TRA kimetumika kwa muda mrefu kuwashugulikia wafanyabiashara wenye mawazo tofauti na CCM

SCOOBY DOO

Member
Dec 16, 2013
76
69
Nimeisikiliza hotuba vizuri ya Mhe Rais, nikasikiliza vizuri maswali na hoja za wafanya Biashara na mwisho Nimeona majibu ya Mhe Rais kwa kuwatumbua aliotaka kuwatumbua.

Ni vyema tukajua chombo hiki TRA kimekuwa Ndio chombo ambacho kimetumika na CCM na Serikali kuwashugulikia wafanyabiashara wote wenye uwezo ambao walionekana kuwa kinyume Cha CCM.

Watumishi wengi wa TRA walitumiwa na CCM na Serikali yake kuwapandishia Kodi na hata kuwapa makadilio ya juu wote walionekana sugu na tishio kwa CCM na wakiwa wafadhili wa Upinzani. Ninayo mifano mingi ya baadhi ya wafanyabiashara waliofirisiwa ama kushughulikiwa na TRA kwa sababu za kisiasa.

Kuwaadhibu TRA kwa sababu ya kuwapa makadilio ya juu ni kuwaonea, TRA Kama ilivyo jeshi la polisi wanafuata maagizo ya wanasiasa tu, kama yako matukio yamefanywa na watendaji wa TRA bila wanasiasa kuwatuma basi ni matukio machache Sana na ninadiriki kusema walifanya hivyo kwa kuwa walijifunza na kuona ni fursa kutokana na wanasiasa na Serikali kuwatumia vibaya!!

Nina hakika matatizo ya TRA na hasa ya kuwafungia Biashara au kuwapa makadirio makubwa wafanyabiashara hayatakwisha mpaka pale CCM iache kuwatumia Kama fimbo ya kuwachapia wapinzani wao.

Tunaona wazi huku mikoani namna ambavyo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, RAS, DAS na Viongozi wa CCM wanavyowatumia TRA kuwashugulikia wafanyabiashara wanaopongana kimawazo. Nimewahi kuona mganyabiashara kafirisiwa kwa sababu tu alikataa kuchangia mwenge, wako waliokomolewa kwa sababu ya kukosana na wakuu Kama wakuu wa Mikoa, na TRA Ndio fimbo pekee inayotumika kushughulikia wafanyabiashara, na ninaamini CCM na Serikali hawataacha kuwatumia TRA kwenye udhalimu huu kama ambavyo hawataacha kuwatumia Polisi na vyombo vingine vya Dola.
 
Hiyo iko wazi kabisa, moja ya fimbo kali inayotumia serikali ya CCM ni TRA.
 
It was tool to punish people with different agenda. Now it is their turn. Ndio maana wana kiburi sana
 
Mwanajeshi awapo kwenye uwanja wa vita silaha yake kubwa ni bunduki .

CCM madarakani silaha yake ni JESHI LA NCHI, TAKUKURU, UHAMIAJI NA TRA...
 
Uliyosema ni sahihi kabisa, lakini pia kile kikao kilikuwa ni cha kisiasa. Kumbuka uchaguzi umekaribia na wameanza kuita makundi wanayoyaumiza na yanayolalamika sana ili kusafisha njia. Tuliona wanaitwa Viongozi wa dini, nao wakapewa semina elekezi, sasa wafanya biashara nao wamepewa semina elekezi, Nilimsikia akiwajaza upepo kwamaba anataka mabilionea wawe watanzania, sijui muwe wazalendo, nyie ndio mlionichagua, nyie ndio mabalozi, mara maendeleo yote yanaletwa na nyie, na ahadi za kushughulikia matatizo yao yote na kutoa watu kafara, hii ni kuwafanya waamini na wamchague au wachague chama chake.
wamekuwa enticed na ahadi hewa na security hewa, ila nchini kwetu tunafahamu wajinga ndio waliwao.Na ule mchezo umeanza wa kutumiwa kama toilet paper maana uchaguzi umefika, haya mtayaona sanaaa stay tuned.
 
NATAKA MATAJIRI WAISHI KAMA Mashetani, SASA BAADA YA KUONA MASKINI WANYONGE WANAISHI KAMA Mazombi NDO MA CCM YAMEAMUA KUJA NA PROPAGANDA MPYA. NA BADO SN KAJINYOOSHA MWENYEWE
 
TRA ni kero kubwa kwa wafanyabiashara hata uwalipe kodi kiasi gani wakiamua kukufirisi wanakufirisi tuu na hawapendi biashara ikue wakiamua wanakufungia Account mara leta vielelezo vya manunuzi au utumaji wako wa pesa kwa kipindi chote ulichofanya biashara...
 
tukithubutu kuchagua chama cha upinzani kikaongoza hata kwa muhula mmoja tu, utatosha sana kuifundisha CCM uwajibikaji na HAKI. na tutakua tumefungua mlango wa kuviwajibisha vyama vya siasa kwenye chaguzi, hivyo basi viongozi hawatakua miungu watu tena.
upinzani wanaweza wasilete maendeleo makubwa lakini watatufungua minyororo ya utumwa tuliyofungwa na hii CCM ya mwalimu nyerere.
kwa nguvu ya umma 2020 inawezekana! jiandikishe kisha piga kura bila kukosa, ikibidi hakikisha kara yako inalindwa, your future depends on that one vote.
 
Back
Top Bottom