TRA KUANZA KUWATOZA KODI WANAOFANYA BIASHARA MTANDAONI

Pastory Kimaryo

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
967
664
> Mamlaka hiyo imesema inatambua uwepo wa Watanzania wanaofanya biashara kupitia Mitandao ya Kijamii hivyo wote watakiwa kujitokeza ili wapewe namba ya mlipa kodi(TIN)
 
1545057457175.png


Chanzo: Ukurasa wa Twitter - Swahili Times

My Take
- Je ni vigezo vipi hivyo?
- Kwa anayejua atusaidie
 
Mbona kama jamaa wanaacha tena maswali mengine.

Biashara za mtandaoni zipo za aina nyingi lakini pia kuna ambao wanafanya biashara ya kuuza physical product lakini pia ni walipa kodi ila mitandao ni kwa ajili ya kujitangaza.

Na hiyo pia inakaaje?

Na pia sifa za mlipa kodi ni zipi maana kuna biashara ambazo zinahusisha digital products(eg ebooks) ambazo unaweza kuanza na zero capital.

Kwa huyo kwa mtu ambaye hatokuwa na uwezo wa kulipa kodi mwanzoni(hasa digital product) hatoruhusiwa kufanya biashara mtandaoni au akifanya atakuwa amekiuka sheria?

Dah hii nchi bhana. Niliona mtandao kama mbadala wa kusaidia watu wasiokuwa na mtaji ila sasa naona wavurugaji wameingia.
 
Back
Top Bottom