TRA inaweza, sasa fikirieni lengo la Trilioni 3.5 ifikapo Dec 2021

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,440
Kwa kufikia lengo la asilimia 101 la tr. 2.08 ninaamini kuwa kuna uwezekano wa kufikia lengo la tr. 3.5 iwapo tu mambo yafuatayo yatazingatiwa:

1. Rais alikwisha sema kwa TRA kupanua wigo wa kodi nchini ili kila mwananchi achangie kutokana na Idadi kubwa ya watu ukilinganisha na nchi nyingine kusini mwa jangwa la sahara.Yapo maeneo mengi ambayo hayajarasmishwa kwenye sekta binafsi kulipia kodi.

2. Bado utaratibu wa kutoa na kudai risti za malipo haujazingatiwa vizuri kwenye mfumo wa kodi na wafanya biashara na wananchi. Kuna leakages nyingi za kimapato.

3. TRA waongeze elimu ya mlipa kodi, ushawishi hamasa na kuondoa mianya ya rushwa na kubambika kodi zenye kuchochea rushwa.

4. Sheria ya kodi iangaliwe upya kwa dhumuni ya kuondoa vikwazo, kodi inayotegemea faini zenye mwelekeo wa kufilisi biashara na kuzuia uwekezaji.

4. Majadiliano rafiki na uwazi wa kanuni za ukadiriaji mapato kuongeza ulipaji wa hiari.

5. Wafanya biashara mara kwa mara kutembelewa kwa ajili ya kuona hali halisi ya changamoto ya biashara zao na kushauri.

6. Kuna haja ya kuwafanyia vetting makampuni ya washauri wa kodi kuona ufanisi wa kazi zao. Kuna malalamiko baadhi ya makampuni hayawaelekezi vizuri nini cha kufanya wafanya biashara kuhusu changamoto za biashara na suluhisho kwa mujibu wa sheria ili kuleta uzingatiwaji.

Kwa maoni haya kweli kuna uewzekano wa kufikis tr.3.5 kwa mwezi. Kilichofikiwa bado ni kidog iwapo Uwajibikaji utakuwepo kwa pande zote mbili walipa kodi na watoza kodi kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi.

HERI YA MWAKA MPYA. TUNASHUKURU KWA KUMPATIA RAIS ZAWADI HIYO KWA KUANZIA. ONGEZENI UBUNIFU ILI MWISHO WA SIKU TUJENGE TAIFA LETU.
 
Safi sana halafu anakuja mjinga mmoja anasema Mh. Rais magufuli hafanyi kitu ,
 
Kwa uvamizi na makadirio makubwa kuliko mtaji inawezekana, ukiweka na DPP mbona tunaweza hadi 5
 
Insu sio kwa kiwango gani unakusanya insu na kwa namba inavyotumika-by dotto James from chato
 
Pamoja na kodi kuongezeka kwa wingi wa tozo lakini bado hatuna Mpango mkakati wa kuwainua wafanyabiashara wenye uwezo wa kibiashara kufikia kiwango cha kuwa mabilionea.

Mfano :-
Serikali ilitakiwa ikuze mitaji ya wakina mangi na Wakinga na wafugaji. Hao wapewe Fursa maalumu ya kuandika Proposal za kuanzisha makampuni makubwa. Wapewe Fursa watu 100,000 . Piga Ua galagaza serikali ihakikishe kuwa baada ya miaka 20 hao watu wanakua ni mabilionea wenye uwezo wa kulipa Kodi kwa Mwaka kuanzia Mil. 500 kila mmoja na kampuni yake .

Pawe na makampuni ya Utalii, uwindaji, madini ,misitu, uvuvi, Kilimo, Usafirishaji, Mafuta,Gesi, Ujenzi, Viwanda, Nyumba za kupangisha watu ,Mahoteli, Uvuvi,ufugaji n.k. Serikali isifanye biashara. Yoyote zaidi ya kuwa na hisa tuu.

