TRA- Nani anapanga kupanda,kushuka au special discount za bidhaa?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Unaingiza mzigo Tanzania, TRA wanapiga gharama za kodi wanakutuma ulipe Kodi husika..ukifika kwa wauzaji TRA wanasema lazima walipe VAT na hivyo kuelekeza kutolewa kwa risit ya kielectronic kwa kila bidhaa inayouzwa.

Kama nguo ilipangwa kuuzwa 100,000 ukiipa punguzo la asilimia 80% itauzwa Kama 20,000 na hii pesa ukikokotoa VAT haitakuwa kuwa sawa na VAT ya 100,000, itqkuwa pungufu.

Napenda kujua hii pungufu inalipwaje au inasamehewa? Means kwa tafsiri nyingine kila mfanyabiashara anayo mamlaka ya kuweka discount kwenye bidhaa zake?

Jambo la pili, Ni kwa namna gani TRA wanaweza kudhibiti Hawa wafanyabiashara wasidanganye kuuza mzigo kwa punguzo la 80% kumbe mzigo mkubwa unaingizwa sokoni kwa njia zisizofaa...mfanyabiashara kwenye duka A anaweka punguzo la 80% anakwenda kwenye duka jingine ambalo ana maslahi nalo anauza bei iaiyo na punguzo baada ya kipindi Cha punguzo kwisha.

TRA , kipindi Cha sikukuu Ni kipindi ambacho wafanyabiashara wanategemea kuuza bidhaa zao, kwa punguzo la 80% kwenye maduka ambayo wamiliki wake wanatiliwa mashaka hakuleti madhara kwa walipa Kodi walio wengi?

Tanzania, ni Nani mwenye mamlaka ya kuelekeza punguzo la bei za bidhaa?

Hasara inayopatikana na mfumo huu Nani anawajibika kuifidia? Huu siyo ule ule mchezo wa akina Quality ambazo tuliwatamka kuwa ni wezi?

Ni vigumu kuamini kwamba kampuni inaweza kuagiza mzigo kwa M100 ikauingiza sokoni kwa 20M.
 
Umeuliza swali zuri sana lakini kuna mambo hujayakumbuka. Nayo ni haya. Mpaka hapo hali hii itakapobadilika, VAT itaendelea kupotezwa;

a) Bidhaa zetu haziko coded ukiondoa pale wanapofanya calculation ya import duty. So hata kwa kutumia EFD machine - hakuna namna system inafahamu kilichouzwa ili VAT yake ni shilingi ngapi. Bidhaa zinapaswa kuwa barcoded na bei isomwe kutopia barcode reader!! Kama vile supermarket. Ndivo kodi sahihi hulipwa nchi zilizoendelea. Coding ni jambo gumu sana.

b) EDF inatoza kodi ya VAT kwa pesa zilizolipwa kwa mpokeaji, sio sana bei ya bidhaa. Hapa linakuja swala la uaminifu na wajibu kwa muuzaji na mnunuaji. Kuna faida katika kukwepa kulipa kabisa VAT au kulipa kidogo. Ni kwa sababu uangalizi wa VAT hauko. Nchi kama Kosovo ina watu wa mamlaka ya mapato mitaani ambao wanaonekana kama raia tu. Wako mitaani wakitafuta wakwepa kodi. Ukitoka dukani mita 50 na ukakutwa una bidhaa uliyonunua na huna receipt. Unashitakiwa kwa kukwepa kodi wewe na muuzaji. Adhabu zake ni kubwa sana kwa muuzaji - anapoteza leseni na kupigwa faini.

Bado tuna safari ndefu hapa nyumbani. Ndio maana VAT yetu ni moja ya kubwa duniani - ni kwa sababu ni wachache wanalipa!
 
1. Umeituhumu mamlaka kana kwamba yenyewe inashiriki kupitisha mizigo isivyo halali na kupelekea watu kuwa na maduka mbadala.

2. Usitishike na bei zinazowekwa ukadhani wanakwepa kodi.

Unaelewa bei inatokea vipi? Kupewa discount hakumfanyi mtu kukwepa kodi sawa na bei inapokuwa juu zaidi hakumfanyi mtu kuzidisha kodi na kuwa amjinyonya ama kumuinea mnunuzi.

Ukielewa mtiririko wa kodi ya ongezeko la thamani wala hutaumia kichwa na hizo discount.


Sent using iphone pro max
 
Back
Top Bottom