tra/ majembe auction wamedundwa

kajunju

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
999
315
maofisa wa tra na majembe auction leo mchana wamedundwa na madereva tax hapa kasulu mjini. baada ya maafsa hawa kuikamata gari na kuanza kumpa kichapo dereva. Kwa kuwa leo ni siku ya soko na dereva huyo alikamatiwa maeneo ya sokoni?basi umati wa uliokuwa sokoni kwa kushirikiana na madereva wa tax wamewadunda sana hawa maafisa. Zoezi limeendeshwa kwa wk kama 3 huku maafisa hawa wakichukua rushwa za waziwazi. Maddereva wanne wa tax issa,hamis,mwambata na semeni wamewekwa korokoroni hadi sasa.ushenzi unaofanywa na hawa majembe kwa kushirikiana na dereva wa tra hapa kasulu ni mkubwa. Wakikuta umepark gari wao ni kuifunga kamba na kuiburuta kama vile inapelekwa dampo.
 
Na pikipiki ya afisa mmoja wa serikali iligongwa na teksi iliyokuwa inafukuzwa na tra wakati wa tukio hilo. Afisa huyo anafikiria kuwachukulia hatua wahusika waliogonga pikipiki yake
 
.....''rushwa ni adui wa haki'' nawapa pongezi wote wanaokinzana na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa ila watu wanaokuchukua sheria mkononi siwaungi mkono.
 
Ndio wakome kuwafuata dereva wa bodaboda kuwaacha kina wazee wa vijisenti na wazee wa "juice" wakitamba
 
vijana walioshikiliwa wamenyimwa mdhamana. Biss wa tra hapa hana tatizo ni mhelewa ila awa majembe na baadhi ya matapeli toka tra kgma ndio wamepondwa.tra, polisi, uhamiaji bado hawajajua jinsi ya kuongea kushawishi watu ili mtu kama ana makosa ajipeleke mwenyewe; wanachi wanaaapply kauri ya pinda 'wapigwe tu'
 
tujuzeni kila kinachojiri pande hizo maana wananchi wamechoka sasa
 
wale vijana waliokuwa wanashikiliwa na polisi badae wakaweka gerezani kwa sababu eti ya kuwapga tra/majembe auction?wametolewa leo korokoroni. Polisi walifanya ukatili kwani wa kuwakomoa vijana hawa. Bifu la mitaani kati ya madereva na polisi limeenda hadi kwenye issue hii. Mungu wape nguvu madereva hawa kupigania haki na amani na walahumu/walaani polisi waliotaka kuwanyima haki ya msingi vijana hawa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom