TRA Namanga wakamata spares ndani ya Sanduku la kubebea Maiti

FIFA

Member
Dec 7, 2011
71
70
Kampuni moja ya kutengeneza barabara ya Kichina ikimtumia mzawa kupitisha spea na vifaa vingine vihusikavyo na ujenzi wa barabara hapa Tz vilikamatwa jana mpakani ( Namanga ) kwa kuviweka ndani ya sanduku la kubebea maiti.Bahati mbaya jamaa hakuwa na document zilizo jitosheleza wakati wa ku clear huyo maiti ndipo TRA wakaamua kufungua hilo sanduku ili wajiridhishe maana jamaa alishindwa kutoa maelezo kwa ufasaha, mara baada ya kushindwa hata kutaja jina la marehemu ndipo waliamua kufungua sanduku nakukuta ni spares.Inasemekana huyo jamaa ndio kazi yake ya kupitisha mali za wachina bila kulipia ushuru.
 

Malipo kwamungu

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
575
195
NIA YETU NI :UAMINIFU,HAKI,UTII,Sijui wangapi wetu wanafuata hata moja katika hayo? hata kama hujafika kuangalia au kushangaa maneno hayo huko CCP MPS
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,153
2,000
Watanzania tunajinyima mapato kwa kuwaneemesha wachina, kweli sisi hamnazo
Wafanyakazi (walio wengi) wa TRA wameamua kukiuka msingi wa kazi zao kwa kuwa 'unfriendly' na walipa kodi na matokeo yake walipa kodi kila kukicha wanabuni njia mpya za kukwepa kodi amabacho sio kitu kizuri.
TRA wasipojirudi wataishia kuwanyanganya wanachi pesa kwa jina la kodi badala ya kujenga mazingira rafiki na kuaminiana na walipa kodi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom