TRA inakusanya bilioni 430 kwa mwezi tangu julai 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA inakusanya bilioni 430 kwa mwezi tangu julai 2010

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 13, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA), imesema makusanyo ya kodi hayajashuka kama inavyodaiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitliya, alisema kuwa makusanyo ya kodi nchini yameongezeka kwa asilimia 18 ikilinganishwa na mwaka uliopita wa fedha. Alisema katika kipindi cha Julai hadi Aprili mwaka huu wamekuwa wakikusanya wastani wa shilingi bilioni 430 kwa kila mwezi.

  Alifafanua kiasi hicho ni sawa na asilimia 93 ya makusanyo, ambapo ni pungufu ya asilimia 7 ya malengo yaliyokusidiwa. Alisema mwaka huu wa fedha 2010/2011 wamepanga kukusanya shilingi trilioni 5.24

  Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku (sio Nipashe), Zitto alikaririwa akisisitiza kuwa serikali haina fedha na kudokeza kuwa taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya mapitio ya uchumi ya mwezi Machi mwaka huu, inaonyesha kuwa imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15. Kwamba, Serikali imeshindwa kukusanya kodi kwa asilimia 15 isipokuwa ushuru wa forodha na hivyo haikufikia malengo ya ukusanyaji wa kodi.

  Hata hivyo, hivi karibuni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alikanusha vikali taarifa iliyotolewa kwamba Serikali imefilisika na hivyo kulazimika kukopa kutoka benki za ndani ili kugharamia mahitaji ya mishahara kwa watumishi wa serikali pamoja na posho mbalimbali za wabunge. Mkulo alisema Serikali inalipa watumishi wake mishahara kwa kutumia mapato yake ya ndani na pia ina uwezo wa kugharamia shughuli nyingine pamoja na gharama za kuendesha Bunge.
   
 2. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiii,
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,934
  Trophy Points: 280
  sasa kwa nini maisha yanazidi kuw a duni??
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ndio hapo sasa ivuga huu ni wizi wa wa wazi kabisa wanaudanganya umma
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kipiondi cha ngonjera huwa hakina muda?
   
 6. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  pesa yote hii inakwenda wapi, ama inatumikaje? kumbe sisi sio maskini kabisa!
   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tatizo sio tunakusanya shilingi ngapi, tatizo ni matumizi ya hiyo pesa, ndio maana inasemekana tumefilisika.

  waweke hapa mapato na matumizi ya serilikali tunao ni ngapi wanakula na ni ngapi zinakwenda kwenye maendeleo
  kwa jinsi ninavyo ona kufilisika inawezekana, semina,GYM za vigogo, misharaha ya wabunge, misharaha ya wafanyakazi, posho za vigogo, safari za kikwete, safari za dr bilali, mafuta ya mashangingi ya vigogo nchi zima, wizi wa mafisadi, chai za vigogo (tsh 2 bilion), n.k


   
 8. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kumbe Kale ka-ahadi cha kupandisha mishahara kanatekeleza!
   
 9. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kumbe Kale ka-ahadi cha kupandisha mishahara kanatekeleza!
   
Loading...