TRA inanuka rushwa

Madcheda

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
422
69
Wadau wenzangu,nimekua nikifuatilia TIN hapa tra kwa muda wa wiki moja saiv kila siku imekua njoo leo njoo kesho,mara mtandao upo down mara bosi hayupo. Ila leo naona wameamua kunitolea uvivu na kuniomba rushwa wazi wazi. Sasa jamani kama kupata TIN number tu naomba rushwa je ikifika ktk kulipia kodi yenyewe itakuaje??

Nazan mwanasiasa na tra management inabidi wafanye kitu kuhusu hili suala maana kama mambo yenyewe ndo hivi izo target zao za kila mwezi zitakua hazitimii kila mwezi,kama trend zinavyoonyesha saiv
 
Tin number ambazo si kwa ajili ya matumizi ya biashara zinatakiwa kutolewa bure, lakini wenzetu wa TRA Samora wanakuambia utoe shilingi elfu kumi, ukigoma wanakuambia certificate yako ifuate baada ya miezi mitatu
 
Baada ya uchaguzi kupita, ukiomba TIN namba TRA Mwenge kwa ajili ya biashara, wanakukadiria kodi kutokana na biashara ambayo hujaifanya bado wala leseni hujapata, na unatakiwa ulipe kwanza kodi ndipo upate TIN namba ya biashara.
 
Wadau wenzangu,nimekua nikifuatilia TIN hapa tra kwa muda wa wiki moja saiv kila siku imekua njoo leo njoo kesho,mara mtandao upo down mara bosi hayupo. Ila leo naona wameamua kunitolea uvivu na kuniomba rushwa wazi wazi. Sasa jamani kama kupata TIN number tu naomba rushwa je ikifika ktk kulipia kodi yenyewe itakuaje??

Nazan mwanasiasa na tra management inabidi wafanye kitu kuhusu hili suala maana kama mambo yenyewe ndo hivi izo target zao za kila mwezi zitakua hazitimii kila mwezi,kama trend zinavyoonyesha saiv

X-mas hiyo TRA yote imajaa wachaga na lazima waende kwao wakahesabiwe ... ungekwenda baada Febrauary kama hukuwa na haraka nayo maana january watakuwa bado wanashida za school fees kukamuliwa kuko pale pale
 
Baada ya uchaguzi kupita, ukiomba TIN namba TRA Mwenge kwa ajili ya biashara, wanakukadiria kodi kutokana na biashara ambayo hujaifanya bado wala leseni hujapata, na unatakiwa ulipe kwanza kodi ndipo upate TIN namba ya biashara.

dah basi ndo tabia yao maana me nilienda hapo hapo TRA mwenge aise
 
Wako nyuma ya malengo hao!
N a huku kwa barabara trafic nao wamekomaaaaaaaaaaaaaaa
 
Wadau wenzangu,nimekua nikifuatilia TIN hapa tra kwa muda wa wiki moja saiv kila siku imekua njoo leo njoo kesho,mara mtandao upo down mara bosi hayupo. Ila leo naona wameamua kunitolea uvivu na kuniomba rushwa wazi wazi. Sasa jamani kama kupata TIN number tu naomba rushwa je ikifika ktk kulipia kodi yenyewe itakuaje??

Nazan mwanasiasa na tra management inabidi wafanye kitu kuhusu hili suala maana kama mambo yenyewe ndo hivi izo target zao za kila mwezi zitakua hazitimii kila mwezi,kama trend zinavyoonyesha saiv

Pole sana! Ila hiyo bolded ni kama weye ndiyo waomba rushwa
 
TRA wanaboa sanaaaa
Halafu mtu akifanya kazi TRA anajiona malaika kwa kula rushwa na kununua magari na kuyabadilisha kila leo
Tena anakuwa na manyumba na miradi mingi ambayo yeye mwenyewe kwa kuwa yupo TRA hailipii kodi
TRA wanahitaji kusafishwa (Kuchujwa)

Maana kazi zao haziendani na lile bango lao la mission and vision ambalo ukiingia tu reception unakumbana nalo
Embu wizara husika iwamulike hawa watu wa TRA
 
TRA ni university ya rushwa. Hata ukiwa na ndugu yako anakukwepesha ili ujilengeshe kwa mfanyakazi msiyejuana akukamue bila huruma
 
Baada ya uchaguzi kupita, ukiomba TIN namba TRA Mwenge kwa ajili ya biashara, wanakukadiria kodi kutokana na biashara ambayo hujaifanya bado wala leseni hujapata, na unatakiwa ulipe kwanza kodi ndipo upate TIN namba ya biashara.

Majimoto,nijuavyo mimi hawa TRA wanafanyakazi zao kwa mujibu wa sheria za nchi.kodi inayotozwa kabla biashara haijaanza ni makadirio ya awali,baada ya mwaka kuisha kodi halisi inakokotolewa na hapo kodi iliyolipwa mwanzo hupunguzwa.iwapo utakuwa umeombwa rushwa tafadhali wasiliana na takukuru ili watu hao wanataka kuifilisi nchi yetu wachukuliwe hatua sitahili.
 
Msiwaonee TRA peke yao ni nchi nzima inanuka rushwa....... Mahakama, TRA, Bandarini, Polisi, Manispaa, Jiji, Wizarani, Barabarani, Maofisini....... KILA MAHARI RUSHWA NJE NJE
 
TRA ni university ya rushwa. Hata ukiwa na ndugu yako anakukwepesha ili ujilengeshe kwa mfanyakazi msiyejuana akukamue bila huruma
Yalisha nikuta wakati nafuatilia cpaital gain baada ya kununua kiwanja kwa mtu, ni noma, kiwanja nimenunua millioni 10, na manispaa wamefanya evaluation millioni kumi na laki 7, Tra wanakwambia hayo maeneo tunaviwango vyetu, milioni 30 mzee, ambapo hapo ni gaini 10% ni 3m badala ya 1.07m ya awali, hapo sasa ufanyaje ugawane nao, maana wao huwa wanataka waanze kujenga msingi kwa hela yako ni noma.
Ila nashanga watawala ni wote wanaohusika na TRA wako kimya kabisa, sijui huwa wanapelekewa hesabu baada ya nakusanyo.
Mramba ndo alipanyofela mbali kabisa, nashangaa hyu Mkulo naye yupo yupo tu.
 
Msiwaonee TRA peke yao ni nchi nzima inanuka rushwa....... Mahakama, TRA, Bandarini, Polisi, Manispaa, Jiji, Wizarani, Barabarani, Maofisini....... KILA MAHARI RUSHWA NJE NJE
Level mzee zinatofautiana, TRA unaweza ukaacha mzigo wako, ni wabaya pasipo kuwaelezea.
 
Msiwaonee TRA peke yao ni nchi nzima inanuka rushwa....... Mahakama, TRA, Bandarini, Polisi, Manispaa, Jiji, Wizarani, Barabarani, Maofisini....... KILA MAHARI RUSHWA NJE NJE

Its about time we do someting about it maana mtu akiwa na uwezo wa kukuomba rushwa live live mana yake nini hapo?si kwanza hakuna linalofanyika?I think PCCB have to get their acts together kama wanaona wanasiasa hawawawezi kuwakamata waje kuwakamata hawa watu wanaolipwa vizuri makazini kwao yet wanaomba rushwa ya vijisenti kwa uchu wa mali kijinga jinga
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom