TRA: Nyumba za Lugumi hazitoshi kulipa deni, hivyo tutashikilia mali nyingine za mfanyabiasha huyo

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
TRA kupitia kwa kamshna wake mkuu Charles Kichere imesema nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi zinazopigwa mnada, hazitoshelezi kulipa deni analodaiwa na mamlaka hiyo.

Ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Kagera na kubainisha kuwa TRA itashikilia mali nyingine za mfanyabishara huyo.

Chanzo: Azam TV
 
kwani na yeye lugumi si anaidai serikali au nilisikia vibaya
utaratibu wa kifedha hakuna kitu kukatana juu kwa juu, inaangaliwa kimkataba nani anatakiwa kumplipa mwenzake kwanza. kama nakudai miatano na wewe unanidai 700,ila deni langu lipo due lazima uninipe kama lilivyo hakuna ile kata hela yako kisha nilipe inayobaki.
 
ok
 
Kwani Lugumi anafanya biashara gani mpaka adaiwe kodi kubwa kiasi hicho, na TRA walikuwa wapi muda wote kudai kodi mpaka iwe kubwa kiasi hicho.
Isije kuwa ni mbinu ya kumshughulikia kutokana na zile tuhuma zake, makadirio yakafanywa kama yale ya Acacia.
 
Ha ha ha ha ha mie nlizan mnapeana chenji tu
 
Kwani Lugumi anafanya biashara gani mpaka adaiwe kodi kubwa kiasi hicho, na TRA walikuwa wapi muda wote kudai kodi mpaka iwe kubwa kiasi hicho.
Isije kuwa ni mbinu ya kumshughulikia kutokana na zile tuhuma zake, makadirio yakafanywa kama yale ya Acacia.
Naona watu wanashughulikiwa kwa mbinu ya kodi.
Hata rugemarila akiachiwa atashughulikiwa kwa style hiyo kufidia ule mgao aliochukua
 
Halafu viongozi waliotufikisha hapa, akiwemo Magufuli, wanaachwa wakitamba mtaani! Huku tukiendelea kuwalipa na kuwatunza wao na familia zao.
 
Back
Top Bottom