TRA kwanini mnawanyanyasa wafanyabiashara kiasi hicho?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
TAR kwanini mnawanyanyasa wafanyabiashara kiasi hicho? Kama kuna mfanyabiashara ambaye hana ugojwa wa moyo kwa sasa hivi nchini Tanzania sijui!

Ni kosa gani kubwa kiasi hicho wafanyabiashara wa nchi hii wamekosa? TRA kwa sasa ni mwendo wa faini ya 3 ama ufilisiwe tu, hakuna maelezo mengine, ukitaka lipa hutaki biashara inafugwa,hakuna maelezo, ukipigwa faini unapewa siku 7 tu ulipe, huna pesa utajuta kuzaliwa

Mh. Waziri wa fedha ni nini hiki? Damu zinavujia tumboni kwa wafanyabiashara tatizo liko wapi?Kama kuna makosa mtusamehe, la sivyo nchi hii itabaki na masikini tupu
 
Leo wakiongozana na viongozi wa kisiasa hapa Iringa wamevamia duka la mfanyabiashara mmoja wakiwa na askari kadhaa wenye bunduki. Sasa unajiuliza haya mabunduki ni ya nini kwenye kukusanya kodi?
 
Tar kwanini mnawanyanyasa wafanyabiashara kiasi hicho?Kama kuna mfanyabiashara ambaye hana ugojwa wa moyo kwa sasa hivi nchini tanzania sijui
Ni kosa gani kubwa kiasi hicho wafanyabiashara wa nchi hii wamekosa?Tra kwa sasa ni mwendo wa faini ya 3 ama ufilisiwe tu,hakuna maelezo mengine,ukitaka lipa hutaki biashara inafugwa,hakuna maelezo,ukipigwa faini unapewa siku 7 tu ulipe,huna pesa utajuta kuzaliwa
Mh,waziri wa fedha ni nini hiki?damu zinavujia tumboni kwa wafanyabiashara tatizo liko wapi?Kama kuna makosa mtusamehe,la sivyo nchi hii itabaki na masikini tupu
Hamna jinsi.Nia ni biashara zote zifungwe.[HASHTAG]#Wote[/HASHTAG] kuishi kama mashetani.
 
Lipa kodi yao. Hutasumbuliwa.
Ndugu yangu kuwa na roho ya nyama,hawa walipa kodi kidogo waliopo nchini wanahitaji utu,ni binaadamu ndugu yangu?lazima pawepo na urafiki kati ya mlipa kodi,na mtoza kodi,lkn usisahau mm nawazungumzia wafanyabiashara wa ngazi ya chini wenye maduka mtaani ndio wanakutana na hizo faini ndugu yangu
 
Leo wakiongozana na viongozi wa kisiasa hapa Iringa wamevamia duka la mfanyabiashara mmoja wakiwa na askari kadhaa wenye bunduki. Sasa unajiuliza haya mabunduki ni ya nini kwenye kukusanya kodi?

ma bush laywer kama nyie msipobebewa na bunduki si mtajifanya wajuaji. tulien dawa iwaingie
 
Nyerere nchi yeyote isiyo kusanya kodi,nchi yenye rushwa huwa haikusanyi kodi,inakimbizana na wafanyabiashara wa maduka ya mtaani
Hatimaye unabidii wa nyerere umetimia
 
Pengine inewezekana mh,rais hajui kama wafanyabiashara wa maduka madogo huku mtaani manzense na mwenge wanalimwa faini kubwa kubwa sana,kwa kisingizio cha hapa kazi tu
 
Hii kauli mbiu ya hapa kazi tu wafanyakazi wa tra hasa tawi mwenge wanaitumia vibaya sana,mh makamu wa rais aliwai kukemea tabia hii
 
Ukipigwa faini milion 3 ukitaka usilipe inabidi utowe rushwa ya sh milion moja au lk 8 tutafika kweli?
 
Hivi ni kweli hata kama tra wanania nzuri ya kukusanya kodi hawezi kufanya utafiki wakajua nani wampige faini ya 3 au wasimgie faini kweli?
 
Vitisho,na personal deals nyingi,baadhi wanatumia fursa ya hapa kazi.
 
TRA irudishe mfumo wa sales tax kwa kila mfanyabiashara apangiwe kwa mwezi atoa kiasi gani kama kodi ya mauzo.
EFDA Machine ni usumbufu na imeongeza masuala rushwa kwa watumishi wa TRA Kodi za Ndani
Fanya hesabu kama kila mfanyabiashara mdogo atatoa sh 20000 kwa mwezi kama kodi ya mauzo Fixed serikali itapata shilingi ngapi
Serikali ipange maduka kwa madaraja iwepo Class A Class B Class C Class D na hizo kodi za sales tax zitolewee kufuatana na mtaji/aina ya biashara na iwepo kitengo cha Investigation kuchunguza ulipaji wa kodi unakuwa sahihi. Hapo bado serikali itawekea kiwango cha kutoza gari za biashara pia kila mwezi.
EFDA Machine ni hasara kwa serikali na wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom