super nova
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 1,479
- 1,095
naskia Yanga wazimendea hizo nyasi..
Wewe jamaa nimekupenda bure. Umeongea hoja perfect kabisa. Humu JF kuna watu wa ajabu sana, haya ma-vilabu ya Yanga na Simba hayapaswi kupewa misamaha ya kodi. Ni mtu mjinga pekee atahoji ni kwanini. I wonder watu wanatetea kumbe wanaongozwa na upenzi, hisia hasi, n.k.Mpira bongo unalipa sana.. Viongozi wengi wa michezo kuanzia kwenye vyama mpaka vilabu wanatajirikia sana kwenye tasnia hii ya mpira.. Sasa kama unalipa wanapaswa kulipia kodi sahihi katika vifaa vya michezo ambavyo vinaingizwa nchini.. Haya mambo ya kuomba kutolipa kodi kwenye vifaa hivyo, halafu baadae unakuta viongozi hao walienda kuomba kuondolewa kodi wanazidi kuwa matajiri, hayakubaliki hata kidogo..
Tuweke unazi pembeni, Simba wakalipe kodi.. Aveva & co mnajua mnavyotajirika kupitia Simba, oneni aibu kidogo..
kuna mtu atayanunua hayo?
Yanga, ili waweke kaunda stadium labda zitasaidia kupunguza mafuriko!kuna mtu atayanunua hayo?
They dont think straightMsiwe na wasi wasi, Simba watafute hela ya Kaisari taratibu tu, nani atanunua nyasi bandia ikiwa hana matumizi nazo?
La pili hili ndio funzo kwa kina tantalila kuwa mabaya hayana mpaka. Imeshindikanwa nini serikali kuiachia Simba Koko majani yake (ukizingatia simba hali majani) halafu kodi ikakatwa kidogo kidogo.
Anyway, wauze tu, maana hata simba yenyewe bandia (kidding)
View attachment 488763 View attachment 488761 View attachment 488759
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imethibitisha kuwa nyasi bandia za klabu ya Simba zilizopo bandarini zitapigwa mnada endapo Simba watashindwa kulipa kodi wanayodaiwa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema Simba pia wananafasi ya kuzipata nyasi hizo endapo watalipa kabla ya tarehe ya mnada.
Kwa taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange amesema “Ni kweli nyasi hizo zimezuiliwa na sababu ya kushindwa kulipia ushuru TRA pamoja na kuomba msamaha serikalini walikataa kufuta ushuru huo.”
Kwa upande wake Kampuni ya ya Udalali ya Majembe (Majembe Auction) wamesema kuwa watazipiga mnada endapo Simba watashindwa kulipa ushuru hadi kufikia tarehe ya mnada.
"Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart inataka kupiga *mnada* nyasi bandia za SIMBA SPORTS CLUB na magoli yake, sababu kubwa ni uongozi (wamiliki) kushindwa kuzilipia *kodi*.
Mnada utafanyika Eneo la Nyuma ya "The Waterfront Sunset Restaurant and Beach Bar", barabara ya Yatch Club, Masaki, ofisi mnada utakaofanyika zinaitwa *LW9*.
Maoni ya mwandishi:
Kama hili litatokea leo basi ni simanzi si kwa Simba tu bali familia nzima ya soka nchini.
Kabla ya kuutupia lawama uongozi wa Simba SC kwa kushindwa kutafuta njia mbadala za kutafuta fedha za kulipa kodi za nyasi hizi? Serikali kwa wizara yenye dhamana ya michezo na shirikisho la soka nchini iliwapasa kuwasaidia Simba SC katika hili hata kwa mkopo au dhamana fulani katika ile sera ya kuendeleza michezo nchini.
Tukirudi kwa uongozi wa Simba kama mlifikia kukwama kiasi hiki , si mngepitisha bakuli kwa wanachama wenu na wadau wa soka nchini ?! Hili suala lisiwe la aibu maana hizi timu ni za wanachama hivyo wana dhamana na timu yao.
Lakini pia huu ni uwekezaji mkubwa kwa Simba SC katika suala la miundo mbinu hivyo lilipaswa kupewa kipaumbele kuliko jambo lolote ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hii kuthubutu kumiliki uwanja wake . Hizo milioni 800 za kutafutia ubingwa si mngewekeza huku???? Daaah

Huyo kwenye bike nani! Aveva?!Hatimaye Simba sports club wamefanikiwa kugomboa nyasi zao
View attachment 489950