TRA kwanini Wamehamishia akaunti ya malipo KCB, siyo tena NMB? Ni ufisadi baada ya Magufuli?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,847
2,000
TRA na BOT watajitetea kwa sababu zozote zile lakini sisi tunaolipa kodi ktk nchi hii, kwa kujua nani anamiliki KCB (Kenya Commercial Bank) hii ni chini ya kiwango cha uzalendo uliohubiliwa miaka mitano iliyopita. Nalinganisha malipo niliyofanya 2020 na mwaka huu, yakielekezwa benki tofauti kabisa!!

Tunafahamu ni Benki iliyosajiliwa hapa nchini lakini pesa ya kodi za serikali kupitia benki ya muwekezaji wa nje badala ya NMB ambako serikali ina hisa, ni ufisadi. TRA wanafidika nini kuitumia KCB? Imetokea nini baada ya kifo cha Magufuli? Je, KRA ya Kenya, kwa ubaguzi wao kibiashara, inaweza kupitishia pesa za kodi za serikali yao benki ya TZ, hata kama imesajiliwa nchini Kenya?

View attachment 1926663

View attachment 1926664

Itakuwa tunadumisha undugu na wakenya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom