TRA, Kodi zinaibiwa sana Kariakoo

Sep 4, 2016
44
28
Leo ni mara ya tatu kununua vitu kariakoo na kupewa risiti ambayo haionyeshi makato ya TRA au VAT. Ukinunua kitu chochote unapewa risiti ila haina makato hata kidogo.

Nilipo wauliza mbona haionyeshi makato ya serikali wakajibu eti mashine zao zimesamehewa mpaka mwaka ujao wa fedha ndio zitaanza kuonyesha makato ya serikali. Nikawambia akisikia neno hilo Raisi Magufuli anaweza kulia hazalani.

Hata humu tunaibiana?. Kodi zetu wenyewe? achana na madini, hata kariakoo.?. Siku nyingine nilienda kwenye supermarket ninunua bidhaa nilipo omba risiti wakasema machine zao hazifanyi kazi, nilishangaa sana. Au kuna mtu anamtandao wa wizi??
 
Kweli kabisa hata mimi nishakutana na risti za namna hiyo mara nyingi sana hawa TRA wajitathimini, sioni kwanini wameshindwa kuwakamata hao wezi wakati ni virahisi kabisa.


Mara utasikia bei niliyokuuzia haina VAT kama unataka risiti itabidi uongeze pesa, huu uhuni upo sana hata huku Arusha.
 
Katika máshne Za efd kuna bidhaa ambazo zinatozwa vật na ambazo hazitozwi.... Bidhaa ambazo hazitozwi huwezi kuona vật value... Pia kwa wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na vật hawâna u wezo wa kucharge vật.... Kwa hao usitegemee pia âkikuuzia kitu risiti itaandikwa vật value... Hivyo kwa wafanyabiashâra wa kati na wadogo risit zao haziwezi kuonyesha vật value.... Cha msingi ni kuhakikisha ủnapewa risit yenye bei halali yan kâma umetoa èlf 20000,risit iandikwe 20000.na iandikwe idadi na jina la bìdhaa.
Pia Risit iwe na jina na anuani ya muuzaji.
Nimeshare uelewa wangu
 
Vijijin huku tra wanakaba mpaka shida. Vibati viwili tu umepakia kwenye baskel wanakusimamisha. Kumbe uko mjin mambo mazur tu
 
Back
Top Bottom