Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,271
- 2,401
Nimekuwa nafuatilia masuala yangu TRA (sisemi ni wapi) hapa Dar. Wakati wahudumu wakiendelea na huduma unasikia wanasema subiri network irudi. Hapo majukumu inabidi yasimame hadi network ikae tena sawa. Ikifika hapo baadhi ya wateja huamua muahirisha kilichowapeleka pale.
Hili nimekumbana nalo siku mbili mfululizo. Ina maana ndio kawaida kwa mtandao kusumbua TRA.
Katika ulimwengu huu wa leo kweli taasisi kama TRA wanasumbuliwa na network? Wanakwamisha huduma kisa mtandao uko chini au umekata? Kweli? Na hela zote mnazokusanya hata kama zinaenda serikali kuu, hamna fungu la kutatua hiyo kero? Mnatia aibu kwa kweli.
Mtu anafika TRA kwa hofu kama anaingia kituo cha polisi. Basi mfanyieni huduma yake kwa ufanisi mkizingatia muda. Hakuna anayetaka kushinda humo ndani maana si sehemu rafiki sana.
Ukiwatazama hata wakadiriaji wenyewe wamekaa kivitisho vitisho tu. Hadi uongee na ndio ujue ni rafiki au la, ila wengi wanaogofya. Mamlaka husika fanyieni kazi hilo suala la mtandao ASAP!