TRA - Napasuwa Ufisadi Mwingine!

sasambuwa two

Member
May 22, 2008
5
0
Ufisadi mwingine unajulikana wazi lakini kwa kuwa umewatajirisha wanene, wengi wao, mpaka wakubwa wa polisi wanapokea mishahara kutoka kwa haka katajiri fisadi. Haka katajiri kanafumbiwa macho na Takukuru na Usalama wa Taifa na hata hiyo polisi yenyewe. Kwa nini? Kwa sababu tuu eti haka kajitu kana fedha na kana kutajirisha kwa kukaachia ukalinde (mafia style). Kana julikana sana haka kajitu kwa kutembelewa na wanene wa TRA na hata mkuu wa kanda maalum ya polisi alikuwa akimtembelea, bila shaka kuchukuwa chake.

Kafisadi haka (kwani ni kajitu kadogo tu, wala hukadhanii) kametajirika kwa record time kwa kushirikiana na mafisadi wenzake wa mostly TRA na sehemu zingine kama vile polisi na wizara ya mambo ya ndani (kwa protection). Kameshasikika kakisema kuwa, hakuna ataeweza kumkamata kwani ana akili nyingi sana na amesha torosha fedha nyingi sana (alizozipata kwa ufisadi) kwa hiyo, kwa sasa hakuna mwenye ujanja wa kumkamata wala kumfikisha mahakamani kwani kanajigamba kuwa kana juwa kula na wakubwa na kucheza na makaratasi.

Mbinu moja ya kifisadi aliyotumia kujitajirisha haraka na ambayo anajigamba kuwa imemtajirisha yeye, na wafanya biashara wengine aliokuwa akiwahudumia na maafisa wakubwa wa TRA (wengine wameshaachishwa kazi lakini washajilimbikizia mali kibao kwa njia za ufisadi walipokuwa kazini), ni ya kuwa clearing agent asiye rasmi. Ki-vipi asiye rasmi? Kwa kushirikiana na baadhi ya mafisadi wa TRA, alikuwa akifunguliwa kampuni za ku-clear mizigo (of course) siyo kwa jina lake, na alikuwa anawaambia matajiri wengi tuu wanaoleta mali kutoka China, Dubai, India na kwingineko watumie kampuni zake, yeye mara nyingi hutowa huduma ya kusafirisha mizigo (containers) toka inapotoka na kui-clear kwa kutumia bandari ya Dar. Na mingine kupitia bandari ya Mombasa na kupitia mipaka ya Kenya na Tanzania, ambako kote huko aliji/walijijengea ka-network chao, yeye, mafisadi wa TRA na polisi ambapo mizigo hiyo anayoihudumia yeye (of course kwa majina yale ya kampuni ambazo si kwa jina lake) hutolewa kwa kulipiwa ushuru mdogo sana. Huwa wanamwambia mwenye mzigo (mteja wao), wewe tutakuchaji million 7 au 10 au 15 au 20 kwa kukutolea kontena lako kila kitu inclusive mpaka tunakukabidhi mwenyewe, wao wanahakikisha gharama zote za kulipia na kulifikisha kontena mpaka kwa mteja halizidi million mbili au tatu au ikizidi sana million tano, zinazobaki ndio mgao wao, yeye na TRA na kina polisi hao wanene huambulia chochote wafunge macho na midomo yao.

Volume ya biashara na (makampuni yaliyosajiliwa na kubarikiwa na TRA kwa zoezi hili) ni kubwa kiasi cha kutamba kuwa alikuwa anaingiza mpaka billioni moja kwa mwezi na hii ni kwa muda mrefu.

Katika Mali alijzojilimbikizia kwa muda mfupi, of course anasema yeye ni mjanja na hawawezi kumshika kwa kuwa mali hizo zote au nyingi katika hizo hajatumia jina lake na hutumia majina ya ndugu, jamaa na marafiki ni pamoja na majumba kadhaa ya Ghorofa Kariakoo, kiwanda, viwanda vya mashuka na mito ambavyo mpaka leo vina exemption za ushuru kwa kutumia mtandao wake na loop-holes za sheria za exemptions, hoteli aliyoinunuwa kwa US$ 8 million hapo Dubai, Hoteli aliyoinunuwa kwa US$ 6 million huko kwao Yemen (asili ya babake ni myemeni, mama yake ni mtanga na ana udugu au ujamaa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa zamani na baadae balozi wa Tanzania uchina na mpaka sasa ni partner wake wa kisiri katika huu ufisadi, aidha kibiashara au kiulinzi (God Father)). Majumba masaki, Dar., majumba keko, majumba mikocheni na kwingine kwingi. Maduka Kariakoo, Uhindini, Mlimani complex, Arusha, Zambia na kwingine kwingi tuu.

Ukitazama mali zote anazomiliki yeye, na ndugu zake na muda alioishi Tanzania, na biashara za halali alizonazo (mwenyewe anaziita "danganya toto") hata uzipigie hesabu maisha huwezi kuja na jibu la faida za kuweza kutajirika kiasi hicho kwa muda mfupi, kwani kwa kipindi kirefu alikuwa nje ya Tanzania na huko nje alikuwa akiajiriwa vikazi vya kawaida na si vya kumpatia utajiri aliokuwa nao, utaona kwamba kaweka mtandao wa kifisadi wa hali ya juu, na anatamba kuwa ana akili anajulikana na hakuna wakumfanya chochote wanene wengi kawatajirisha na wapo mfukoni mwake.

Huyu si mwingine bali ni Saidi Saad au almaarufu kama Saidi Mahonda anajulikana sana Dar. Kwa machachari yake, dharau zake, dhuluma zake (nyingi tuu) na anatambia fedha zake za ufisadi.

Takukuru, Usalama wa taifa, mawaziri waadilifu, waathirika wa ufisadi mnafanya kazi gani au na nyinyi kawatia mfukoni?

Tushirikiane kufichuwa mafisadi.
 
Habari ni nzito, jee kuna ukweli? au ni chuki binafsi?

Dar. Ni habari nzito kweli na nimezifupisha sana kwa kuwa uandishi si fani yangu. Ndio kuna ukweli mtupu na kama kuna sehemu unataka ufafanuzi na unamashaka nayo basi uliza niiweke wazi zaidi. Yes, kama kuuweka wazi ufisadi ni chuki binafsi, basi jibu ni ndio, nina chuki binafsi na mafisadi wote wanaojilimbikizia mali za wa Tanzania wote na wanaacha wa Tanzania wengine wanakufa kwa kukosa au kushindwa kumudu hata dawa za malaria kwa kuwa tuu mali zao zinaliwa na mafisadi wachache wenye uchu wa fedha na wako tayari kuzipata kwa njia yoyote bila kujali maisha ya yeyote na maslahi ya walo wengi.

Jee, Dar. wewe huna chuki binafsi na watu kama hawa?
 
Huyu Saidi Aliwahi Kusoma Mzumbe Au Ifm ?

Huyu saidi mahonda hajawahi kusoma Mzumbe wala IFM, nimjuavyo mimi hana IQ ya kusoma huko.

Na kwa mujibu wa habari nilizozipata sasa hivi, hivi karibuni amemuajiri Miss Tanzania wa kidosi kama secretary wake na ninavyoambiwa ndio yeye alimnunulia huo umiss kwa thamani kubwa sana (hili sina uhakika nalo nimelipata sasa hivi). Lakini ni kweli kamuajiri Richa Adhia.
 
....... huko kwao Yemen (asili ya babake ni myemeni, mama yake ni mtanga na ana udugu au ujamaa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa zamani na baadae balozi wa Tanzania uchina na mpaka sasa ni partner wake wa kisiri katika huu ufisadi, aidha kibiashara au kiulinzi (God Father))............

Hii habari inaukweli mwingi sana, kwani hilo la ufisadi kupitia clearing agency lilianza tangia enzi za RUKSA. Sasa huyo mhesimiwa balozi Omar R. Mapuri anajisikia vipi kumlinda FISADI?? Halafu kumbukeni kuwa huyu ndo alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM. Inasikitisha!!!
 
Mhh sounds true but ... angalau tungepata wala viji-document kusubstantiate hizi claims,wenzako walioibua issues za TPB,ATC,Buzwagi,Richmond,BOT walikuja na documents na kuanzia hapo matokeo yake yanaonekana...
 
Hii habari ni nzito sana... lakini mwisho wa yote haya nini jamani?
Hii nchi ni ya Watanzania wote na si ya hao mafisadi pekee. Mali na rasilimali yote inapaswa kuwanufaisha wavuja jasho na walala puuu wote.
Maana tutasema sana lakini hakuna kinachofanyika na rasilimali za nchi ndio zinazidi kumalizwa na mafisadi.
Viongozi na taasisi zilizopewa majukumu ya kulinda rasilimali za nchi wao ndio wako mstari wa mbele kulinda wanao tafuna rasilimali hizo!
Mafisadi ambao ni viongozi wa nchi baada ya kugunduliwa madhambi yao, wameona dawa ni kujiuzulu na kuendelea kupeta kwa uhuru zaidi kutumia viji senti vyao! Jamani hivi hii nchi imekosa wa kuinusuru kabla ya kufutika kabisa katika ulimwengu huu? Mimi nawaachia wenzangu ili nanyi mchangie.
 
Katika Mali alijzojilimbikizia kwa muda mfupi, of course anasema yeye ni mjanja na hawawezi kumshika kwa kuwa mali hizo zote au nyingi katika hizo hajatumia jina lake na hutumia majina ya ndugu, jamaa na marafiki ni pamoja na majumba kadhaa ya Ghorofa Kariakoo, kiwanda, viwanda vya mashuka na mito ambavyo mpaka leo vina exemption za ushuru kwa kutumia mtandao wake na loop-holes za sheria za exemptions, hoteli aliyoinunuwa kwa US$ 8 million hapo Dubai, Hoteli aliyoinunuwa kwa US$ 6 million huko kwao Yemen (asili ya babake ni myemeni, mama yake ni mtanga na ana udugu au ujamaa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa zamani na baadae balozi wa Tanzania uchina na mpaka sasa ni partner wake wa kisiri katika huu ufisadi, aidha kibiashara au kiulinzi (God Father)). Majumba masaki, Dar., majumba keko, majumba mikocheni na kwingine kwingi. Maduka Kariakoo, Uhindini, Mlimani complex, Arusha, Zambia na kwingine kwingi tuu.

QUOTE]

mzee hii part inahitaji documents....

Vipi yeye anasemaje navyo ni vijisent au? maana naona zipo in term of US Dollars
 
No place tu hide, kila sehemu ufisadi tu, what should we do. Sasa naamini kuwa Tanzania inaweza kucover budget yake kwa 100% provided hakuna madudu ya aina hii.
 
Mhh sounds true but ... angalau tungepata wala viji-document kusubstantiate hizi claims,wenzako walioibua issues za TPB,ATC,Buzwagi,Richmond,BOT walikuja na documents na kuanzia hapo matokeo yake yanaonekana...

ibambasi, sina document yoyote kwa sasa zaidi ya kutowa hilo jina na zaidi yapo ni biashara zake za maduka anaziita home shopping centre. Nina uhakika kama takukuru au wahusika wowote serikalini kama ambao nadhani bado wapo wenye nia ya kweli ya kuwasaidia wa Tanzania huo ni mwanzo mzuri kwao. Jina la biashara ya halali? ni hilo na jina lake ni hilo hapo juu. Waanzie hapo, na kila nitapopata data zaidi nitawasilisha. Tunaambiwa tushirikiane na vyombo vya dola kufichuwa ufisadi, lakini ukitazama hata kina mzee tiba wanamtembelea huyu mtu ofisini kwake, si unaona ni kwa nini tunakuja kuyasasambuwa haya humu JF. Na kama kweli serikali wanania ya kupigana na ufisadi basi waanzie hapa na tuone.
 
No place tu hide, kila sehemu ufisadi tu, what should we do. Sasa naamini kuwa Tanzania inaweza kucover budget yake kwa 100% provided hakuna madudu ya aina hii.

Hata mimi nakuunga mkono nina uhakika kabisa wa hilo na hatuna haja ya kuwa omba-omba ili mradi tuupige vita ufisadi tuu.
 
Labda tuanze mkakati wa kuwachoma moto hawa jamaa kama wa south wanavyowafanyia unyama ma black wenzao. Tuwatokomeze hawa jamaa waishilie mbali. Kuna haja ya kuunda Mungiki ya Bongo. Hali hii inakera saaana, na inatuumiza mno!
 
Lisemwalo lipo kila siku ukipita Dar barabarani mifumo ni mibovu ya maji taka na ukijiuliza serikali inafanya nini huoni labda aje kiongozi kama GW Kichaka kutoka Marekani tena sijui huu utamaduni waTZ tumeupata wapi? Kila kitu ni zima moto
 
Hao au hayo majina yanatosha kwani anaekamatwa na ngozi ndie mwizi na hayo majina yakiwa na ukweli basi mtungo mzima utapatika yeye akiwa wa mwisho na tatizo la nyama ya mshikaki ile ya mwisho ndio inayoliwa mwanzo na kukumbana na masaibu ya meno.
 
Mhh sounds true but ... angalau tungepata wala viji-document kusubstantiate hizi claims,wenzako walioibua issues za TPB,ATC,Buzwagi,Richmond,BOT walikuja na documents na kuanzia hapo matokeo yake yanaonekana...

Nakuunga mkono ndugu yangu, ushahidi ni muhimu, bila ya kusahau na Kajipicha kake japo tuweze kumjua.
 
Katika Mali alijzojilimbikizia kwa muda mfupi, of course anasema yeye ni mjanja na hawawezi kumshika kwa kuwa mali hizo zote au nyingi katika hizo hajatumia jina lake na hutumia majina ya ndugu, jamaa na marafiki ni pamoja na majumba kadhaa ya Ghorofa Kariakoo, kiwanda, viwanda vya mashuka na mito ambavyo mpaka leo vina exemption za ushuru kwa kutumia mtandao wake na loop-holes za sheria za exemptions, hoteli aliyoinunuwa kwa US$ 8 million hapo Dubai, Hoteli aliyoinunuwa kwa US$ 6 million huko kwao Yemen (asili ya babake ni myemeni, mama yake ni mtanga na ana udugu au ujamaa na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa zamani na baadae balozi wa Tanzania uchina na mpaka sasa ni partner wake wa kisiri katika huu ufisadi, aidha kibiashara au kiulinzi (God Father)). Majumba masaki, Dar., majumba keko, majumba mikocheni na kwingine kwingi. Maduka Kariakoo, Uhindini, Mlimani complex, Arusha, Zambia na kwingine kwingi tuu.

QUOTE]

mzee hii part inahitaji documents....

Vipi yeye anasemaje navyo ni vijisent au? maana naona zipo in term of US Dollars

Ni kweli kama kutakuwa na documents itaongeza uzito na ushahidi zaidi. Hata hivyo mafisadi kuwapata kwa documents kazi kweli kweli.
 
Mafisadi wa design hii ni wengi sana.Na ufisadi kusema kweli uko nchi nzima.Vyombo vya kisheria havina meno kwa hawa majambazi.Wana influence kila mahali.

Ni watu wa kutoa michango haraka haraka kwenye dhifa mbalimbali.Ni watu wanaoweza kufanya lolote ili kubaki katika life style waliyonayo.

Hata hivyo kuwataja pekee haitoshi.Tunahitaji kupata haidhuru nyaraka zinazoweza kutupa pa kuanzia.

Mimi naona kila ofisi ya serikali ya jiji au serikali kuu ninayoifikia nikiwa na shida ya kuhudumiwa napewa maswali na masharti ya kifisadi ili niache pesa pale.

Najitahidi kuwa mtu mwaminifu lakini katika shughuli najikuta nina mafisadi wa ofisini hadi barabarani ninakopita.

Sheria zimewekwa lakini wenye kitu wanazipinda na kuchukua wanachokiona madhali wana power ya pesa.

Ndugu zangu wa JF tunaweza kweli kunyoosha mambo hapa nchini? Tunawezaje kuishi bila ufisadi? Mtu umelala na ukiamka asubuhi unakuta open space mtu kajenga.

Watu wanatengeneza documents fake na kukopa mabilioni kisha wanapotea lakini wewe mwenye kibanda cha halali unafika benki na kupewa masharti kibao hadi unakata tamaa ya kupata mkopo.Ufisadi umeemea kila mahali,kwenye vyombo vya fedha,vyombo vya kutoa huduma na hata vyombo vya sheria.

Nani atuokoe jamani genge la wajivuni limeshika kila kitu? Twende wapi?
 
Back
Top Bottom