maofisa wa tra na majembe auction leo mchana wamedundwa na madereva tax hapa kasulu mjini. baada ya maafsa hawa kuikamata gari na kuanza kumpa kichapo dereva. Kwa kuwa leo ni siku ya soko na dereva huyo alikamatiwa maeneo ya sokoni?basi umati wa uliokuwa sokoni kwa kushirikiana na madereva wa tax wamewadunda sana hawa maafisa. Zoezi limeendeshwa kwa wk kama 3 huku maafisa hawa wakichukua rushwa za waziwazi. Maddereva wanne wa tax issa,hamis,mwambata na semeni wamewekwa korokoroni hadi sasa.ushenzi unaofanywa na hawa majembe kwa kushirikiana na dereva wa tra hapa kasulu ni mkubwa. Wakikuta umepark gari wao ni kuifunga kamba na kuiburuta kama vile inapelekwa dampo.