TRA mmekuwa chanzo kikubwa cha vijana wengi kufeli maisha

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Asilimia 70 ya vijana wengi waliomaliza chuo na shule ambao hawakupata nafasi ya kuajiriwa wengi siku hizi wamejiingiza katika biashara hii ikiwa kama plan B.

Sasa shida inakuja kwa hawa TRA mmetuwekea kodi kubwa pale mnapokuja kukadiria biashara na kodi unayotakiwa kuilipa kila siku madukani mnatusumbua faini ndogo ndogo zimekuwa ni nyingi sana imefikia hatua watu biashara wamefunga.

Kuna wengine ndo kwanza vijana biashara ndo tumeianzaa lakini mnatukaba sana vijana tutashidwa kutoka kimaisha.

TRA kuweni na huruma
 
Ungeandika kwa herufi ndogo ingekuwa na hamu ya kuusoma uzi wako mpaka mwisho,jifunze pia kulipa kodi hata kama inauma.
 
waanzishe kitengo maalumu cha kulea wqfanyabiashara wadogo wenye maono makubwa kwa kuwapa likizo za kodi kwa kipindi flani huku wakiwasaidia kwa ushauri pia ili wasife.

ifikie kipindi tusikia mtu anatumbiliwa, kwa kusababisha biashara ambazo hazikupaswa kufa zinakufa kisa umakini mdogo juu ya kodi na uhalisia wa mtoa kodi.

hili ni eneo ambao tra wanapaswa kuja na ufafanuzi na mpango kabambe kufanya reformation ambayo watakusanya kodi bila biashara kusinyaa hadi kifo.
 
dah ni kweli mkuu hawa jamaa wanasumbua hadi vijiwe vya kuoneshea mpira mtaani
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom