TRA tuacheni Watanzania tukuze uchumi wa nchi yetu mnatubana sana punguzeni njaa zisizo na tija kwa Taifa

Molleli

Senior Member
Aug 29, 2020
178
160
Sio kwamba msikusanye kodi hapana ila Kuna mambo mengi TRA wanafanya ambayo yamekua ni kero kwa wafanya biashara unakuta mtu katoka na mzigo China Ile kutua tu AirPort anakutana na msururu wa TRA apo na wapo serious vibaya mno wanakagua mzigo mmoja baada ya mwingine.

Unakuta mtu kabeba simu Tatu kwajili ya ndugu zake nyumbani ataambiwa azilipie kulingana na makadilio ya bei ya simu husika na moja kwa moja Lazima rushwa itatolewa pale na pesa zinawekwa mifukoni bado ukifika dukani wanakuja Tena kudai kodi.

Hii sio fair kabisa jamani TRA ni jipu kwetu wafanya biashara hasa tunaojumua mzigo kutoka nje ya nchi punguzeni kutubana kwa vitu vidogo vidogo tupate kuwagana ajira na hapo uchumi wa nchi yetu utakua kwa kasi na vijana tutapiga kazi.

Punguzeni tamaa TRA. ASANTENI.
 
Pole bwana Molleli ........ ila umeandika kama unaongea , af ukatufokea kabisa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hiii inji ni Kodi,Kodi,Kodi
Tena Kodi!

Namaana hiii!
Ukiagiza gari ikifika bandarini unakatwa bonge Kodi,
Unaanza kuisajiri Kodi,
Inaanza kutembelea Kodi,
Mafuta unayoyajaza Kodi,
Ikibeba mzigo au abiria Kodi,
Walioipanda wanalipishwa Kodi,
Bima ya gari kodiii
Plate number kodii

Hapo hujakutana na tarafiki kodiiiiiii!
Yaani kitu kimoja kinalipia Kodi 50

Shame!
 
Misaada na Kodi hizo tunazopewa wajukuu wa wajukuu zetu watakuja kuzilipa na muda huo Hawa jamaa wangece Sana vizazi vyao vitakuwa vinaishi huko kwa towers za New York wakijadai kuwa their forefathers waliopigana Sana walisoma Sana na huku waliaminiwa na umma wakapewa nchi wakaiba na kujimbilikizia Mali..
 
Sio kwamba msikusanye kodi hapana ila Kuna mambo mengi TRA wanafanya ambayo yamekua ni kero kwa wafanya biashara unakuta mtu katoka na mzigo China Ile kutua tu AirPort anakutana na msururu wa TRA apo na wapo serious vibaya mno wanakagua mzigo mmoja baada ya mwingine.

Unakuta mtu kabeba simu Tatu kwajili ya ndugu zake nyumbani ataambiwa azilipie kulingana na makadilio ya bei ya simu husika na moja kwa moja Lazima rushwa itatolewa pale na pesa zinawekwa mifukoni bado ukifika dukani wanakuja Tena kudai kodi.

Hii sio fair kabisa jamani TRA ni jipu kwetu wafanya biashara hasa tunaojumua mzigo kutoka nje ya nchi punguzeni kutubana kwa vitu vidogo vidogo tupate kuwagana ajira na hapo uchumi wa nchi yetu utakua kwa kasi na vijana tutapiga kazi.

Punguzeni tamaa TRA. ASANTENI.
sasa wewe unakuja na simu kama iphone13pro max 3 ambayo thamani yake kama milinioni za kibongo 4 kwa moja mwenzio anagari vits moja thamani milioni 6 za kibongo analipa kodi unaona kulipa kodi unaonewa je mwenye vits naye asemaje? Nachojua kuna thamani ya bidhaa ukipita hulipi kodi ila ikizidi hata kama ni bidhaa ndogo utalipa tu na hata kama ikiwa ndogo kiasi gani.Kinachoangaliwa ni thamani siyo bidhaa au idadi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom