TRA inanuka rushwa (tafadhali serikali wachunguze wafanyakazi wa idara hii)

Bongani

Member
Feb 27, 2011
44
18
Wakati TRA ikiongoza kwa kulipa wafanyakazi wake mishahara mizito, lmebainika kwamba Malaka hii inaongoza kwa rushwa nchini. Wafanyakazi wa TRA wamejenga majumba ya kufuru ambayo hayaendani na mishahara yao.

Tunaomba viongozi wa juu wa idara hii kuwachunguza watendaji wao mali walizokuwa nazo kama zinaendana na vipato vyao.
 
Kwani mishahara mikubwa haiendani na ujenzi wa majumba. Au ulitaka waongeze idadi ya vimada mkuu. Heri yao hawazipeleki uswis
 
Weka ushahidi mkuu, taja majina lau ya wachache na maeneo walipojenga/ mali wanazomiliki, usiishie kusema kijumla jumla tu
 
Acha ulimbukeni wewe!!!! Hujui siku hizi mtu ukiwa na mshahara mzuri unaweza kukopa fedha za kutosha kujiendesha huku ukitumia mshahara wako kama dhamana.

Walioanza kazi zamani wataniunga mkono maana kununua gari tu ilikua ishu. Siku hizi waalimu wenyewe wamejipanga na wanamiliki majumba na magari ya Hatari sembuse mtumishi wa TRA?
 
Katiba mpya ndio suluhisho wafanyakazi wote wawe wanachunguzwa,majumba yanayojengwa wamiliki waweke source za fedha zao.
=====================
Ukipata Ujumbe wa chuki matusi futa delete kabisa
=====================
 
TRA ni pango la Rushwa. Mtu aki-import gari ndio ataijua TRA ni chaka la rushwa. Mwezi July mwaka huu kuna mjasiriamali mmoja alikuwa anafuatilia TIN ili aanzishe biashara ( mtaji laki nne), kufika tu TRA akaambiwa atoe laki mbili ili aweze kuipata hiyo namba within hours.
 
Wakati TRA ikiongoza kwa kulipa wafanyakazi wake mishahara mizito, lmebainika kwamba Malaka hii inaongoza kwa rushwa nchini. Wafanyakazi wa TRA wamejenga majumba ya kufuru ambayo hayaendani na mishahara yao. tunaomba viongozi wa juu wa indara hii kuwachunguza watendaji wao mali walizokuwa nazo kama zinaendana na vipato vyao.
  • sio kweli mkuu mishahara yao ni yakawaida tu,
  • kuhusu kuongoza kwa rushwa pia nakataa,kwani ripoti za rushwa nchini zipo wazi idara kama polisi,mahakama,uhamiaji nk ndizo zaongoza sijawahi sikia TRA,wala mtumishi wao kasimamishwa kizimbani kwa rushwa
  • kuhusu kujenga nyumba,hilo jambo la kawaida sana mabenki siku hizo yanotoa mikopo kwa wafanyakazi kwa kutumia hati zao za mishahara,vilevile siku hizi maisha kupambana watu wanafanya shughuli zingine za kujiongezea kipato mfano kilimo na ujasiliamali
mkuu ila kama wewe ni mzalendo kweli unaipenda nchi yako na unataarifa zozote za rushwa ni vizuri ukaripoti PCCB,ukileta hapa jf sidhani kama patakuwa mahali sahii sana maana utaonekana ni mbea,mchochezi na mzandiki.
 
acha ulimbukeni wewe!!!! Hujui siku hizi mtu ukiwa na mshahara mzuri unaweza kukopa fedha za kutosha kujiendesha huku ukitumia mshahara wako kama dhamana.

Walioanza kazi zamani wataniunga mkono maana kununua gari tu ilikua ishu. Siku hizi waalimu wenyewe wamejipanga na wanamiliki majumba na magari ya hatari sembuse mtumishi wa tra?

si kila mtu anakula urefu wa kamba yake??sasa ubaya uko wapi?nadhani kamba yako haina urefu wowote ndio maana unalalamika.
 
