TRA sasa yapewa kazi ya kupiga hodi kila nyumba kusaka kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA sasa yapewa kazi ya kupiga hodi kila nyumba kusaka kodi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Jul 1, 2008.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Baadhi wa wakazi wa Dar es Salaam wakiwa na bidhaa walizonunua katika maonyesho ya kimataifa ya biashara yaliyoanza Jumanne Jijini.
  • Utekelezaji umeanza rasmi jana
  • Majengo yote kuthaminiwa upya
  • Mkoa wa Dar kufungua mlango
  Hussein Issa na Saa Mohamed

  SERIKALI imekabidhi rasmi jukumu la kukusanya kodi ya majengo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kamishna wa Kodi za ndani, Joannes Mallya tafanya kazi hiyo kwa niaba ya Serikali za Mitaa na kwamba inaanza kutekelezwa mwezi huu.

  Habari kamili bofya hapa
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sheria ilishipitishwa na bunge kitambo
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu nafikiri ulitaka kuandika heading "TRA sasa yapewa..."

  Bado kidogo nifikiri "RA apewa...." nikasema sasa huyu ananyang'anywa Dowans anapewa ulaji zaidi...

  Luckily it was just a bad nightmare, caused by a typo. I am awake. Thanks to the singularity.
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Shukrani,

  Kwa hakika serikali imepoteza mapato mengi hapa!!! sasa subiria what will happen...

  Wenye nyumba watakuwa registered watakuwa na TIN, hakuna kukwepa kodi...
   
 5. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kasheshe, tatizo sio tu kwenye kukusanya pesa, tatizo ni kuwa hata zinazokusanywa zinachukuliwa na kufanyia kampeni ya uraisi ili kushinda kwa kishindo. Zinazobakia wanapewa manji, rostam, na wazee wa vijisenti.

  Kukusanya mapato bila kutunza au kutumia vizuri kilichokusanywa si suluhisho pekee la matatizo.
   
 6. M

  Mnyoofu Senior Member

  #6
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Sina ugomvi na jinsi wanavyopenda kukusanya kodi in a more efficient and equitable way, my concerns ni jinsi wanavyotumia kodi zetu vibaya! Im seriously disapointed!

  Pia TRA waache kuwa wazembe wakufikiri, kila siku tunawapigia kelele they r too lazy in thinking and exploring more avenues in broadening the tax base, they are just milking a very small group of taxpayers, yote hii ni uvivu wa kufikiri pia ubinafsi, coz wao wanapata mishahara na kujineemesha kwa rushwa iliyokithiri wakati wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Sasa na hao 'wachukuaji' wa rasilimali zetu ambao hawalipi kodi ni lini na wao wataanza kulipa kodo kutokana na faida kubwa wanayoipata? Watanzania tu ndiyo wanaokamuliwa kulipa kodi kupita kiasi na kodi hiyo hawaoni manufaa yake maana huishia mifukoni mwa mafisadi.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na katika hili ifahamike kuwa TRA wamepewa kama mkataba wa muda fulani lengo likiwa ni kuzisaidia local govt kujenga uwezo wa kukusanya kodi hii kwa ufanisi. Baada ya muda jukumu litarudishwa hukohuko serikali za mitaa, ambako kwanza walishindwa kukusanya na kuna ulaji mwingi (anyway, hata serikali kuu nako kuna ulaji kama ilivyosemwa hapo juu)
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  Jul 1, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,424
  Trophy Points: 280
  nasikia .....walevi Na Wavuta Sigara ....ndio Kikomo Cha Kufikiri Tra Wakati Wanapendekeza Vyanzo Vipya Wakati Wa Bjeti....

  Kimsingi Walevi Wanachangia Kiasi Kikubwa Mapato Ya Chi Hii...itafikia Siku Itabidi Walokole Wazuiwe Kuhubiri Kwa Kuwa Kwa Kila Mlevi Mmoja Wanayemvua Na Kumfanya Aache Pombe....wanakuwa Wameinyima Serikali Mapato Makubwa......

  Mfano Kama Kila Siku Unakunywa Bia 5 Tu.....unachangia Tsh 500 Kwa Kila Bia Au Tsh 2,500 Kwa Siku ....kwa Mwezi Tsh 75,000....kwa Mwaka Tsh 900,000/=.....

  Jamani Kwa Nini Muendelee Kuwadharau Walevi???....walevi Wanawaweka Mjini...
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Vyanzo vya mapato ni vingi sana............however, ukusanyaji wake ni wa upendeleo(biased) mkubwa........na kinachotkea ni kuwa anayeumia ni mnyoge.........kwani mnyonge ndio hufidia gap la wanaokula "tax holidays" na wazee wa "vijisenti"........na wanyonge hao hao ndio hufa mahospitalini kwa kukosa matibabu/kinga thabiti..............
   
 11. K

  Koba JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Yaani kwa dunia ya leo na high tech ilivyo advance katika kila area ya maisha yetu ya kila siku,lakini hawa TRA bado wanazungumzia kugonga milango ya watu kukusanya kodi? jamani hii ni aibu na uzembe wa hali ya juu na hakuna excuse yeyote ya kufanya kazi kwa style hii...hii ni aibu kubwa sana kwa viongozi wa TRA na inaonekana hawajui chochote,dawa yao kuwaondoa tuu na kuweka watu wanaoweza kufanya kazi,pesa nyingi sana zinapotea kwa incompetency za hawa watu.
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Sina hakika kama ni vizuri. Tunaweza kushangaa tunarudi kulekule kwenye kodi kama za mkoloni, breast tax, head tax na kodi nyingine za ajabu ajabu. Bado kuna maeneo mengi sana ya kukusanya kodi yanaachwa. na matokeo yake wanaotozwa kodi ni wanyonge wenye moyo wa kulipa kodi na wanasamehewa ni wale wenye uwezo wa kulipa na kukwepa kodi.
   
 13. M

  Major JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  ni bora kodi alizokuwa anakusanya mkoloni maana angalau barabara za mitaani ziliwekwa lami na usafi ulikuwa kwa sana tofauti na sasa barabara za katikati ya mji ni vumbi tupu ma miji ni michafu kupindukia utafikiri ni miji ya nguruwe na siyo ya binadamu
   
 14. m

  mkwegi Member

  #14
  Jul 4, 2008
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Wala tusilisifie hilo la nyumba-kwa- nyumba jamani maana litaongeza kero tu kwetu wenyewe. ni walewale walipaji wa kila siku ndo wataendelea kulipa tu!
  Hiyo ni pesa kidogo sana itakayokuwa recovered mainly toka kwa walala hoi na watu wa kipato cha chini/wastani!
  kimsingi makusanyo hayo yote kwa mwaka hayatafikia kodi inayokwepwa na wawekezaji wa madini ikiwemo Barrick kwa mwaka mmoja tu(achilia mbali miaka yao 11 ya msamaha iliyobaki hadi 2019); pia haitafikia 3/4 ya kodi inayokwepwa ktk mipaka yetu wakati wa import and export.
  Haitakuwa rahisi Tanzania kuwa na mstakabali ulio nyooka,elekezi na unaotekelezeka kwa kutumia rasilimali watu(manpower) wazalendo hadi pale wanasiasa watakapoacha kutoa maamuzi juu ya masuala yanayohusu taaluma ya kisayansi. BILA HIVYO, Watanzania tutaendelea kuonekana wapumbavu tu na wepesi wa kudanganywa na kuridhika na ahadi zisizotekelezwa! TUAMKE, TUWE AGGRESSIVE NA MALI ZETU na TUWE TAYARI KWA LOLOTE. Hapo hata wawekezaji wanaomiminika kama kumbikumbi wa msimu watapunguza kasi maana watajua ni lazima kodi walipe!!
   
 15. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sio wawaonee wananchi wa hali ya chini tuu kama ilivyojadi yao TRA, waendee na kwakina Manji na Bakhresa wakachukue Kodi na hasahasa kwa BAKHRESA. Maana huu ndio mwanzo wa kuanza kunyanyaswa kwa wananchi waliojichokea. Halafu hii nchi inashangaza sana ninauhakika waliopendekeza hii ni mafisadi na nafikiri kwa lengo la kutukomoa au kuendelea kuchota serikalini.
   
Loading...