TRA na mfumo mpya wa kufanya valuation of Used Vehicles

Wao wanadhani Tz ni Dar es Salaam tu, wanasahau kwamba kule vijijini hata hizo barabara tu ni shida achilia mbali magari. .... sio kwamba hapa Tz tuna kiwanda cha kutengeza magari ambacho tunakilinda. Hawa watu ni majuha sana.

Sijaelewa kama hawa walibuni utumbo huu ni wanauchumi wa ukweli! Yaani kwao Tanzania ni Dar peke yake, kuwakomoa watu wa Dar ina affect nchi nzima. Huu ni ujuha nambari wani. Tanzania hakuna kiwanda cha magari tunachokilinda, sasa kuweka mfumo huu ni kwa faida ya nani?

Kitilya na TRA yake wajivue gamba la kutumikishwa na wanasiasa.

,
 
Hawa watu mie siwaelewi, hivi mtu mwene gari akiamua kuuza gari lake kwa dola 3000. Kwanini TRA im-penalize mnunuzi na kumwambia kwamba hili gari lina thamani ya dola 6000? Kwanini? siwezi kupata jibu. Kwanini nilipie bei ambayo ni ya kufikirika? hilo ongezeko ni la nini? na kwanini nilipe mimi mnunuzi?
 
Usafiri wa umma wenyewe hivi una exists?? mi naona tu kila mtu anaishi kibahati bahati very close to anarchy. Hivi kweli Tz tunaeza kusema tuna public transport? tuna takwimu zozote za magari, abiria, muda wa safari n.k?

Mi ninafikiri TRA haijapata wataamalu wenye uelewa wa kutosha. Usafiri ni njia moja wapo inayomaliza tatizo la ajira duniani. kwa sababu kutokana na mihangaiko na mizunguko itakayokuwepo mahali panapo husika. Na ndio maana nchi zilizoendelea zinalinda sana na zimeweka mpangilio mzuri ili kila mtu awe na usafiri kutokana na unafuu anaouona mtumiaji, mradi usitumie hicho chombo vibaya kama mlevi, wizi nk. Na ndio maana wamejitahidi kuboresha barabara zao ili shughuli za kuwasumbua raia zisitokee. Yaani ninasema mazao tulio nayo na madini na rasilimali nyingine tulizo nazo TRA wakitengeneza njia nzuri za ukusanyaji wa mapato watapata hela nyingi sana. Swala ni kuwaelimisha wananchi na kuwafungia calculeta ya computer ambayo inatoa mahesabu arudishe hela yake na kodi ni kiasi fulani na hii mashine inampa risiti hapo hapo. Kama mtu atauza bila kutoa au kupokea risiti iwepo faini. TRA wawe na kikosi chao kama cha polisi sio hawa polisi feki tulionao sasa hivi ambacho kitakagua hata kama kodi itakuwa ndogo kila mtu atalipa na ukwepaji utakuwa ni mgumu. Waache uhuru kwa mali zinazo toka nje ili wananchi wawe na ubunifu wa kutosha, lengo ni kujenga taifa letu.
 
Wala msiumize vichwa, serikali itashuhudia kuporomoka kwa mapato yatokanayo na uagizaji wa magari nje ya nchi
 
siyo kwamba wataanza july mosi,wameanza june 1.ni kilio hata kwangu we acha tu nimepigwa kodi hiyo cjawahi pata cna hamu!
 
Kama hujaipata hii basi jiandae!!!!!!

Tarehe 1 July 2011 TRA wanaplan kuintroduce system yao mpya kwa ajili ya valuation ya used motorvehicles...

Mfumo mpya utakuwa kama ifuatavyo...Used vehicles zitakuwa valued on either ex-factory FOB au market value in local market...

Nianze na ex factory FOB..

Kwenye mfumo hu, TRA wataestablish database itakayo kuwa na bei za magari kipindi yameingizwa sokoni kwa mara ya kwanza...labda nitoe mfano mana kidogo ina mahesabu

Mfano: Mtu akiagiza gari aina ya Toyota Premio 2001 model..hapo ina maana hii gari imezidi miaka kumi tokea itengenezwe...kwa hilo bei pungufu itakayoruhusiwa ni asilimia 70% ya bei ilipoingia sokoni kwa mara ya kwanza..PREMIO bei yake ya awali sokoni ilikuwa USD 40,000 kwa huko Japan...

Kwa maana hiyo FOB ex factory itakuwa USD 40,000 toa 28,000 (70% of USD 40,000) = USD 12,000 na hiyo ndo itakuwa Customs Value ambayo itakuwa subjected kwenye Import Duty, Excise Duty, VAT na uchakavu (kama upo)....

Kwa namna hiyo kodi jumla itakuwa kama ifuatavyo

Import duty (ID)=0.25*12,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(12,000+0.25*12,000)
Excise (E) =0.1*(12,000+0.25*12,000)
VAT= 0.18* (12,000+ID+DF+E)

Hii ni tofauti na bei za sasa ambazo weza kuagiza premio ya mwaka 2001 kwa CIF ya USD 3,000 to USD 3,500...na kodi ingekuwa kama ifuatavyo
ukiweka na uchakavu

Import Duty (ID)=0.25*,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(3,000+0.25*3,000)
Excise (E) =0.1*(3,000+0.25*3,000)
VAT= 0.18* (3,000+ID+DF+E)

Market Valuation Method

Kwa market value method watachukua bei za sokoni Tanzania na kutoa profit margin ya asilimia 25 na kutoa gharama za kodi zilizolipiwa ili waweze kupata CIF kipindi gari linaingia nchini...Mfumo huu utatumika pale tu ambapo bei halisi wakati gari linaingia sokoni kwa mara ya kwanza itakuwa ni vigumu kujulikana...

My take:
Je hii ndiyo njia ya kupunguza foleni za magari Dar? na je vipi kule ambapo bado kuna shida ya usafiri itakuwaje?

Kaka naomba kuelewesha wanatumia FOB au CIF . maana siku zote naona wanatumia CIF yaani wanakata kodi hat gharama za usafirishaji, bima .Nikitazama hapo juu ni kwamba mteja atalazimika kulipa kati ya asilimia 60-80 ya gharama ya CIF. hii ni kodi kubwa kupata kutokea duniani.
Naomba kuelewa hii ni kwa magari yote ama kuna kategory ? wenye data kamili naomba washushe hapa JF tuelimike.
 
Kama hujaipata hii basi jiandae!!!!!!

Tarehe 1 July 2011 TRA wanaplan kuintroduce system yao mpya kwa ajili ya valuation ya used motorvehicles...

Mfumo mpya utakuwa kama ifuatavyo...Used vehicles zitakuwa valued on either ex-factory FOB au market value in local market...

Nianze na ex factory FOB..

Kwenye mfumo hu, TRA wataestablish database itakayo kuwa na bei za magari kipindi yameingizwa sokoni kwa mara ya kwanza...labda nitoe mfano mana kidogo ina mahesabu

Mfano: Mtu akiagiza gari aina ya Toyota Premio 2001 model..hapo ina maana hii gari imezidi miaka kumi tokea itengenezwe...kwa hilo bei pungufu itakayoruhusiwa ni asilimia 70% ya bei ilipoingia sokoni kwa mara ya kwanza..PREMIO bei yake ya awali sokoni ilikuwa USD 40,000 kwa huko Japan...

Kwa maana hiyo FOB ex factory itakuwa USD 40,000 toa 28,000 (70% of USD 40,000) = USD 12,000 na hiyo ndo itakuwa Customs Value ambayo itakuwa subjected kwenye Import Duty, Excise Duty, VAT na uchakavu (kama upo)....

Kwa namna hiyo kodi jumla itakuwa kama ifuatavyo

Import duty (ID)=0.25*12,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(12,000+0.25*12,000)
Excise (E) =0.1*(12,000+0.25*12,000)
VAT= 0.18* (12,000+ID+DF+E)

Hii ni tofauti na bei za sasa ambazo weza kuagiza premio ya mwaka 2001 kwa CIF ya USD 3,000 to USD 3,500...na kodi ingekuwa kama ifuatavyo
ukiweka na uchakavu

Import Duty (ID)=0.25*,000
Dumping Fees (DF) =0.2*(3,000+0.25*3,000)
Excise (E) =0.1*(3,000+0.25*3,000)
VAT= 0.18* (3,000+ID+DF+E)

Market Valuation Method

Kwa market value method watachukua bei za sokoni Tanzania na kutoa profit margin ya asilimia 25 na kutoa gharama za kodi zilizolipiwa ili waweze kupata CIF kipindi gari linaingia nchini...Mfumo huu utatumika pale tu ambapo bei halisi wakati gari linaingia sokoni kwa mara ya kwanza itakuwa ni vigumu kujulikana...

My take:
Je hii ndiyo njia ya kupunguza foleni za magari Dar? na je vipi kule ambapo bado kuna shida ya usafiri itakuwaje?

Hakika huu ni upuuzi tunaofanyiwa. Kwani lengo la wananchi kuiweka serikali ni kuwa waliopewa madaraka wahakikishe mwananchi hapati ugumu wa maisha, sasa inakuwaje tena huyo boss wa TRA anawatufanyia haya watanzania? ivi hiyo kodi anaipandisha kwa manufaa ya nani? kama ni watanzania basi asingepandisha ili kuwapa nafuu ya kimaisha aone kama serikali yake italalamikiwa. Sikufichi mie vitu vingine huwa vinanichefua kiasi kwamba natamani huyo aliyetoa wazo hilo afukuzwe kazi, kwani hatutendei haki. Gari japani iuzwe usd 1500 wewe uje uniambie hapana hiyo gari ni usd 12000? jamani ivi tunaenda wapi? basi kama hawataki watanzania wanunue magari watangaze tu ijulikane kuwa tumepigwa marufuku kununua magari. Au serikali ianzishe kiwanda hapa hapa nchini. Nchi ya sudani baada ya kuona usumbufu kuhusu magari walianzisha kiwanda cha magari GIAD wako poa na magari wanawauzia wananchi wao kwa bei nafuu sana. TRA kama wanaweza basi watuanzishie kuliko kuanzisha maajabu hayo
 
Serikali imekosea kumuweka mtu ambaye ana kinyongo na wivu kwa watanzania. Kama anafikiri itatusaidia kakosea, kwani wakiingiza watu wengi magari kodi itaongezeka, kuliko hivo au ana mpango na TRA ife? apate kufurahia.
 
Huu ni wizi na UKANDAMIZAJI wa mtu wa chini! Shida yetu na sisi ni kulalamika, hakuna hata mmoja wa kuchukua hatua! TUMEKWISHA!
 
Mi ninafikiri TRA haijapata wataamalu wenye uelewa wa kutosha. Usafiri ni njia moja wapo inayomaliza tatizo la ajira duniani. kwa sababu kutokana na mihangaiko na mizunguko itakayokuwepo mahali panapo husika. Na ndio maana nchi zilizoendelea zinalinda sana na zimeweka mpangilio mzuri ili kila mtu awe na usafiri kutokana na unafuu anaouona mtumiaji, mradi usitumie hicho chombo vibaya kama mlevi, wizi nk. Na ndio maana wamejitahidi kuboresha barabara zao ili shughuli za kuwasumbua raia zisitokee. Yaani ninasema mazao tulio nayo na madini na rasilimali nyingine tulizo nazo TRA wakitengeneza njia nzuri za ukusanyaji wa mapato watapata hela nyingi sana. Swala ni kuwaelimisha wananchi na kuwafungia calculeta ya computer ambayo inatoa mahesabu arudishe hela yake na kodi ni kiasi fulani na hii mashine inampa risiti hapo hapo. Kama mtu atauza bila kutoa au kupokea risiti iwepo faini. TRA wawe na kikosi chao kama cha polisi sio hawa polisi feki tulionao sasa hivi ambacho kitakagua hata kama kodi itakuwa ndogo kila mtu atalipa na ukwepaji utakuwa ni mgumu. Waache uhuru kwa mali zinazo toka nje ili wananchi wawe na ubunifu wa kutosha, lengo ni kujenga taifa letu.

Unachoongea ni sahihi kabisa. Ukiona serikali inakuwa na muelekeo kwamba usafiri ni starehe na anasa basi unajua tu kwamba tunaongozwa na watu wanaohifadhi makamasi kichwani. Hivi ktk dunia ya leo ni kitu gani ambacho hakitegemei usafiri wa uhakika? Sidhani kama kama kipo. Nadhani kwamba hata kama tungekuwa na kiwanda cha magari tunachohitaji kukikingia kifua soko lake au tunastrategize kupunguza foleni za magari, solution ya kwanza ilikuwa ni kuweka sawa usafiri wa umma. Usafiri wa umma kwa jiji kama la Dar kwa maoni yangu mimi ni non-existent, manake transport efficiency kwa hali ya sasa is close to zero. Kwamba safari fupi ya dakika 10 unaweza ukachukua hadi masaa 2, tungekuwa na utamaduni wa kuchukua takwimu, we would be surprised na hasara inayosababishwa na kutokuwa na usafiri wa uhakika.

Lakini kwa TRA I think we have a bigger fish to fry, maana sio usafiri tu, hata ukifanya transaction za kawaida na mtu ukimuuzia mfano nyumba au gari kwenda kubadili umiliki kimbembe cha TRA bado kipo palepale, wao TRA hujaga na ma-estimation yao, yaani unaeza nunua nyumba kwa milioni 20 wao watakuja na mkadiriaji wao na atabuni figa anayoijua yeye ambayo ianweza hata kuwa mara 2 yake!. Sijui ni commonsense ya wapi hii.
 
Nilikuwa nimepanga kuagiza ka corolla kangu ka mahesabu ya miln.9 walau na mimi niongeze nafasi moja ya ajira kwa dreva pamoja na wale waosha magari wapate riziki, ila kwa mtaji huu duh!
 
AKILI KAMA HIZI JUU YA NCHI YAKO MWENYEWE.....NADHANI ILIMFANYA YO YO AOMBE URAIA WA KENYA!
DOWN WITH THIS...!
RAIS UNAHUJUMIWA NA WATENDAJI WANAOTAKA KUONYESHA KUWA SERIKALI YAKO IMESHINDWA KUWAHUDUMIA WANANCHI WA KAWAIDA....!

ILI WAKIINGIA WATU WAO WARUDISHE MFUMO WA AWALI

TAKE CARE JK....... they are with you and they are not fighting with you
 
hiyo ndo wameona njia ya kuongeza mapato badala ya kubuni vyanzo vipya yahani wamekaa tu pale na nothing new to them na wanapokea mishahara mikubwa for nothing. Ilitakiwa wawe na kitengo cha research kwa ajili ya kuangalia opportunities za vyanzo vipya na sio kuzidi kuwapandishia gharama za maisha wananchi.

soma hapa mkuu..

http://www.tra.go.tz/images/organisation structure.jpg

wanacho hicho kitengo kabla hata wewe hujazaliwa enzi ya kibanga ampiga mkoloni....shida ni kuwa wanafanya nini hao watu chini ya huyo director wa research and policy?
 
Wataalam wetu wengi hawajaelimika vya kutosha na wanasiasa ndio hivyo wengi pia Mbumbumbu sasa nchi inaenda kwa kudra za Mwenzi Mungu tu!
 
Welcome to the Tanzania Robbery Association! bado sina uhakika kama hili linchi lina viongozi na kama wapo ndio nchi ya kwanza Duniani kwa viongozi kuchukia wananchi wake ili wasiendelee! hehehe! . Mafisadi wameona sasa wadanganyika nao wana kiherehere sababu tunaweza kuendesha magari pia sasa wameamua kututuliza ili waendeshe wenyewe na mitumbo yao iliyojaa **** !!!!
 
shida ni kuweka siasa kila pahala..

hata hii thread iko katika jukwaa la siasa ingawa kinachozumgumzwa ni uchumi na jukwaa stahiki la uchumi lipo...

nadhani lengo la TRA ni kuzuia chakachua kwenye CIF price za magari makuukuu kutoka ng'ambo ingawa approach yao si sahihi, si vibaya pia tukiwalaumu na wachakachuaji(wenye kutuma TT mbilimbili au kutumia majina ya watumishi wa serikali ili wakwepe kulipa Import duty wakati magari ni yao...tunawajua na tunajijiua ingawa kama kawaida yetu wabongo hatuwezi kukiri hilo); mi naamini hawa wametuponza kwa reaction hii ya serikali kupitia TRA.
 
Wakuu,hii nchi CCM wameishindwa kabisa.Nape Nnauya anapiga kelele tu.TRA wana afya nzuri sana ukilinganisha na wafanyakazi wa idara nyingine za serikali.Watu wanafurahiya lakini madhara yake ni makubwa sana.Kwanza market value ya magari tanzania hakuna kwa sababu hatuzalishi magara.Pia 70% wameipata wapi?Huu ni ufisadi,Japani barabara ni nzuri na bei zao wanaziweka kuendana na market value ya soko la dunia,sasa TZ viongozi wameshafika mwisho wa kufikiria basi wanakuja na mambo ya ajabu.CHADEMA, mko wapi?Mambo kama haya yasipite.Nimeichukia sana SISIMU.Usafiri lazima uwe juu mara milioni moja.
 
Back
Top Bottom