Wakati TRA ikiongoza kwa kulipa wafanyakazi wake mishahara mizito,


wamejenga majumba ya kufuru ambayo hayaendani na mishahara yao.
"Wanaongoza kwa kulipwa mishahara mizito lakini majumba wanayojenga hayaendani na mishahara..."

You are not making any sense
 
Wakati TRA ikiongoza kwa kulipa wafanyakazi wake mishahara mizito, lmebainika kwamba Malaka hii inaongoza kwa rushwa nchini. Wafanyakazi wa TRA wamejenga majumba ya kufuru ambayo hayaendani na mishahara yao.

Tunaomba viongozi wa juu wa idara hii kuwachunguza watendaji wao mali walizokuwa nazo kama zinaendana na vipato vyao.
Watu kwa kukariri? Una uhakika kuwa TRA ndio inayoongoza kulipa mishahara mizito kweli? Au wewe ni Mwalimu wa Primary nini? Maana umeaminishwa na kukariri pasipo kufanya utafiti wowote, remember the general rule: No Research No Right to Speak! Rudi ukajipange upya!
 
Wakati TRA ikiongoza kwa kulipa wafanyakazi wake mishahara mizito, lmebainika kwamba Malaka hii inaongoza kwa rushwa nchini. Wafanyakazi wa TRA wamejenga majumba ya kufuru ambayo hayaendani na mishahara yao.

Nadhani red iko compatible na blue au? kama vinapingana tuambie ni kwa vipi
 
Siwezi kuwalaumu TRA kwani mianya ya rushwa imetengenezwa na watunga sheria.Mfano utaratibu wa kukadiriwa kodi unapoanza biasharaa,usipoongea vizuri unalipishwa kodi'halali'ambayo ukipigiwa unaweza kufunga hata biashara.Wafanya biashara wanajua vizuri.Ni kama tu askari wa usalama barabarani,akikutoza sh.10000 badala ya faini halali ya sh.30000 si atakuwa kakusaidia!Hiyo pesa ya faini si ndiyo inaenda kununua mabomu na kulipa posho zisizo na tija kwa wabunge na viongozi?Kama ni barabara zitajengwa tu kwani kuna rasilimali nyingi zinaondokea barabara hizo.Watapitishia wapi magogo na mchanga wa dhahabu?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wakati TRA ikiongoza kwa kulipa wafanyakazi wake mishahara mizito, lmebainika kwamba Malaka hii inaongoza kwa rushwa nchini. Wafanyakazi wa TRA wamejenga majumba ya kufuru ambayo hayaendani na mishahara yao.

Tunaomba viongozi wa juu wa idara hii kuwachunguza watendaji wao mali walizokuwa nazo kama zinaendana na vipato vyao.

Ni nani alikuambia kujenga nyumba au kuwa tajiri kunategemea ukubwa wa mshahara? Kitu cha muhimu ni discipline ya hela tu wala si kiasi cha hela kinachoingia.
Ntakupa mifano:
1. Kuna afisa mmoja wa Benku kuu ya Tanzania analipwa mshahara wa TZS 6M na point kadhaa achilia mbali marupurupu mengine lakini hana hata kibanda cha kwake anaishi kwenye nyumba ya ofisi
2. Kuna mhudumu wa ofisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni anaishi kwenye nyumba yake Mwananyamala tena katika kiwanja kilichopimwa.
3. Kuna msafisha viatu pale posta na fundi saa wanaishi kwenye nyumba za kwao Mbagala ingawa viwanja havijapiwa lakini ni majumba ya maana.

Kwa hiyo mifano michache unasemaje hapo Bongani
 
Last edited by a moderator:
njoo Bongani hujibu hoja,mbona umekimbia?

