TRA kodi ya jengo na Withholding Tax zinatakiwa ziwe na uamuzi sawa

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,587
22,185
Withholding Tax ni kodi anayolipishwa mpangaji kwa niaba ya mwenye nyumba kwa kigezo cha urahisi wa kuikusanya kupitia mpangaji!

Na TRA ikimshauri mpangaji amdai mwenye nyumba ili amrejeshee alicholipa! Je, hili linawezekana? Hapana, huku ni kuporwa kwa kulazimishwa.

TRA inapokuja na kauli tata kuwa mwenye nyumba alipie kodi ya jengo kwenye nyumba anayaishi mpangaji na huenda ni serikali ndiye mwenye nyumba!

Utata mwingine, mpangaji atanunua umeme na kutozwa hiyo kodi, je serikali itamrudishia pesa yake? Na kama TRA inavyodai alipe mwenye nyumba kwanini isidai pia Withholding Tax alipe mwenye nyumba badala ya kumtwisha mzigo mpanganji?
 
Hii nchi tuishi tu hivi hivi na naanza kuliona tatizo lilipoanzia kama si kwa Julius basi kuna mitishamba walifanyiwa wazazi wetu wa kipindi chake.

Maana si kwa madudu kama haya na tunashangilia kama mazuzu.

How come serikali inafahamu wananchi wengi wamepanga na ndiyo wanunuaji wakubwa wa LUKU na si wenye nyumba, leo mzigo huo tunaoambiwa ni mdogo kabebeshwa huyo mpangaji?.
 
Withholding Tax ni kodi anayolipishwa mpangaji kwa niaba ya mwenye nyumba kwa kigezo cha urahisi wa kuikusanya kupitia mpangaji! Na TRA ikimshauri mpangaji amdai mwenye nyumba ili amrejeshee alicholipa! Je, hili linawezekana? Hapana, huku ni kuporwa kwa kulazimishwa. TRA inapokuja na kauli tata kuwa mwenye nyumba alipie kodi ya jengo kwenye nyumba anayaishi mpangaji na huenda ni serikali ndiye mwenye nyumba! Utata mwingine, mpangaji atanunua umeme na kutozwa hiyo kodi, je serikali itamrudishia pesa yake? Na kama TRA inavyodai alipe mwenye nyumba kwanini isidai pia Withholding Tax alipe mwenye nyumba badala ya kumtwisha mzigo mpanganji?
Dhamira Ni hii
IMG_20210821_145411.jpg
 
Nchi ya kibabe hii,Kodi ya mtu mwingine analipishwa mwingine kibabe
 
Hii nchi tuishi tu hivi hivi.
Miaka miwili iliyopita niliwahi kuweka Post hapa ikihusu Withholding Tax kutozwa mpangaji lakini watu hawakunielewe, sasa kinachotokea ni kilekile tofauti ni majina tu kwani kodi zote mbili ni za jengo moja.
 
Withholding Tax ni kodi anayolipishwa mpangaji kwa niaba ya mwenye nyumba kwa kigezo cha urahisi wa kuikusanya kupitia mpangaji! Na TRA ikimshauri mpangaji amdai mwenye nyumba ili amrejeshee alicholipa! Je, hili linawezekana? Hapana, huku ni kuporwa kwa kulazimishwa. TRA inapokuja na kauli tata kuwa mwenye nyumba alipie kodi ya jengo kwenye nyumba anayaishi mpangaji na huenda ni serikali ndiye mwenye nyumba! Utata mwingine, mpangaji atanunua umeme na kutozwa hiyo kodi, je serikali itamrudishia pesa yake? Na kama TRA inavyodai alipe mwenye nyumba kwanini isidai pia Withholding Tax alipe mwenye nyumba badala ya kumtwisha mzigo mpanganji?
Treatment/Collectability ya WHT on rental ina ukakasi sana, ni matokeo ya kuwa na wasomi wachache bungeni
 
Tofauti na tozo za miamala, ambayo imekosa logic kabisa...kwa hili la LUKU nadhani mimi naweza kuwa na maoni tofauti.

Tukumbuke hapa lengo ni kuzifikia nyumba nyingi kadri iwezekanavyo, na kupitia mita za umeme nadhani imeonekana kama ni moja ya mbinu bora kwa sasa.

Nadhani kama yupo Mwenye ushauri mbadala wa jinsi ya kuzifikia Nyumba nyingi hata kama si zote basi atoe ushauri huo kwa Mamlaka.

Hili la kusema kwamba atalipishwa Mpangaji bado sioni athari zake kihivyo, unless kama ingekuwa kodi inalipishwa mara mbili...yaani Mpangaji na Mwenye Nyumba wote wanakatwa.

Sasa hata kukosa masikilizano kati ya Mwenye Nyumba na Mpangaji wake mnataka serikali ifanye nini? Kila nikijaribu kuitafuta logic ya Uma kwa kweli bado naona serikali wanashinda kwa pointi.

Kwa nini Nyie Wapangaji msiungane kuhakikisha mnarekebisha mikataba yenu na Wenye nyumba kuweka kipengele ambapo iwapo Mpangaji atakuwa anakatwa hiyo kodi bila Mwenye Nyumba kuhusika, basi mwisho wa mkataba Mpangaji atapunguza kiasi chote alicholipia Nyumba hiyo kwenye malipo ya mwishoni wa mkataba?.

Mimi warekebishe tu kule kwenye miamala ila huku kwenye Majengo sina shida, na ninaenda kulipa kabisa hiyo 12000 ili wasikate huku kwenye luku..12,000 kwangu imekaa haki kabisa.

Labda kama nitakutana na sababu nyingine zitakazonifikirisha tofauti lakini so far naunga mkono mfumo huo.
 
Tofauti na tozo za miamala, ambayo imekosa logic kabisa...kwa hili la LUKU nadhani mimi naweza kuwa na maoni tofauti.

Tukumbuke hapa lengo ni kuzifikia nyumba nyingi kadri iwezekanavyo, na kupitia mita za umeme nadhani imeonekana kama ni moja ya mbinu bora kwa sasa.

Nadhani kama yupo Mwenye ushauri mbadala wa jinsi ya kuzifikia Nyumba nyingi hata kama si zote basi atoe ushauri huo kwa Mamlaka.

Hili la kusema kwamba atalipishwa Mpangaji bado sioni athari zake kihivyo, unless kama ingekuwa kodi inalipishwa mara mbili...yaani Mpangaji na Mwenye Nyumba wote wanakatwa.

Sasa hata kukosa masikilizano kati ya Mwenye Nyumba na Mpangaji wake mnataka serikali ifanye nini? Kila nikijaribu kuitafuta logic ya Uma kwa kweli bado naona serikali wanashinda kwa pointi.

Kwa nini Nyie Wapangaji msiungane kuhakikisha mnarekebisha mikataba yenu na Wenye nyumba kuweka kipengele ambapo iwapo Mpangaji atakuwa anakatwa hiyo kodi bila Mwenye Nyumba kuhusika, basi mwisho wa mkataba Mpangaji atapunguza kiasi chote alicholipia Nyumba hiyo kwenye malipo ya mwishoni wa mkataba?.

Mimi warekebishe tu kule kwenye miamala ila huku kwenye Majengo sina shida, na ninaenda kulipa kabisa hiy0 12000 ili wasikate huku kwenye luku..12,000 kwangu imekaa haki kabisa.

Labda kama nitakutana na sababu nyingine zitakazonifikirisha tofauti lakini so far naunga mkono mfumo huo.

Una mawazo sahihi. Nia ya serikali ni kupata tozo katika majengo wakiamini LUKU nyingi ziko kwenye majengo!

Sioni mpangaji au anayetumia LUKU akikwepa mzigo huu. Mlaji wa huduma ndio hulipa tozo na gharama zote. Wenye nyumba sasa wataandika mikataba itayoonesha au ongezeko la kodi kwa shiling 12,000 ili wakazilipe mara moja na zisionekane kwenye LUKU katika mwaka husika. Au kodi itabaki palepale na mpangaji kulipa kiasi hicho kupitia manunuzi ya umeme. Either way, hakuna net gain or loss kwa yeyote!!

Wasiwasi wangu ni kama hii inayoitwa tozo ya jengo imeunganishwa kwa kila kiwanja au jengo lililosajiliwa (ambalo linaweza kuwa moja kwa msingi wa hati kiwanja au hati ya ujenzi) au kila mita ya LUKU katika jengo hilo moja kuchukuliwa ni jengo in its own rights. Fikiria mita tano ambazo jumla yake kwa mwaka ni 60,000 na wapangaji watarajie mwenye jengo apunguze tu kiasi hicho kutoka koafi za wapangaji?? Katika baadhi ya sehemu katika nchi hii - hiyo ni sawa na kumpangisha mtu miezi kadhaa bure!! Itakuwa pia sio sawa kwa nyumba moja kulipa 12,000 na nyingine ya namna hiyo kulipa 60,000 kwa kuwa tu na idadi tofauti ya mita za LUKU.

Nadhani kuna kosa kuita tozo hii eti ni ya jengo. Ingeitwa ni tozo kama service charge ya kuwa na mita ya LUKU ingependeza. Sawa na ilivo kwa mita za maji au account benki ambapo kuna kuna tozo pia.

Nadhani kuna udhaifu katika messaging kwa upande wa serikali. Jambo hili hakikupaswa kuwa lilivokuwa!!
 
Najaribu kuelewa kiasi, ila bado naona kwa kuwa hakuna mbinu mbadala ya kurahisisha hili tupambane nalo mpaka likae sawa.

Ni kweli kutakuwa na changamoto kwa kuwa zoezi limeanza katikati ya ilivyozoeleka, lakini wenye nafasi nzuri ya kuweka mambo sawa ni Tanesco maana wao huwa ni lazima wanafika kwenye nyumba husika kabla ya kusimika mita yao, hivyo wanakuwa na taarifa na picha halisi ya Jengo.

Iwapo mita waliyoitoa ni kwa ajili ya chumba/vyumba basi waweke utaratibu wa kuitambua ile mita kuu itakayolipishwa au la kiwango cha kodi(sh 12000) kigawanywe kwa kila mita iliyopo kwenye vyumba vya eneo/plot.

Yaani bado kufanikisha hili kunahitajika ushirikiano wa Wenye nyumba, Tanesco na serikali...kabisa siioni busara ya kutumia nguvu kubwa kukwepa 12000 kwa mwaka.

Na tusisahau hii sio kodi mpya, tumekuwa tukilipa tangu awali, sasa itashangaza kama kuna Mwenye nyumba ataigomea kwa kuwa tu imebadilishiwa mfumo wa kulipa.
 
Back
Top Bottom