TRA ni SHIDA: Wavamia Ofisi hapa Viwandani

Wafanyabiashara Tanzania hawataki kulipa kodi halali, na matamshi yakukurupuka ya SSH yamewapa kibri cha kukataa kulipa kodi halali kwa uwazi kabisa, TRA wafanye nini kwa mtu anayekataa kulipa kodi kwa uwazi kabisa? SSH is naive na anaenda kuleta mgogoro mkubwa wa TRA kwa sababu akili finyu.
Wewe utakua mfanyakazi, hawa watu malengo yao ni rushwa, Hakuna mtu anayekataa kulipa kodi, watu wanataka kulipa kodi ya halali, na kama kipindi hiki cha korona wanafayabiashara Wengi hawezi kulipa kodi kwani biashara zimekwama.
 
Acha upotoshaji. eti matamko yamefanya mfanya biashara asilipe kodi. toka lini?

Kodi iko kisheria sio tamko la rais?

Wala rais hakusema watu wasilipe kodi.
Nchi imejaa Wakurupukaji sana hii, sasa sijui Raisi anahusikaje na kulipa au kutolipa kodi.

Raisi kuhimiza busara itumike inaonekana ni kosa kubwa sana kwa hiyo alipaswa kuwaagiza TRA watumie nguvu na vurugu na kudhulumu.

Hii ndio inadhihirisha tulivyo na Watu wasio na uwezo kiutendaji. , kama Ofisa wa kodi na unalalamika kuwa unashindwa kukusanya kodi si upishe wapewe kazi wenye uwezo huo unang'ang'ania nini?.
 
Wafanyabiashara Tanzania hawataki kulipa kodi halali, na matamshi yakukurupuka ya SSH yamewapa kibri cha kukataa kulipa kodi halali kwa uwazi kabisa, TRA wafanye nini kwa mtu anayekataa kulipa kodi kwa uwazi kabisa? SSH is naive na anaenda kuleta mgogoro mkubwa wa TRA kwa sababu akili finyu.
Mwamba una akili sana. Umewaza Mbali. Nataka niandike Maoni kwa SSH, aongezee mkazo. Asiishie alichosema, aseme pia kuwa walipa kodi wanao wajibu wa kulipa kodi bila shuruti pia. Yeye aliwasema tu TRA. Mheshimiwa Rais pale kidogo aliteleza. Juzi nimemuona RC wa Mwanza bwana Chalamila anasema hotuba ya Rais ingeendelea, maana yake angesema Wafanyabiashara nao walipe kodi bila shuruti, lakini Mheshimiwa Rais hilo hakulisema.

Kingine naona mleta uzi pia hajazingatia mamlaka waliyo nayo TRA, naye kwasababu ya SSH anaona TRA wabaya. Kodi ni Sheria na imeweka hatua zote za kuchukua kama mtu hajalipa kodi halali na pia Sheria hiyo hiyo inampa Mlipa kodi mwaya wa kukata rufaa mpaka kufika mahakamani akionewa.

Jamani Mh. SSH, badilisha kidogo kauli.
 
Wewe acha kutetea ujinga. Kwa hiyo kumharasi mtu ndio njia nzuri ya kudai kodi stahiki?. Kama halipi kodi kuna njia za kutumia kuna mazungumzo,then mahakamani. Sio mtu unamvamia kama jambazi. Wapo waliopoteza maisha kwa mshtuko kwa kuvamiwa namna hiyo. Zipo sheria za kufuatwa mtu kama halipi kodi. Kuna mahakama pia. Sasa kwa nini TRA wajichukulie sheria mkononi,kujifanya wenyewe ndio final kwa matendo yote yahusuyo binadamu hapa Tz?. Imefikia hatua wanaogopwa kama mashetani hivi,wakifika ofisini kwako,kama una roho nyepesi au mtu mzima unaweza kuanguka na kuzimia au kupoteza maisha. Na wao wanaifurahia hiyo hali ya kuogopwa,na wanaendelea na vitisho vyao. Hii hali ipo Tz tu,na mtabaki peke yenu,hakuna mwekezaji atabaki kwa mtindo huu.
 
Ndio unajua leo?
 
Katika hali ya kawaida kodi hukusanywa kupitia "voluntary tax compliance" endapo kutakuwa na njia nzuri ya mahusiano ya kibiashara kati ya mlipa kodi na mamlaka husika za ukusanyaji wa kodi. Ikishindikana ndipo njia za misuli hitumika kupitia "involuntary tax compliance" na jambo hili limeainishwa pia kisheria.

Mtoa mada pengine angeweza kutujuza zaidi ni maafisa wa kitengo kipi kutoka TRA walihusika na zoezi hilo alilolishuhudia. Ni lazima kujiridhisha kabla ya kuwatuhumu, usije ukakuta ni wa kitengo cha "Investigation or Post Clearance" ambapo wamefikia kuchukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa mlipa kodi alijihusisha na "tax evasion" ambapo ni kosa kubwa kisheria.

Naomba tusikimbilie kuwahukumu wakusanya kodi pale wanapotekeleza majukumu yao yaliyoanishwa kisheria. Nao pia ni binadamu pale tunapohisi wakienda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa, basi tujiridhishe kwa kutoa taarifa hizo kwa kitengo cha elimu kwa mlipa kodi. Ambapo namba zake zipo mitandaoni na ni bure kabisa kuzipiga.
Nondo ya maana hii umeitoa. Safi sana. Watu wanadhani sheria ni Voluntary tu.
 
Samahani kwa kukujibu rude

Lakini huko unaposema kodi inaonekana kwenye maisha ya watu wao siyo huku hao TRA wanakuja kama wavamizi bado kodi inachezewa na watu wachache na familia zao

Na wengi wanao sema na kushupaza shingo sijui TRA wapo sahihi ujue hata hana uwekezaji mdogo tu kuanzia hata kibanda cha mini-supermarket ya kimtaa

Tusi copy tu ya ulaya wale wana nidhamu hata kwa matumizi ya kodi inayokusanywa huku wanasiasa /watumishi wa Umma wanachukua kutukoga hizo kodi kwa kugawa ovyo pesa za wananchi na kuwa na vimada kila pembe nk
Mbunyimayi; Mimi ni mtaalamu wa kodi. Kodi hailipwi kwa mtaji, mfano corporate tax inalipwa kwa faida uliyoipata. Full stop. Ukifuata masharti hayo hutaumia. VAT wewe ni mkusanyaji kwa niaba ya TRA na si vingine. Sasa shida ni nini.

Watanzania waelimishwe.
 
Hiyo ni kazi yao na wanaijua vizuri. Msihukumu kwa haraka, mpaka TRA wamechukua hatua hiyo lazima huyu mlipa kodi atakuwa na ujeuri fulani. Nchi hii kuna udanganyifu mkubwa sana wa kodi! na kazi ya TRA ni ngumu sana! Kuna watu hawawezi kabisa ustaarabu, watu wa namna hiyo ndio wale mama alisema ukinizingua tunazinguana!! Sasa ukiandaa mazingira ya kuzinguana, usije hapa na kuanza kulia lia!!
Takwa la kodi lipo kisheria sio la taasisi husika kujiamulia jinsi itakavyo kusanya mapato.

Hata wao wanatafsiri sheria jinsi wanavyotakiwa kukusanya kodi kama mlipa kodi anavyotafsiri sheria hiyo hiyo jinsi anavyotakiwa kulipa; aina maana kila action ya TRA ni legal.

Uwezi kwenda kwenye biashara ya mtu nakuondoka na nyaraka zake kisa unataka kuhakiki kodi, laptop ya biashara ina uhusiano gani na kodi?

TRA wanachotaka ni evidence to verify you tax bill kama wanadhani unawaongopea utapata barua wanataka kukufanyia Tax Inquiry na inabidi utoe ushirikiano.

Tax inquiry inawaruhusu kufanya auditing trail; usipotoa ushirikiano sheria inawaruhusu kukudaria kiasi gani wanadhani unatakiwa ulipe na uwezi kupinga hiyo kodi yao mpaka utoe ushahidi wako unaoonyesha tofauti kwa muda uliowekwa ndio watarekebisha, vinginevyo utalipa makadirio.

Wakiamua usipotoa ushirikiano wanaweza kukufungulia case ya tax evasion too na adhabu yake sio ndogo. Kwa ivyo wana mbinu nyingi za kukulazimisha kutoa ushahidi, kwenda kwenye biashara ya mtu na kuchukua ushahidi kilazima huo ni ujambazi, whose to say uwezi iba siri za biashara kama bei zake na suppliers wake ni cheap kushinda wanazopewa washindani wake na mambo mengine ambayo ni siri zake.

Hakuna nchi duniani wakusanya kodi wanaweza chukua ushahidi kwa lazima kisa madai, that’s a criminal offence.

Sipingi watu kudaiwa kodi kwa nguvu; ila sheria lazima zifuatwe kwenye kufanya ivyo.
 
Hapo kuna "NANGA" amechoresha mchongo kwa TRA
Nadhani tutaongea mengi sana na mengine kumsingizia Mh Raisi. Alichosema Mhe SSH ni kwamba TRA wafanye kazi kwa mujibu wa sheria na wasimuonee mtu katika utendaji wao wa kazi.Hivo TRA wanawajibiu wa kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.Navyofahamu mimi kama tax consultant TRA huwa sheria inawaruhusu pale ambapo mteja hatoi ushirikiano wa kutosha wanaweza tumia taratibu zingine za kisheria ili kuweza komboa mapato ya serikali.Mfano kama mtu anatumia lap top kuiba kodi unategemea hizo lap top zisifanyiwe uchunguzi kubaini wizi wa kodi?

Kama mtu kajazishwa form ya kuonyesha nini wamechukua tatizo lipo wapi huo siyo wizi. Je mwenyebiashara yake mwenyewe kasemaje kaibiwa? Wakati mwingine tusipende kuwalaumu TRA pasipo na sababu za msingi. Nadhani ni vizuri tuzisome sheria tuzijue na hata mkija kwetu tax consultant tunaweza wasaidia kufahamu.
 
Hawa watu ni Tatizo ktk hii nchi, Raisi aweke wakurugenzi kutoka nje kama Majirani zetu ambao wana weledi wa namna ya kufanya kazi kwa pamoja kati ya wafanya biashara na Serekali, kuweka mifumo ya kieletronic ili walipa kodi wasionane na hwa watu, na waondolewe kinga ya kutokushitakiwa wanapobambikia watu kodi na wakivamia maofisi ya watu washitakiwe kama wao na si Serikali
Ndugu huu utakuwa wivu sasa. Mtawaonea sana viongozi wa tra , tulipe kodi ndugu zangu tunazostahili sidhani kama kutakuwa na mgogoro au malalamiko yoyote. Tujiulize ITV hapo kuna viwanda vingapi kwanini awe huyo tu?
 
Hakuna wa kulipa Kodi bila shuruti
Huo ndio ukweli ambao inabidi tulazimike kuukubali. Kizazi cha sasa hakikuandaliwa kimaadili kiasi cha kuweza kufurahia na kuona fahari ya kulipa kodi bila shuruti. Inabidi tu TRA mara nyingi watumie nguvu kuwalzzimisha watu kulipa kodi stahiki. Walipa kodi wengi huficha mapato yao halisi na wengi hawapendi kutoa risiti za EFD na sisi wote hapa ni mashahidi.
Kwa sasa serikali ijipange kuandaa kizazi kijacho kuwa cha walipa kodi wazuri. Elimu ya kodi ifundishwe kuanzia darasa la kwanza. Kwa sasa hakuna mtanzania atakayeshangaa kuona taxi bubu gesti bubu nk. Vyote hivyo maana yake ni kukwepa kodi!
 
Mwamba una akili sana. Umewaza Mbali. Nataka niandike Maoni kwa SSH, aongezee mkazo. Asiishie alichosema, aseme pia kuwa walipa kodi wanao wajibu wa kulipa kodi bila shuruti pia. Yeye aliwasema tu TRA. Mheshimiwa Rais pale kidogo aliteleza. Juzi nimemuona RC wa Mwanza bwana Chalamila anasema hotuba ya Rais ingeendelea, maana yake angesema Wafanyabiashara nao walipe kodi bila shuruti, lakini Mheshimiwa Rais hilo hakulisema.

Kingine naona mleta uzi pia hajazingatia mamlaka waliyo nayo TRA, naye kwasababu ya SSH anaona TRA wabaya. Kodi ni Sheria na imeweka hatua zote za kuchukua kama mtu hajalipa kodi halali na pia Sheria hiyo hiyo inampa Mlipa kodi mwaya wa kukata rufaa mpaka kufika mahakamani akionewa.

Jamani Mh. SSH, badilisha kidogo kauli.
Ungekua na biashara hata ya genge basi kodi unalipa baada ya kupata faida mzunguko wa biashara Uko kimya serekali inapaswa kutoa maelezo juu ya mdololo wa uchumi watueleze wamekosea wapi bila mifumo yote kwenda sawa lazima kuwe na tatizo nani ataende kulipa kodi pesa itatoka wapi?
 
  • Thanks
Reactions: Lob
Back
Top Bottom