TRA ni shirika la kawaida kuna mashirika mengi yenye mishahara mizuri kuliko TRA eg. TANAPA.EWURA,TCRA, etc bt kuwahukumu TRA cz watu walshakrem kuwa TRA kuna pesa si kweli tofautsheni kukusanya mapato na kuwa na kipato bnafs ni sawa na kusema teller wa bank ana pesa nyingi sana kwa sababu kwa sku anahudumia wateja/anafanya transaction za zaidi ya M 200
 
mambo kama haya ukiyaongelea utaonekana tu una wivu na majungu, huwa naona kila mtu aishi kama alivyoamua, aliyependa zaidi kuwa fisadi awe, anayependa kuwa mwaminifu awe alimradi uwe kama ulivyoamua. Ila sasa, gharama za hiyo tabia usiikwepe, maana kwa vyovyote tabia yako kama ina afect wengine tarajia wakati wowote reaction kutoka upande unaokuwa affected.
Na pia kuna rule inayotawala tabia na maisha ya mwanadamu, uovu una kikomo, whether watu wanakurudi au (kwa wale waaminio dini), Mungu ana wakati wa kuacha kumlinda mtu mwovu na sio lazima mali iishe, hasha, inaweza ikawepo lakini isikunufaishe, pesa, majumba, magari sio maisha. Wengine wanavyo hivyo vyote lakini hawana amani, hata akijifaragua kuwa yuko bomba deep inside anajua kuwa hana amani, especially akijua ameiba, amedhulumu au njia yoyote ambayo si halali.
unaona watu wengi wanajaribu ku justify uhalali wa kuwa na hizo mali, oh tunakopa, money management, lakini bado hujaona hilo jumba huyo mfanyakazi akuambie amekopa kiasi gani na mshahara wake ni kiasi gani! atasema uongo, mfanyakazi wa serikali umekopa mil 500 and above kujenga nyumba! utazirudisha kwa muda gani wakati kwa mtanzania yeyote hata mwenye mshahara mkubwa kiasi gani, pension yake inafika sh ngapi jamani tusidanganyane?
 
Mugo"The Great";7281933 said:
TRA ni pango la Rushwa. Mtu aki-import gari ndio ataijua TRA ni chaka la rushwa. Mwezi July mwaka huu kuna mjasiriamali mmoja alikuwa anafuatilia TIN ili aanzishe biashara ( mtaji laki nne), kufika tu TRA akaambiwa atoe laki mbili ili aweze kuipata hiyo namba within hours.

Mkuu umenigusa na ni kweli TRA wamezoea sana rushwa jamaa zetu hawa, Juzi nilikuwa njiani natokea Mwanza Njiani nikakamatwa na Traffic MV Licence imeisha ina kama siku tatu hivi, wale traffic wa pale Misungwi wakaning'ang'ania na hatukuelewana nao kwani nilijitahidi kuwaeleza kuwa allowance ya TRA ni mwezi mmoja na bado haujaisha,,hawakunielewa matokeo nikaona watanichelewesha safari yangu then tukamalizana kwa Buku mbili, nikaanza safari mpaka Shinyanga TRA na kabla ya kuingia ndani nikalipia kwa mpesa nikitumia simu yangu kwani nilikuwa na copy ya maelekezo ya TRA, na nilipoingia ndani na kuwapatia ID ya muamala nikaulizwa maswali ya kijinga/kirushwa rushwa yakaanza.. Kweni umelipia Tsh ngapi? nikamjibu Laki nne na kidogo, Gari yako namba Ngapi? Nikamjibu.., Wewe ndio Fulani? Nikamjibu mie sio lakini gari ni ya fulani, alipoona sina mwelekeo wa kutoa chochote akaniambia kaa pembeni na kweli nilikaaa mpaka nikaona miguu inataka kuingia tumboni ikabidi nimwite pembeni na nikaacha kitu kidogo (Msimbazi) nikapewa Sticker nikaendelea na safari yangu, (eg 10000X30=300000/day?), hawa TRA na traffic hawana tofauti kabisa ni mjomba na shangazi baba yao tumbo moja, hivi sasa Mpesa inawatesa sana lakini Wakubwa wa TRA wangeweza kufanya hivyo na kwenye mizigo na Magari nafikiri wengi wataacha kazi hapo Bandarini
 
Back
Top Bottom