Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,695
- 2,553
Watanzania mliokuwa katika wilaya zingine Tanzania tupeana taarifa kuhusiana na zoezi wanalofanya hawa jamaa wa TRA wilayani Ruangwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kunyanyasa wafanyabiashara na wamiliki wa magari.
Leo jamaa wameanzisha kamata kamata ya magari na kulazimisha wamiliki kulipia road license ya magari yaliyoandikishwa kwa jina lako hata kama ni chakavu na hayako barabarani.
Wanaendesha zoezi kwa kiburi kikubwa tena wakijinadi wametumwa na wakubwa, haina maana watu hawataki kulipa kodi bali value for money muhimu sana na system inabambikia watu madeni hata kwa gari zilizotoka barabarani miaka 10 iliyopita na wanaachilia kwa upendeleo mkubwa sana.
Rai yangu kwa JPM watumishi inawezekana hawajaelewa maagizo yako na woga wao kwako unakuwa kero kwa wananchi na wapiga kura. Kama akina Bakhresa mnakaa nao na kuzungumza nao namna bora ya kulipa madeni yao basi muulika na hawa watu wenu wa ngazi ya wilaya. Inaonekana kila mtu anataka aonekane anafanya kazi kuridhisha wakubwa kumbe wanawaharibia na chukueni hatua sasa.
Wadau tupeane taarifa zoezi la namna hii linafanyika na wapi katika nchi hii na kwa nini ni Ruangwa?