Baada ya miaka 20 mwananchi mwenye mtaji mdogo na mfanyakazi wa kima cha Chini atalipa kodi isiyozidi 5% tuu.Pato la taifa litakua ni kubwa sana na ajira zitakua ni nyingi sana. Serikali iwekeze kwa wafanyabiashara wenye maono makubwa na iwape mitaji na kuwatafutia Fursa.

Hivi tunaitumiaje Fursa iliyoko Kongo isiyo na amani ya kutosha? Tunaitumiaje Fursa iliyopo Msumbiji,Sudani kusini,Somalia n.k. Tunawapa sapoti gani wafanyabiashara wanaojitahidi kufanya bishara kwenye hizo nchi zenye soko kubwa !! ?

Au tunasubiri waanzishe vibiashara vyao huko kwa kuhatarisha maisha yao na wakishaanza kupata pesa na kuingiza nchini vimitaji vyao basi Mfilisi mkuu TRA anakwenda kuwasambaratisha kwa kodi utadhani ana visa. !!

Tanzania inaweza kuwa nchi Tajiri kabisa Afrika lakini tumeendekeza watumishi wa TRA wenye maslahi binafsi lakini pia serikali isiyo na mawaziri wabunifu zaidi ya kufoka na kutisha watu.

Matokeo yake serikali inapata wakati mgomu kwenye Bajeti yake bila kutegemea matajiri wa nje toka China na Ulaya.
Tuwezeshe watanzania wenye uwezo wa kushindana kibiashara.

Wakina mangi ni kizazi kilichofikia kiwango cha wahindi kwenye biashara kutokana na kuwa walianza biashara karne nyingi kushindana na wageni.

Hao wengine wana uwezo wa kuwekeza kupitia ofisi za umma kwanza mana ni kizazi kisicho na historia ya biashara kuanzia kwenye familia. Ndio maana wengi wakipata mitaji wanawekeza kwenye majengo na mashamba porini na viwanja hata mia lakini sio kuanzisha kampuni.
 
Kwa kufikia lengo la asilimia 101 la tr. 2.08 ninaamini kuwa kuna uwezekano wa kufikia lengo la tr. 3.5 iwapo tu mambo yafuatayo yatazingatiwa:
1. Rais alikwisha sema kwa TRA kupanua wigo wa kodi nchini ili kila mwananchi achangie kutokana na Idadi kubwa ya watu ukilinganisha na nchi nyingine kusini mwa jangwa la sahara.Yapo maeneo mengi ambayo hayajarasmishwa kwenye sekta binafsi kulipia kodi...
Hakuna muujiza wowote ule. Kilichofanyika sasaivi ni hela zote za serikali zinakusanywa na TRA. Kama hadi mamlaka za Ngorongoro na Tanapa na uhamiaji zimenyang’anywa kukusanya mapato ya utalii na imepelekewa TRA hizo figures wala hazishangazi.

Tena utalii ukirudi kwenye hali yake tutakuja kutangaziwa imefikia hata trillion 4 na washamba wakashangaa kumbe hizo hela zilikuwepo tangu zamani.
 
Kwa kufikia lengo la asilimia 101 la tr. 2.08 ninaamini kuwa kuna uwezekano wa kufikia lengo la tr. 3.5 iwapo tu mambo yafuatayo yatazingatiwa:
1. Rais alikwisha sema kwa TRA kupanua wigo wa kodi nchini ili kila mwananchi achangie kutokana na Idadi kubwa ya watu ukilinganisha na nchi nyingine kusini mwa jangwa la sahara.Yapo maeneo mengi ambayo hayajarasmishwa kwenye sekta binafsi kulipia kodi...
Sio ukusanyaji ni tatizo bali biashara. Bila kuongezeka biashara TRA itakuwa inauwa biashara👆 Isije kufika wakati kuwa na biashara ni kero.
 
Ninakubaliana na kanuni ya KODI ni BIASHARA na BIASHARA ni KODI. Kimojawapo kikiathirika mzunguko unakatika. Vinategemeana. maana yake huwezi kukusanya kodi bila kuwepo na biashara za kutosha na zenye faida na ustawi na pia hakuna biashara kama kodi haikusanywi na kuboresha mazingira ya biashara kwa faida tarajiwa!
 
Back
Top Bottom