TRA na Kodi ya Majengo (Property Tax) naombeni ufafanuzi katika hili

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
825
246
Wadau habari za asubuhi,

Kwa wataalamu wa kodi (Tax Consultants) ama watumishi wa TRA, kama nina nyumba eneo halijapimwa na mimi binafsi sina Tax Identification Number (TIN) nawezaje kulipa kodi ya majengo?

Asanteni
 
Jana nimekuta kwenye nyumba yangu wameandika 01/05 WASILISHA KIBALI 16/06/2020 sasa sielewi naanzia wapi, mwenye uelewa tafadhari
 
Wadau habari za asubuhi,

Kwa wataalamu wa kodi ( Tax Consultants) ama watumishi wa TRA, kama nina nyumba eneo halijapimwa na mimi binafsi sina Tax Identification Number ( TIN) nawezaje kulipa kodi ya majengo?

Asanteni
Nenda TRA chukua form ambayo utaenda kujaza na mwenyekiti au mtendaji wa mtaa/kijiji/kitongoji unachotoka ukishaijaza irudishe TRA ukiwa na kopi ya kitambulisho cha uraia.Kitambulisho cha uraia ndio cha msingi.Pia naona hata kama eneo halijapimwa lazima ulipie Jodi ya jengo
 
Jana nimekuta kwenye nyumba yangu wameandika 01/05 WASILISHA KIBALI 16/06/2020 sasa sielewi naanzia wapi, mwenye uelewa tafadhari
Sheria inahitaji uwe na kibali cha ujenzi.Nenda halmaushauri kwenye ofisi ya ardhi ukiwa na ramani ya kiwanja pia utalipia Kibali cha ujenzi sijui kwa sasa itakuwa bei gani mimi 2018 nililipa 50,000
 
Sheria inahitaji uwe na kibali cha ujenzi.Nenda halmaushauri kwenye ofisi ya ardhi ukiwa na ramani ya kiwanja pia utalipia Kibali cha ujenzi sijui kwa sasa itakuwa bei gani mimi 2018 nililipa 50,000

Dah elfu 50 mbona nyingi namna hiyo? Aiseee
 
Nenda TRA chukua form ambayo utaenda kujaza na mwenyekiti au mtendaji wa mtaa/kijiji/kitongoji unachotoka ukishaijaza irudishe TRA ukiwa na kopi ya kitambulisho cha uraia.Kitambulisho cha uraia ndio cha msingi.Pia naona hata kama eneo halijapimwa lazima ulipie Jodi ya jengo
Asante sana sana JAPO JINA LAKO HALIENDANI NA MAJIBUYAKO MAZURI
 
Sheria inahitaji uwe na kibali cha ujenzi.Nenda halmaushauri kwenye ofisi ya ardhi ukiwa na ramani ya kiwanja pia utalipia Kibali cha ujenzi sijui kwa sasa itakuwa bei gani mimi 2018 nililipa 50,000
Nadhani hili eneo TRA walifanyie kazi, mimi niko Namtumbo kijijini huku kibali cha ujenzi napata wapi
 
As long as unataka Kibali utaitoa tu hata ungekuwa unajenga nyumba ya laki 1 na 50 elfu huwezi shindwa kutoa 50 elfu ya Kibali chief

Sasa kwa wale ambao tumejenga na tumeishi karibia miaka minne , leo ndo wamejua kama kuna watu wanaishi huku? Kipindi chote walikuwa wapi
 
Sasa kwa wale ambao tumejenga na tumeishi karibia miaka minne , leo ndo wamejua kama kuna watu wanaishi huku? Kipindi chote walikuwa wapi
Ishu si walikuwa wapi,sheria zimeshawekwa ukijijua unataka kujenga lazima ukaombe Kibali cha ujenzi kwa kukushangaza zaidi sheria haitambui iwapo una taarifa au hauna taarifa kuhusu sheria hiyo najua utasema ulikuwa hujui iwapo sheria hiyo ipo,kwa kuongezea kutojua sheria hakukufanyi uiepuke hiyo sheria isikuadhibu
 
Wadau habari za asubuhi,

Kwa wataalamu wa kodi (Tax Consultants) ama watumishi wa TRA, kama nina nyumba eneo halijapimwa na mimi binafsi sina Tax Identification Number (TIN) nawezaje kulipa kodi ya majengo?

Asanteni
MKuu ingia kwenye mtandao wa tra www.tra.go.tz ingia sehemu ile imeandikwa "laws and regulations" utaikuta "regulation" ya property tax ya mwaka 2020 inainisha vizuri namna ya kufanya lakin pia niliona pia kuwa unaweza kufanya usajili kupitia mtandao (online) sasa sina uhakika sana na lugha iliyotumika hapo lakin naweza kusema haya mchache.

Sheria inaonesha kinachohusika ni"property " na tra wanashirikiana na halimashauri kupata taarifa sahihi za" property" itafute hiyo "regulation" uisome itakupa mengi.( samhani kwa kuchanganya lugha ni katika kujaribu kuelewesha)
 
MKuu ingia kwenye mtandao wa tra www.tra.go.tz ingia sehemu ile imeandikwa "laws and regulations" utaikuta "regulation" ya property tax ya mwaka 2020 inainisha vizuri namna ya kufanya lakin pia niliona pia kuwa unaweza kufanya usajili kupitia mtandao ( online ) sasa sina uhakika sana na lugha iliyotumika hapo lakin naweza kusema haya mchache. Sheria inaonesha kinachohusika ni"property " na tra wanashirikiana na halimashauri kupata taarifa sahihi za" property" itafute hiyo "regulation" uisome itakupa mengi.( samhani kwa kuchanganya lugha ni katika kujaribu kuelewesha)
Imenisadiia sana kumbe sio lazima uwe na TIN unaweza tumia hata number simu
 
Kama umeona unastahili kulipa hiyo kodi (property tax), we jongea tu mpaka ofisi za TRA, utawapa taarifa zako na anuani ya makazi, then watakuingiza kwenye mfumo rasmi wa kulipa hiyo prop tax. Kwa kodi hiyo huitaji kuwa na TIN wala hata Hati ya nyumba au kiwanja. Pia hata watakapo kuingiza kwenye mfumo hawakupi TIN number bali wanakupa Tax payer ID na kuanzia hapo utakuwa unatumiwa deni lako kwenye simu yako pamoja na Controll Number ambapo utaweza kulipia hiyo property tax kwa njia ya mtandao bila hata kwendapanga msululu TRA.
 
Gharama yake ni kiasi gani? Au inategemea na nyumba?
 
Back
Top Bottom