TRA mnahusika na wizi huu wa wafanyabiashara Kariakoo?

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,150
1,812
Wadau ninaurudisha tena uzi huu hapa kwenu jamvini huu
Ukwepaji kodi wa wazi kabisa unaofanywa na wafanyabiashara wa kariakoo TRA wanahusika?

Karibu wafanyabiashara wote kariakoo hawatoi risiti za thamani inayofanana na pesa iliyolipwa kwa mzigo husika. Ukiuliza utaambiwa hiyo ni risiti ya kukusaidia njiani tu, kama huwezi rudisha mzigo.

Ukinunua bidhaa zenye thamani ya laki mbili tatu ama tano bado risiti utakayopewa inaweza isizidi thamani ya tsh 40,000.
je hili hamlioni? Ni kweli hamna uwezo wa kufanya uchunguzi? Au nanyi ni wahusika wa uhalifu na ukwepaji huu..?

Mchezo huu upo sana kwa wateja wanao nunua mizigo kwa jumla, hili suala linakera sana kama tumeamua kujenga Taifa letu kila mtu atimize wajibu wake sio mimi nikupe milioni halafu wewe unipe risiti ya 50000.. hili sio sawa TRA timizeni wajibu wenu.
 
Huu mchezo ndio hhufanyika 95% yaa wafanyabiashara wote.

mimi nilikuwa nanuunua blender ya 200,000 nikaomba nipunguziwee mkp 170,000 jamaa Akasema poa ila risiti itaandikwa 80,000 nikamwambiaa poaa mzee, nikabeba mzigo.

Nilifanya hivi kumkomoa Magu coz ajira kabana, pesa kabana kwanini na mimi nisimbannieeee???

mwaafaaa!!
 
Hahahaaaa huoo ujinga awafanyi tra

We unatoanlaki unapewa rst ya hamsini unaondoka nayo TRA aje kukusaidia hapana ....Mkuu watake radhi na kichwa chako cha habari n kuwazalilisha tra...

Kama hutaki unaacha siolazima ununue hamia kwingine ndio uzuri wa krkoo
 
HAHAHAAAA HUOO UJINGA AWAFANYI TRA

WE UNATOANLAKI UNAPEWA RST YA HAMSINI UNAONDOKA NAYO TRA AJE KUKUSAIDIA HAPANA ....MKUU WATAKE RADHI NA KICHWA CHAKO CHA HABARI N KUWAZALILISHA TRA...

KAMA HUTAKI UNAACHA SIOLAZIMA UNUNUE HAMIA KWINGINE NDIO UZURI WA KRKOO
TRA wanashirikiana na watu wa kariakoo kukwepa kodi Rais tunaomba uingilie kati
 
HAHAHAAAA HUOO UJINGA AWAFANYI TRA

WE UNATOANLAKI UNAPEWA RST YA HAMSINI UNAONDOKA NAYO TRA AJE KUKUSAIDIA HAPANA ....MKUU WATAKE RADHI NA KICHWA CHAKO CHA HABARI N KUWAZALILISHA TRA...

KAMA HUTAKI UNAACHA SIOLAZIMA UNUNUE HAMIA KWINGINE NDIO UZURI WA KRKOO
Umeambiwa ni karibu wafanyabiashara wote wa kariakoo wanafanya hivyo.Unataka aache akanunue wapi.Kwa hali ilivyo,inabidi TRA wafuatilie.
 
ile kamata kamata irudi tuu maana mpaka mafuta ya kupakaa yaliyopigwa marufufuku yamerudi kariakoo na woga hamna tena.
 
Acheni umbeya

-pesa ya pango
-pesa ya luku
-pesa ya halmashauri
-pesa ya usafi

Lazima tukwepe kodi ukilipa kila kitu kinavyostahiki utaishia kula tu

Hebu siku fungueni biashara k koo halafu mjionee

Bila umafia utafunga duka mwenyewe
Kodi ya mapato. Kodi ya pango. Kodi ya taka. Withholding tax. City service levy. Kodi ya Leseni. Kwa kodi hizi kweli mfanyabiashara huo uzalendo anautoa wapi? Msizungumze tu mambo msiyoyajua. Kodi zimekuwa nyingi mno mpaka MTU unachanganyikiwa. Nabado hapo kama una nyumba utadaiwa property tax. Kodi ya ardhi. Nabado kama una gari watakuuliza road license, sasa jamani, Mimi mfanyabiashara hiyo hela natoa wapi? Hii nchi INA kodi mpaka inakatisha tamaa kwakweli
 
niliwahi rudisha jokofu hvyo hvyo nilinunua 320,000/= akanipa risiti ya 220,000/=
 
Hujalazimishwa kukubaliana na muuzaji, unahiari ya kukubali unachopewa au kukataa, muuzaji Hana kosa lolote, umempa 100000 kakupa risiti 10000 umekubali, kama vipi kataa kununua rudi home na pesa
 
Hujalazimishwa kukubaliana na muuzaji, unahiari ya kukubali unachopewa au kukataa, muuzaji Hana kosa lolote, umempa 100000 kakupa risiti 10000 umekubali, kama vipi kataa kununua rudi home na pesa
 
Wadau ninaurudisha tena uzi huu hapa kwenu jamvini huu
Ukwepaji kodi wa wazi kabisa unaofanywa na wafanyabiashara wa kariakoo TRA wanahusika?

Karibu wafanyabiashara wote kariakoo hawatoi risiti za thamani inayofanana na pesa iliyolipwa kwa mzigo husika. Ukiuliza utaambiwa hiyo ni risiti ya kukusaidia njiani tu, kama huwezi rudisha mzigo.

Ukinunua bidhaa zenye thamani ya laki mbili tatu ama tano bado risiti utakayopewa inaweza isizidi thamani ya tsh 40,000.
je hili hamlioni? Ni kweli hamna uwezo wa kufanya uchunguzi? Au nanyi ni wahusika wa uhalifu na ukwepaji huu..?

Mchezo huu upo sana kwa wateja wanao nunua mizigo kwa jumla, hili suala linakera sana kama tumeamua kujenga Taifa letu kila mtu atimize wajibu wake sio mimi nikupe milioni halafu wewe unipe risiti ya 50000.. hili sio sawa TRA timizeni wajibu wenu.

Hili ni rahisi tuu, polisi wapewe pesa wakikamata mzigo unaonekana thamani yake ni kubwa kuliko risiti inavyosoma, basi huyo mwenye mzigi arudishiwe pesa inayosoma kwenye risiti aende zake.

Kuna watu tunapigika sana kwenye kulipa kodi sahihi mfano mfanyakazi na washauri (consultants) wanaofanya kazi na sekta rasmi hakuna muamala tunaoweza kufanya bilia kulipia kodi. Serikali itumie mbinu zote ili kila anayestahili kulipa kodi alipe
 
Sura na shape yangu vimekaa ki-ofisa flani japo ni mpoli poili(kwa maelezo ya wanaonifahamu) hivyo mara nyingi huwa napigwa bei za juu kwenye maduka na risiti huwa napewa fasta bila kujadiliana na muuzaji, baada ya kugundua hilo sasa hivi manunuzi mengi ananifanyia dogo na risiti zake ni kama hizo mnazosema: laki tatu wanamuandikia laki na nusu, ila nikiuliza bei ya kitu kile kile naambiwa laki nne! Nimeishakata tamaa na hawa TRA kwanini hawaweki mitego?
 
Wadau ninaurudisha tena uzi huu hapa kwenu jamvini huu
Ukwepaji kodi wa wazi kabisa unaofanywa na wafanyabiashara wa kariakoo TRA wanahusika?

Karibu wafanyabiashara wote kariakoo hawatoi risiti za thamani inayofanana na pesa iliyolipwa kwa mzigo husika. Ukiuliza utaambiwa hiyo ni risiti ya kukusaidia njiani tu, kama huwezi rudisha mzigo.

Ukinunua bidhaa zenye thamani ya laki mbili tatu ama tano bado risiti utakayopewa inaweza isizidi thamani ya tsh 40,000.
je hili hamlioni? Ni kweli hamna uwezo wa kufanya uchunguzi? Au nanyi ni wahusika wa uhalifu na ukwepaji huu..?

Mchezo huu upo sana kwa wateja wanao nunua mizigo kwa jumla, hili suala linakera sana kama tumeamua kujenga Taifa letu kila mtu atimize wajibu wake sio mimi nikupe milioni halafu wewe unipe risiti ya 50000.. hili sio sawa TRA timizeni wajibu wenu.
Ndomana mwanafalsafa mmoja alishasemaga umaskini wa nchi zinazoendelea kama tanzania unasababishwa na sisi wenyewe,,sas kweli unaiba mpka kodi si hatari hiii??ila poa tu mana tumezoea kuwa wamwisho freshi tuuuuuuuuuuu,,,wcha tunyonywe mpk basi
 
Back
Top Bottom