TRA na ujanja wa leseni za wakala wa forodha (clearing & fowarding)

Nomile

Member
Dec 5, 2012
99
122
Kwa Wadau wote. Hivi majuzi TRA waliitisha maombi kwa makampuni yanayoitaji kupata leseni za uwakala wa forodha, Katika Tangazo lao la tarehe 27/11/2014 (the guardian) Vigezo vilivyowekwa vilikua na AJENDA ya sili,katika hari ya kawaida kila mhitaji analuhusiwa kuomba leseni provided anavigezo na sifa stahiki Tatizo ni kwamba masharti yaliyowekwa ni ya kibaguzi katika mazingira yafatayo 1.kwanza walengwa ni wale wenye makampuni ambayo yalishakuwepo na si kwa kampuni mpya iliyosajiliwa hivi karibuni.2 Bank Guarantee ya 100,000,000 kiasi hiki ni kikubwa kwa kampuni mpya na hata zile zinazoendelea, maana ili bank wakupe hiyo guarantee lazima uwe na vigezo stahiki , kitu ambacho sio rahis kupata kwa makampuni mengi ya wazawa, 3. Working Capital ya 50,00,0000 hiki ni kiasi kikubwa kwa Mtanzania ambaye ameamua kujiajiri kama serikali inavotuimiza vijana kujiajiri. ikumbukwe kwamba kulikuwepo na kilio cha mda mrefu kwa mamlaka kuruhusu kutolewa kwa leseni hizo sasa tunaona wazi kwamba zoezi hili limelenga kuwanufaisha baadhi ya walengwa na wenye maslahi binafsi na TRA. Tunatoa wito kwa mh,Naibu Waziri Mwiguru Nchemba Ulione hili sisi vijana tulioamua kujiajiri mazingira haya tutaweza wapi? Ni matumaini yetu kwamba Mh,ulitazame hili kwa jicho pevu.
 
Kuna muarabu ameshaona kuna ushindani kwenye kampuni yake, ameamua kuitumia TRA kusitisha hizo huduma.
 
Back
Top Bottom