Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imenunua mashine 8,000 za kutolea risiti za kieletroniki (EFD), ambazo zitagawiwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.
Meneja wa masuala ya Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, kwamba wafanyabiasha wagaiwe bure mashine hizo.Alisema kuwa mashine hizo ni kati na kati ya 200,000 ambazo TRA imeweka mkakati wa kuzigawa bure kwa wafanyabiasha, ili kudhibiti ukwepaji kodi na kukuza mapato.
Awali akifungua semina kwa Chama cha Walimu wenye Ulemavu (CWUT), Mwangosi alisema mafunzo hayo yamelenga kuwapa elimu watu walio katika makundi maalum pamoja na Watanzania kwa ujumla, ili kufahamu umuhimu wa kulipa kodi.