Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,005
- 3,641
Nimesoma hotuba ya bajeti 2017/2018 nikagundua yafuatayo:-
1. Makusanyo ya fedha za kodi hayakufikia malengo .
2. Biashara elfu 7 hivi zimefungwa,na laki 2 hivi zimefunguliwa.
3. Bajeti ya maendeleo imetekelezwa chini ya 40%.
4. Waziri wa fedha anasema uchumi umekua kuliko huko nyuma.
Sawa ninajiuliza mambo kadhaa kuhusiana na yaliyoelezwa hapo juu.
A. Kama biashara zimefunguliwa nyingi kuliko zilizofungwa,kwa nini makusanyo ni kidogo?
B. Kama uchumi umekua,kwa nini uwekezaji/ utekelezaji miradi ya maendeleo umeshuka kiasi hicho? Nimegundua aidha kuna mahali hapako sawa na maelezo ya hotuba ya bajeti yamefunika jambo na unatakiwa utafiti makini.
Nitaeleza kidogo kwa uelewa wangu.
I) Biashara elfu 7 zilizofungwa,kuna uwezekano zilikuwa na mtaji mkubwa zaidi kuliko biashara laki 2 zilizofunguliwa. Yaani wafanyabiashara wameshift kutoka biashara kubwa kwenda biashara ndogo (umachinga) ambazo kodi hakuna au ni kidogo sana.
II). Uchumi kwa maana ya GDP,umeonekana kukua kutokana na matumizi makubwa yaliyotokana na inflation (dola imepanda mara kadhaa), na uwekezaji umeshuka ( ambapo imejionyesha kwenye bajeti ya miradi ya maendeleo 40%). Na kwa vile uwekezaji umeshuka,hakuna uuzaji mkubwa wa bidhaa nje. Hivyo,ni dhahiri,dhana ya uchumi kukua kunakosemwa kuangaliwe kwa jicho la tatu.
Maoni yangu:-
i). Kiwango cha kodi kinachotozwa wafanyabiashara
/wawekezaji wakubwa na hata wa kati,kiangaliwe upya ikibidi kipunguzwe,ili wengi waingie na kodi ipatikane zaidi.
ii). Mwananchi anayeanza biashara asianze hapohapo kulipa kodi,apewe grace period ya miezi 3 au 6 ndiyo aanze. Hapo nyuma ilikuwa hivyo,na hata nchi jirani kama Zambia (walikokimbilia wengi),wanafanya hivyo. Kwa kufanya hivyo, biashara nyingi na zenye tija zitafunguliwa,mapato yataongezeka.
iii). Maafisa wetu wa TRA,Biashara na BRELA,wasikae tuu maofisini kucheza na kompyuta,wawatembelee /wawekezaji /wafanyabiashara wajue hali zao,watoe elimu nk. Na wasisubiri tu maofisini kuletewa na kupokea barua za kufunga biashara! Na ikitokea eneo fulani,biashara nyingi ziimefungwa,maofisa hawa wawajibishwe.
iv). Ikitokea mfanyabiashara ana deni la kodi,isiwe ni sababu ya kufungiwa au kukamatiwa mali. Zifanyike logical negotiations ikibidi alipe kidogokidogo hadi amalize. Kwa kufanya hivyo,TRA,wataendelea kupata mapato kwa mtu huyu miaka nenda rudi kuliko angefunga.
v).TRA,iwe ni Agency kwa maana ijitegemee. Isibanwe ndani ya Wizara ya Fedha kuepuka wakati mwingine kutumika kisiasa. Ifanye kazi kitaalamu zaidi na autonomously.