wenye akili tangu mwanzo mpaka sasa walikuwa wanajenga KANISA, SHULE na HOSPITAL I.
Wenye akili walijua kuwa hivi vitu vitatu lazima viende sambamba.
 
We are so stupid kiasi kwamba wanaotuongoza ndio maana wanatukandamiza
Mtoa mada ametahadharisha hiyo victimization ma effects zake mtu anakuja ku discuss structure ya katoliki so alivyofanyiwa kakobe ni sawa?kauli yake then linakaguliwa kanisa zima?
 
Wewe umesema YOTE. Mtindo huu ukiachiliwa uendelee basi utafungua Pandora box na itakuwa ni vigumu kuja kulifunga tena.
Nje ya mada! Unapotumia msemo wa "opening of Pandora box" unakuwa uko sahihi lakini unaposema "...itakuwa ni vigumu kuja kulifunga tena" unakuwa unakosea coz hakuna msemo wa closing/sealing of Pandora box! Kwenye lugha the least haina connotation/kirejelewa.
 
Naona tuishie hapo.
Shukrani.
Nashukuru kwa kuwa umeitambua kweli na hiyo kweli itakuweka huru na kundi la wajinga na wapumbavu, maana hata waswahili wana msemo wao " Wajinga ndio waliwao" so usikubali kuwa chakula cha binadamu mwenzio kwa kisingizio/kivuli cha " uaskofu"..........Jumapili njema mkuu!
 
Ha! Ha! Ha! Haaaa!
Daisam umenikumbusha mbali: Mwaka 1999 "Mchungaji" (by then) aliwaaminisha Wafuasi wake kuwa anaponya UKIMWI. Kwa hiyo akawaagiza wote wakapime, wajue status zao halafu awaponye. Walipima kwa wingi kweli! Nikiwa katika taasisi fulani ghafla tukaona influx kubwa ya watu wanahitaji kupima HIV. Tukafulahi tukadhani Kiongozi ameona umuhimu wa kupima afya enzi hizo kulikuwa na stigma sana!
Baadaye after 4 weeks tukaona wale wote waliokuwa wame-test "HIV positive" awali, wamerudi tena kupima. Tukawauliza kama bado hawajayakubali majibu yao?? Wakasema hapana, walikubali isipokuwa "Wamefanyiwa maombezi kwa wiki 3 na wamepona kabisa; na sasa wamefika kuhakiki ili wapeleke taarifa za kupona" Tukaanza kuwaelimisha upya, na kuwapima tena! Majibu yao wote yalibaki kuwa HIV Positive. Wengine wakawa disappointed lakini wengine wakasema wanakwenda kuombewa tena ili wauondoe kanisa UKIMWI miilini mwao.
....................... Ni kweli kabisa Viongozi wa Dini ni vema wakiwa na elimu ya kutosha kwani watawasaidia sana Wafuasi wao!
 
Nashukuru kwa kuwa umeitambua kweli na hiyo kweli itakuweka huru na kundi la wajinga na wapumbavu, maana hata waswahili wana msemo wao " Wajinga ndio waliwao" so usikubali kuwa chakula cha binadamu mwenzio kwa kisingizio/kivuli cha " uaskofu"..........Jumapili njema mkuu!
Yesu kristu ndo KWELI kando yake hamna kweli nyingine.
Sijui unapozungumzia neno "Kweli" una maana ya Yesu ama msemo tu uliozoea?
Maana kama ni Yesu aliniweka HURU siku nilipomwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu.
Kweli yakoni aina gani mkuu?
 
Nje ya mada! Unapotumia msemo wa "opening of Pandora box" unakuwa uko sahihi lakini unaposema "...itakuwa ni vigumu kuja kulifunga tena" unakuwa unakosea coz hakuna msemo wa closing/sealing of Pandora box! Kwenye lugha the least haina connotation/kirejelewa.
Nimekuelewa vizuri sana. Ila ni kuwa hypothetical/ Figuratively ili tu ingie na iingie vichwani mwa wengine!.
Nashukuru.
 
Yesu kristu ndo KWELI kando yake hamna kweli nyingine.
Sijui unapozungumzia neno "Kweli" una maana ya Yesu ama msemo tu uliozoea?
Maana kama ni Yesu aliniweka HURU siku nilipomwamini kama Bwana na mwokozi wa maisha yangu.
Kweli yakoni aina gani mkuu?
Kweli ya kukuweka huru na manabii wa uwongo!
 
Kuna mtu mmoja hapa anauliza utaratibu wa kuwa mtumishi wa Mungu.
Naomba niseme kuwa, mtumishi wa Mungu kwanza anaitwa na Mungu. Kisha anawekwa WAKFU na Mungu kupitia mikono ya watu wengine.
Hata kama wewe ni Daktari bingwa namna gani lakini ukiugua ni lazima akutibu Daktari mwingine. Hivyo utaona kuwa hata Yesu ingawa ni Mungu lakini HAKUJIBATIZA mwenyewe bali alibatizwa na Yohana.
Kwa hiyo kama kweli Kanisa lako ni taasisi huwezi kujipa Uchungaji na Uaskofu wewe mwenyewe.
Kufanya hivyo ni sawa na kujitungia mtihani wewe mwenyewe, kujisajihishia wewe mwenyewe na kujitangazia matokeo ya mtihani huo wewe mwenyewe.
Ndivyo yanavyofanya makanisa ya watu binafsi na ndiyo maana tunayaita SACCOS.
Lakini pia suala la Elimu kwa kiongozi wa Kanisa ni muhimu sana. Katika Dunia ya leo huwezi kuwa kiongozi wa Dini bila kuwa na Elimu angalau kwa kiwango fulani.
Mchungaji kutokuwa na Elimu angalau kwa kiwango fulani hustahili kuitwa MCHUNGAJI bali ni MCHUNGWAJI.
Kwa kawaida huwezi kuchunga kondoo waliokuzidi sana maarifa.
Mchungaji ni lazima awe na maarifa ya kuelimisha watu mambo ya KIROHO na KIMWILI.
Mambo ya KIROHO unaweza kusema umefunuliwa je, mambo ya kuelimisha KIMWILI?
Ili kuwa na Maarifa ya Mambo ya KIMWILI ni lazima uende shule.
Waamini wako wanaweza kuugua kipindupindu kisha wewe mchungaji kwa kukosa maarifa ya KIMWILI ukaanza kuwaaminisha kuwa wana mapepo badala ya kuwapeleka Hospitalini.
Makanisa ya watu wenye akili tangu mwanzo mpaka sasa walikuwa wanajenga KANISA, SHULE na HOSPITAL I.
Wenye akili walijua kuwa hivi vitu vitatu lazima viende sambamba.
Nakubaana nawe. Isipokuwa tusiwahumu.
Sidhani kuwa NI WOTE hujitungia mitihani na kujipa matokeo yao wao wenyewe.
Isipokuwa naamini husimikwa na Maaskofu wenzao..

Nakubaliana nawe kuwa ELIMU ni ya muhimu sana maana bila hiyo kunakuwa na matatizo ya kuzuka Viji SECTS.
Bali si wote walio hivyo.
Mfano wako ni mzuri na unaeleweka.
 
We are so stupid kiasi kwamba wanaotuongoza ndio maana wanatukandamiza
Mtoa mada ametahadharisha hiyo victimization ma effects zake mtu anakuja ku discuss structure ya katoliki so alivyofanyiwa kakobe ni sawa?kauli yake then linakaguliwa kanisa zima?
Ahsante kwa kunielewa. Wengine wana unafiki sana. Ni lazima tusifu mahali panapohitajika . Na Tuukosoe mahali pana makosa.
Haiitaji PhD mtu kunielewa nilikuwa ninasema nini hasa.
Ila watu wengine wanakurupuka na utetezi based on "DINI" Japokuwa hiyo haikuwa Mada yangu.
 
Back
Top Bottom