TRA, kufungia biashara endelevu ni mbinu ya kizamani

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
2,064
2,301
Nawaasa TRA kuwa kufungia biashara endelevu kwa kisa cha kukusanya malimbikizo yakodi ni mbinu ya kizamani. Badilikeni. Mna wahasibu wengi tu. Kama mnaidai kampuni na bado inaendelea na biashara pelekeni mhasibu wenu aisimamie ili fedha zinazoingia zitumike kulipa kodi inayodaiwa. Wakati huohuo kamouni itakuwa inaendelea na shughuli zake. Mbinu hii hutumiwa pia na mabenki yanapokuwa yanadai marejesho ya mikopo kwa makampuni ambayo hayajafilisika. Itumieni.
 
Ni mbinu nzuri..changamoto zipo kwa pande mbili (Kwa haraka haraka) aidha wadaiwa wamezoea kuwapa kitu kidogo watumishi na baadhi yao hawaambiliki..lakini mbinu ya kufungia biashara hua ni suluhisho la mwisho baada ya maonyo kadhaa!
Deni ni kama usingizi..usipolala utaulipa tu!

Niliwahi shuhudia wakifungia mahali na nilikua sehemu ya wanahabari ilikua scenario mbaya sana hasa kwa wafanyakazi ambao walikua hawana taarifa na baadhi yao wakikosa hata nauli ya kurejea majumbani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom