TRA Kimara imekosa eneo "location" bora?

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
2,671
2,000
Kwako Comm Gen Phd Mhede,

Hii ofisi yetu siye walipa kodi wa Kimara inatukwaza sana.

Kwanza njia ya kuelekea ilipo ofisi za TRA Kimara ni chafu, mbaya madimbwi ya maji n.k

Pili ofisi yenyewe unapoingia getini ni mteremko mkali ambao unaweza leta ajali kwa sie walipa kodi hivyo tukapeleka kodi kwenye matibabu.

Ombi kwako, toa maelekezo ofisi hiyo iwekwe sehemu bora na salama kwa wateja.

Vinginevyo nawapongeza walipakodi wa Kimara kwa kutimiza wajibu zao.

Nawapongeza pia wetendaji wa ofisi ya TRA kimara kwa kujitahidi kutoa huduma nzuri.

Pamoja tunajenga Taifa letu.
 

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,157
2,000
Kwel aise sijui kwann waliweka ofisi pale mahara pamebanana sana na unapoingia mtelemko ule ni hatar mnoo

Na pia pamezongwa sana na maduka duka mengiiiiii........


Hameni bwana ninyi MNA hela jengeni jengo sehemu kubwa ya wazi na pawe na nafasi ya sie walipa kodi tukija tupate chakula na vinywaji huku tukiichangia nchi yetu
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
890
1,000
Wakajenge Luguluruni, wawe karibu na ofizi za Manispaa, Mkuu wa Wilaya ambazo tayari zimekwishajengwa na zinatumika. Hata watu wa Mahakama, jengeni mahakama ya Wilaya ya Ubungo pale Luguruni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom